RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

Kweli Makonda ni BASHITE(Zero Brain):-

Jana nilikuwa natizama taarifa ya habari akatamka kabisa "SANTAIZA" hivi kweli makonda hajui vitakasa mikono vinaitwaje? Nikasema labda "Slip of the Tongue" kama Phillip Mulugo alivyosema nikasema haya ghafla akasisitiza kwamba makampuni ya simu wachange ring tone ziweke zinazotoa elimu jinsi ya kujikinga na corona.nikasema hivi kweli makonda hajui tofauti ya caller tunes na ring tones? Huyu jamaa kweli ni zero brain anaongea bila kuwa na uelewa.
 
Yeye anavaa masks kwa bajeti za hayo mabilioni ya kupambana na corona na ana mishahara na marupurupu chungu tele. Kwa nini na wengine wasifaidike nayo!? Au waliotoa walisema watumie wao wenye madaraka!?
Iwapo hata ulaya na marekani hawakuweza kutoa barakoa za bure bongo watawezaje?
Nikupe hesabu rahisi: Dar es Salaam ina wakazi takriban milioni tano. Kila barakoa moja kwa sasa ni sh 2,500/=. Kwa hiyo gharama ya barakoa moja kwa kila mkazi wa Dar ni:
5,000,000/= × 2,500/= = 12,500,000,000/=. Hizo ni shilingi bilioni 12.5 kwa siku moja. Halafu kitaalamu huwezi kutumia barakoa moja kwa zaidi ya masaa 4! Kwa hiyo kiwango cha chini ni barakoa 2 kwa siku. Hapo gharama ya siku moja kwa barakoa za kuwatosha wakazi wa Dar pekee ni shilingi bilioni 25! Fikiria kama janga likidumu kwa miezi zaidi ya mitatu ni gharama kiasi gani!
Sasa hapo ni Dar tu, ukiongelea kwa mikoa yote ya Tanzania ni balaa!.
Kwa hiyo unaweza kuona kwa nini hata mataifa makubwa yanalia sana!!
Sasa hapo ni gharama ya barakoa tu hujaongelea gharama za matibabu nk
Ndiyo maana Rais wetu ameitisha maombi ili Mungu atunusuru na balaa hili LA korona!! Halafu mtu akiwa ameshiba maharage yake anakuja hapa na kukujeli wito wa rais wa kufanya maombi!!
 
Pamoja na maelezo yako hafifu...ukitazama hiki ulichoandika unahisi umejibu hiyo comment ya mdau...
Pia kwa taarifa yako hiyo bei ya 25oo ni bei ya kitapeli fuatilia bei yake halisi ndio utaelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kanisani twende na barakoa au
. Tutasalije sasa [emoji23]

Jamani si ibada zisitishwe tu

[emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu wanatamani sana ibada zisitishwe! Hawa bila shaka ni wachawi!! Maombi yakipamba moto wanashindwa kuruka na ungo!! Kipindi hiki si cha ksitisha ibada bali cha kuongeza ibada na Mungu atatuponya na janga hili!
Niwaombe vioongozi wetu wa kitaifa wabaki na msimamo huo wa kuruhusu ibada ili mradi marekebisho yafanyike kuondoa misongamano na watu wanawe kabla na baada ya ibada kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu.
 
Pamoja na maelezo yako hafifu...ukitazama hiki ulichoandika unahisi umejibu hiyo comment ya mdau...
Pia kwa taarifa yako hiyo bei ya 25oo ni bei ya kitapeli fuatilia bei yake halisi ndio utaelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kanuni ya bei sokoni kwa mujibu wa soko huria huzingatia wingi wa uhitaji!!
Tuambie wewe bei ni IPI halafu tupigie hesabu yake ya kutosha wakazi wa Dar kwa mwezi mmoja tu halafu utuambie hiyo pesa unaweza kuipata wapi?
 
Hivi kweli na akili zako unaenda kanisani kufanya nini?

Upstairs uko vizuri kweli?
Yani hadi Makonda akuambie usiende kanisani ndio utaacha kwenda?
Mtu mpagani utamjua tu kwa maneno yake! Ibada haijawahi kuwa na faida kwa mpagani wa moyoni!! Huyo huenda kanisani kama maficho ya upagani wake tu!! Kwake hakuna tofauti kati ya kusali kanisani na kutokusali. Kwake huyo hakuna faida ya kwenda ibadani na hakuna hasara ya kutokuenda ibadani.
Lakini kwa yule aabuduye katika roho na kweli ibada ni kila kitu kwake!!
Wapagani wa moyoni utawajua tu kwa nyakati kama hizi!
 
Barakoa million Hamsini na Tano(55,000,000) au tuseme Million Saba(7,000,000) lockdown is necessary
Nani amekuzuia kuji-lockdown wewe mwenyewe na familia yako?
Huhitaji ruhusa ya mtu kujifungia mwenyewe!! Anza wewe kujilockdown mwenyewe!
 
Aisee! Halafu bado anajimwambafai eti yuko juu kwa kila kitu hata wale waliocheza naye!
Ashukuru kodi zetu huyo bila hivyo huku mitaani labda angeuza wowowo ili aweze kuishi
 
Wagawe maski bure kila nyumba.Hela tu ya kununua muhogo au andazi la sh 200 watu hawana hizo za kununua maski watatoa wapi? Hali wao ndio waliovuruga uchumi kwa ujuaji wao walishindwa kutofautisha kuchunga ng'ombe na kuchunga watu
 
Back
Top Bottom