RC Mtaka anaponzwa na sifa kutoka mitandaoni

RC Mtaka anaponzwa na sifa kutoka mitandaoni

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Kiufupi RC Mtaka ni mtu anayeamini katika kufurahisha watu washangilie kwa muda baadae kombe linafunikwa mwanaharamu anapita bila mabadiliko kutokea au kufanyika. RC ni mtu anayejijenga kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la umaarufu bali si utendaji.

Nashangazwa sana ni kwa namna gani amefanikiwa kutengeneza vijana wengi wa kumshangilia mitandaoni hata kwa maamuzi na kauli za kukurupuka.

Hivi kweli RC ni mtu wa kumjibu vile Waziri ambaye ndio mwenye sera ya kitaifa ya Elimu? Wazir anapozungumzia suala la elimu anazungumza kama mtu mwenye uzoefu wa kutosha kwenye kada hiyo na uwezo mkubwa wa kitaaluma lakini maamuzi na uwezo wake unabezwa na RC na mbunge kama Msukuma? Ifike mahali watu waheshimu taaluma za watu. RC anafikri kwa mtazamo wake wa makambi unaweza kuwa sera mbadala ya elimu?

Uwezo wa Prof.Ndalichako wa kitaalumu na uzoefu ni mkubwa sana kulinganisha na wa RC Mtaka, asitake sifa za kushangiliwa mitandaoni huku ukweli halisi ukijulikana.
 
Katika nia na Ari ya kusaidia wanyonge na maskini yuko sahihi.

Bila Shaka RC Mtaka Ni mtu mwenye kuguswa. Katika wigo mdogo wa ubunifu ameona umuhimu wa jitihada binafsi ya mwanafunzi,mzazi na labda serikali ya mkoa kuweka kambi za kujisomea. Kama aliwawezesha watani zangu wasukuma katika mazingira bila Shaka Wagogo na Warangi wataweza.

Ndalichako hana credibility...toka alipokuwa NECTA ndio maana alipigwa chini. Alibebwa na upepo wa Mwendazake kupenda 'ukinzani' dhidi ya JK. Aliowaona JK hawafai ndio aliowabeba na aliowaona Jakaya wanafaa ndio aliowaangusha.
 
Kwenda zako umeandika upuuzi tu.

Kama yeye ndo mwenye Sera ya elimu mbona Sera yake haiamini anasomesha watoto wake shule za International?

Ivi mkikaa kivulini kula kodi za maskini huwa mnadhani ambao hatupo kwenye politics hatuna akili au??

RC Mtaka ni mtu smart alichoongea ni sahihi tatizo ni kwamba mlizoea kunyenyekewa na kusifiwa.
Huko Marian girls na boys wanapofaulu kwa division 1 darasa zima unadhani wanafuatisha hiyo Sera yenu ya kijinga kwa 100% ?

Mungu fundi najua umenielewa
 
Huyo mtu mwenyewe unaye mtetea ana uwezo wa kwenye makaratasi tu. Nje ya hapo ni bendera fuata upepo! Hivyo alistahili kabisa kuambiwa ukweli. Muda wa kuwalea wanafiki nadhani umeshapita kitambo.

Na ushahidi wa unafiki wake, na ubendera fuata upepo ni kwenye sakata zima la kuandaa somo la historia! Alikuwa anapelekwa pelekwa tu! Mpaka bosi wake alipokufa, ndiyo akili yake ikamrudia.
 
Prof. si mtu wa kumlinganisha na RC kwenye kada ya elimu, msimponze huyo kijana mtampoteza. RC Mtaka anaponzwa na mitandao
Hahaaa hawa ma profesa wetu ni wa kuonea huruma tu maana hamna kitu mkuuu yaan wamekalilishwa ujinga tu ndo maana hawana msaada kwenye taifa ndo maana na ujinga wangu nakomaana watoto wangu private school ili hata wajifunze kujiamini na utandawazi mapema nije niwatupe hata nje kwa ndugu na jamaa wakaendelee huko ila sio bongo
 
Prof. si mtu wa kumlinganisha na RC kwenye kada ya elimu, msimponze huyo kijana mtampoteza. RC Mtaka anaponzwa na mitandao
Ataponzwa na lipi? Wewe usidhani watu wote wamewekeza mioyo na akili zao kwenye vyeo kama wahuni wengine unaowafahamu? Ambao wako tayari kukaa kimya ama kutofanya maamuzi ili kulinda vyeo.

Mtaka hanaga unafiki. Yupo kwa kwa ajili ya wananchi.a
 
Back
Top Bottom