RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

Bwashee shona Barakoa ya kitambaa!
kuna video na picha zinasambaa mtandaoni, wahuni wanaokota barakoa zilizotupwa wanazifua wanazipiga pasi halafu wanaziuza tena kwa watu... hii ni hatari sana kwa afya na serikali iko kimya tu.
acheni masihara
 
Cc Pascal Mayalla
Njoo ujenge hoja sio kutetea ccm kila Siku/ kwanini mnagawa tisheti za CCM bure lakini Mask mnashindwa.
Asante
P
 
Watu tumevaa barakoa mpaka Harari shepu na design mbalimbali. Kuna barakoa maridadi kuliko za manesi.

Nimeshonesha la kwangu naficha na midevu. Kuna barakoa za vitenge mamaae utapenda na za kanga. Tatizo lipo kweny kuvuta CO2 happooo
 
Leo nimeshuhudia roughly 30% ya watu Kariakoo wakiwa hawajavaa kabisa barakoa, yaani wanaamini kwamba 70% ya watu ambao wao wamevaa barakoa ni mtaahira au wendawazimi of some sort.

Hivi RC anatoa agizo la halali kabisa halafu mtu bila woga anakaidi bila wasiwasi wowote, where is the discipline, why is there no disciplinary action? Huu udhaifu wa serikali kusimamia matamko yake unatokana na nini???!!!

Je, tumsaidie RC mawazo ya adhabu ipi kwa wakaidi, Mboko au faini nzito za papo kwa hapo??
 
Mkuu wale wanaopiga mikelele "miamia dada hapo kamata mchupi huo" wakivaa barakoa matangazo watayatangazaje..?
 
Mkuu wale wanaopiga mikelele "miamia dada hapo kamata mchupi huo" wakivaa barakoa matangazo watayatangazaje..?
Mbona sauti inasikika vizuri tu, maana hao ndio huwa wanarusha mimate mno wakipiga debe
 
Mbona sauti inasikika vizuri tu, maana hao ndio huwa wanarusha mimate mno wakipiga debe
Mi naona wapewe adhabu zote kwa wale wakaidi ila ikitokea mtoto wa kike kakosea halafu ni mzuri mzuri itakuwa afadhali zaidi kama wakiwaleta kwangu nitawavisha barakoa na nitawaelimisha bila hiana.
 
Makonda si mtu wa sifa na jiwe wake?
Basi watangaze kuwa atakayekutwa amevaa barakoa atapewa kilo ya unga papo hapo!
Hapo ndipo watu tutazivaa!
Si wanasema sisi ni "dona kantri"
 
Elimu kwanza ..
Watu bado hawajaelewa sababu waliambiwa mwanzo masks ni Kwa wagonjwa au wahudumu wa afya...

Sasa waelimishwe tena kuhusu masks..watavaa..

Nimeona mtu havai masks lakini ananawa mikono..ina maana elimu ya kunawa imemuingia
Bado ya masks
 
Elimu kwanza ..
Watu bado hawajaelewa sababu waliambiwa mwanzo masks ni Kwa wagonjwa au wahudumu wa afya...

Sasa waelimishwe tena kuhusu masks..watavaa..

Nimeona mtu havai masks lakini ananawa mikono..ina maana elimu ya kunawa imemuingia
Bado ya masks
 
Yeye angesema,Nikimkuta mtu popotepale amevaa barakoa nitampa buku10 hapohapo.Angeona sasa,wengine wange vaa hata mbilimbili ilimladi wapate buku20.
 
Pamoja kwamba maelezo ya jinsi ya kuvaa barakoa yametolewa na yanaendelea kutolewa, nashangaa na kusikitika ninapoona mtu ameivua kwenye mdomo na pua na kufunika kidevu.

Kinachosikitisha zaidi ni viongozi wanaotoa maagizo wakiwa ama hawana kabisa au wamefunika videvu vyao na wengine wanaishika kwa mikono kwa mbele ili kuirekebisha usoni.

Kwa nini basi waingie gharama ya kuinunua barakoa kama haitumiki ipasavyo?
 
Bado sijaona sababu zinazofanya serikali yangu pendwa ishindwe kugawa BARAKOA kwa raia wake walio katika hatari kubwa ya maambukizi ya COVID19!!!!!!!!!
Kwanini serikali isiangalie maeneo yenye hatari na inafahamika kuwa mkoa wa Dar es salaam ndio wenye visa vingi na hatari kubwa.

Sawa munashindwa kufanya hivyo lakini hata kusimamia bei za hii bidhaa kwa kutoa bei elekezi kwa mtumiaji wa mwisho imekuwa ngumu kwenu?!!!!matokeo yake kila mtu anajipangia bei yake ,Serikali ikiamua inaweza jaribuni kupanga bei ambayo ni affordable kwa raia ili kwa pamoja tushirikiane kupambana na hili tatizo.

Mfano mimi juzi nimeenda katika duka moja la dawa kununua hiyo barakoa nikanunua kwa Tsh 2000 pic 1 leo naenda katika hilo duka nakuta wanauza Tsh4000 pic1 ...hii sio sawa ,na hili limepelekea mafundi cherehani kuzishona kwa wingi huku mtaani jambo ambalo ni hatari maana hazina viwango.Kwenye madaladala unaweza kucheka mpaka basi maana utaona barakoa ambazo hujawahi kuziona toka dunia iumbwe za khanga,vitenge,taulo,nailoni n.k

kama barakoa zinawashinda ,Je mtaiweza LOCKDOWN kweli?

Gaweni Barakoa kwa raia waliopo katika maeneo hatarishi pamoja na elimu ya matumizi yake itasaidia sana kupunguza kasi ya maambukizi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…