Ni kama mmeamua kutuaacha wananchi kila mtu ajihangaikie kivyake, kama chama tu tuna uwezo wa kugawa Tshirt, kofia, khanga, vipeperushi, mabango na posho nchi nzima kipindi cha kampeni.. Serikali inashindwa ku-waorganize wafanyabiashara wakubwa na wadau wengine wa afya kushirikiana na serikali tukapata Barakoa bure kabisa kwa kila mwananchi? kama mmeshindwa kwa nini msitoe msamaha wa kodi kwa hizi bidhaa ili zipatikane kirahisi kipindi hiki na kwa bei nafuu angalau ya tsh 500? Angalia sasa watu wanakimbilia kusafiri kurudi kijijini bila kupimwa nyie serikali ni kama hampo, siku si nyingi huko vijijini nako ugonjwa unaenda kutapakaa.. Jamani hivi nini kazi yenu?
Hao migambo na polisi mnaoweka kukamata wasiovaa Barakoa ni wa nini wakati upatikanaji wake bado ni kizungumkuti? Gawa kwa watu halafu wakamate wasipovaa, sio kama mnavyotaka kufanya hivi sasa..,Katibu mkuu wangu bashiru saidia kuwashauri hawa watu maana mpaka sasa raia hawajui wafuate lipi,ummy alishawahi kusema wanaotakiwa kuvaa barakoa ni wale waliopatwa na maambukizi tu juzi makonda kasema watu wavae barakoa hata za vitambaa vya khanga, naibu waziri wa afya akatoa kauli bungeni kwamba kuna barakoa maalum kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya corona sio kuvaa yoyote watu hawajui washike lipi?
viongozi wetu kuweni serious, ni kama mmewatelekeza watanzania na sasa kila mmoja anapambana kivyake..., angalieni hapo kenya tu serikali inagawa hivi vifaa vyote bure, kwa nini sisi? Jamani 😭😭