RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

Maelekezo yote yanayolenga kupunguza maambukizi yaungwe mkono.

Makonda kwenye hili anastahili kuungwa mkono lakini anatakiwa kwenda mbele zaidi.

Ushauri wangu ni kuwa mikusanyiko ya ibada idhibitiwe. Kila msikiti au kanisa, siku za ibada, idadi ya washiriki isizidi watu 20 - 30 kwa kutegemea ukubwa wa jengo. Kuwe na umbali usiopungua mita 10 kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Watu wengine wafuatilie ibada kwa kupitia televison majumbani mwao, wakiona inafaa. Na wale wanaoona wanaweza kuandaa utaratibu wao wa ibada majumbani wafanye hivyo.

TBC watoa ratiba za ibada kwa kila dhehebu na dini.
Tibisii hii ninayoijua mimi ya bamaga????? acha masihara wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni muumini, mkristo lakini nimeanza na familia yangu kusalia nyumbani. Mungu yupo pamoja na mimi. Napaswa kutuma zaka na sadaka yangu kanisani. Biblia inaelezea wakati flani wa dharura kujifungia ndani na tusiwe wajinga. "Isaya:26.20
Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita" Ni kitambo tu korona itakwisha. Acha wakaidi wasubiri Serikali iwatangazie wajifungie ndani wao ndio wataumia na watoto wao sio Serikali. Kwani Serikali ni nani? Ni pamoja na wewe!
Maelekezo yote yanayolenga kupunguza maambukizi yaungwe mkono.

Makonda kwenye hili anastahili kuungwa mkono lakini anatakiwa kwenda mbele zaidi.

Ushauri wangu ni kuwa mikusanyiko ya ibada idhibitiwe. Kila msikiti au kanisa, siku za ibada, idadi ya washiriki isizidi watu 20 - 30 kwa kutegemea ukubwa wa jengo. Kuwe na umbali usiopungua mita 10 kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Watu wengine wafuatilie ibada kwa kupitia televison majumbani mwao, wakiona inafaa. Na wale wanaoona wanaweza kuandaa utaratibu wao wa ibada majumbani wafanye hivyo.

TBC watoa ratiba za ibada kwa kila dhehebu na dini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr Ndugulile anazichambua masks za Makonda
 
Attachments

  • PART 3 ...Dr.Fauci Anthony anasema ,_There is currently shortage of N95 and surg ( 480 X 480 ).mp4
    1.3 MB
Makonda sio mtaalam wa afya na mkoa wake ndio unaongoza kwa maambukizi amuamua kuhamasisha watu wa Dar wavae mask iwe kitambaa, chupi, kanga ilimradi uvae mask, yeye hapo kamaliza wajibu wake

Wakija watu wa wizara ya afya wakisema
Vaeni mask N 95 zilizothibitishwa kuzuia corona
Watakuwa wametimiza wajibu wao
Kama alivyo fanya makonda

Angeyasema haya makonda kama vaeni barakoa N95 angekuwa amefanya makosa yeye sio kazi yake kutambua ipi inazuia vumbi na ipi inazuia bacteria na corona..
Kila mtu ahamasishe namna bora ya kupambana na corona sio kubezana hapo ndio watanzania tunapokwama..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani tuzingatie ujumbe uliokusudiwa. Anachomaanisha ni kuwa chochote utakachoenda kununua, ununue na kuondoka. Usinunue kuku choma na kukaa baa. Ukiweza nunua kuku wako, nenda ukale ukiwa nyumbani.

Lakini nadhani ofisi zote za umma na makampuni, wafanyakazi wakae majumbani. Kama haiwezekani kufunga kabisa, wabakizwe wafanyakzi 25%. Wengine wakae majumbani.

Masoko yazuie biashara nyingine zote isipokuwa vyakula.

Maduka yafungwe, tabakie na maduka ya dawa, groceries na supermarkets. Na kwenye maduka hayo uandaliwe utaratibu wa namna ya kufanya manunuzi bila msongamano. Kukifanyika haya, hata msongamano kwenye vyombo vya usafiri utaondoka.

Unaelewa unachokitaka wewe??
Masoko yafungwe ivi unajua machinga wangapi na wafanya biashara ndogondogo watakosa hata hela hata ya kula?? Maduka yafungwe?? Au utamshauri pia kabla hajafungia biashara za watu atoe kwanza unemployment compesations?
Mnataka watu wakae majumbani mtawalisha nyie? Eti maduk yafungwe aisee ivi unajua Tanzania hii wangapi wanaweza kukaa bila hizo biashara au kazi ndani na kwa mda gani bila kufa na njaa??
Acheni kuigaiga vitu nje nusunusu kama mnashauri afunge maduka na bisahara nyingine zote watu wakae ndani tu mwambieni pia either atoe unemployment compensations kwa kila familia au apitishe chakula majumbani tofauti na hapo mkae kwa kutulia kila mtu afanye kazi zake kwa kujilinda vizuri, nyie mlioko huko serikalini kama mmeshiba mishahara mnaweza jifungia tu ndani kwenu na familia zenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kujua "UKAIDI WA WATANZANIA" kesho kuna viongozi wa dini watapanda madhabahuni kufanya ibada kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu.
Shida ni kwamba wasipofanya ibada,kula yao ipo mashakani

Hawana sehemu nyingine za kujipatia kipato,ukweli ndio huo
 
Mtu tu hela ya kununua fungu la nyanya la jero hana ndio atapata hela ya kununua "MAX" na "SANTAIZA"?
 
Maagizo ya kijinga hayo.
Hebu fafanua: ujinga uko wapi? Ulimwenguni kote kumetolewa agizo hilo la kuvaa barakoa. Sasa iweje mkuu wa Mkoa wa Dar akiagiza hivyo liwe agizo la kijinga? Wewe agizo lako lenye busara ni lipi?
 
Hata vitu vinavyohusu afya yako unataka serikali ikugawie, atakayekufa nani wewe au serikali?
Yeye anavaa masks kwa bajeti za hayo mabilioni ya kupambana na corona na ana mishahara na marupurupu chungu tele. Kwa nini na wengine wasifaidike nayo!? Au waliotoa walisema watumie wao wenye madaraka!?
 
Hii ni dalili maambukizi yamezidi, ukiona hatua kali zinazidi kuchukuliwa ujue hali ni mbaya zaidi ya tunavyodhania/kuambiwa.

Japo jana wamesema wataanza kutuambia ukweli, tujihadhari Corona inatuchapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtaani kwako hali ikoje maana maradhi hayafichiki na ukificha kifo kitakuumbua.
 
Maelekezo yote yanayolenga kupunguza maambukizi yaungwe mkono.

Makonda kwenye hili anastahili kuungwa mkono lakini anatakiwa kwenda mbele zaidi.

Ushauri wangu ni kuwa mikusanyiko ya ibada idhibitiwe. Kila msikiti au kanisa, siku za ibada, idadi ya washiriki isizidi watu 20 - 30 kwa kutegemea ukubwa wa jengo. Kuwe na umbali usiopungua mita 10 kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Watu wengine wafuatilie ibada kwa kupitia televison majumbani mwao, wakiona inafaa. Na wale wanaoona wanaweza kuandaa utaratibu wao wa ibada majumbani wafanye hivyo.

TBC watoa ratiba za ibada kwa kila dhehebu na dini.
Hata masuala ya imani yanahitaji elimu tusidharau hilo.
 
Hebu fafanua: ujinga uko wapi? Ulimwenguni kote kumetolewa agizo hilo la kuvaa barakoa. Sasa iweje mkuu wa Mkoa wa Dar akiagiza hivyo liwe agizo la kijinga? Wewe agizo lako lenye busara ni lipi?
Ulimwenguni kote!? Hata huko ulimwenguni kuna lockdown mbona hatuigi!? Wao wanapokea mabilioni ya michango kupambana na corona wanaishia kununua mask zao na kupiga dawa maofisi yao. Kwa nini wasinunue za kuwagawia watu!? Hivi pesa walipewa watumie wao binafsi? Mimi agizo langu lenye busara ni wewe kufunga tu hilo bakuli lako.
 
Back
Top Bottom