Bado sijaona sababu zinazofanya serikali yangu pendwa ishindwe kugawa BARAKOA kwa raia wake walio katika hatari kubwa ya maambukizi ya COVID19!!!!!!!!!
Kwanini serikali isiangalie maeneo yenye hatari na inafahamika kuwa mkoa wa Dar es salaam ndio wenye visa vingi na hatari kubwa.
Sawa munashindwa kufanya hivyo lakini hata kusimamia bei za hii bidhaa kwa kutoa bei elekezi kwa mtumiaji wa mwisho imekuwa ngumu kwenu?!!!!matokeo yake kila mtu anajipangia bei yake ,Serikali ikiamua inaweza jaribuni kupanga bei ambayo ni affordable kwa raia ili kwa pamoja tushirikiane kupambana na hili tatizo.
Mfano mimi juzi nimeenda katika duka moja la dawa kununua hiyo barakoa nikanunua kwa Tsh 2000 pic 1 leo naenda katika hilo duka nakuta wanauza Tsh4000 pic1 ...hii sio sawa ,na hili limepelekea mafundi cherehani kuzishona kwa wingi huku mtaani jambo ambalo ni hatari maana hazina viwango.Kwenye madaladala unaweza kucheka mpaka basi maana utaona barakoa ambazo hujawahi kuziona toka dunia iumbwe za khanga,vitenge,taulo,nailoni n.k
kama barakoa zinawashinda ,Je mtaiweza LOCKDOWN kweli?
Gaweni Barakoa kwa raia waliopo katika maeneo hatarishi pamoja na elimu ya matumizi yake itasaidia sana kupunguza kasi ya maambukizi,