RC Mtaka anaponzwa na sifa kutoka mitandaoni

RC Mtaka anaponzwa na sifa kutoka mitandaoni

Kiufupi RC Mtaka ni mtu anayeamini katika kufurahisha watu washangilie kwa muda baadae kombe linafunikwa mwanaharamu anapita bila mabadiliko kutokea au kufanyika. RC ni mtu anayejijenga kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la umaarufu bali si utendaji.

Nashangazwa sana ni kwa namna gani amefanikiwa kutengeneza vijana wengi wa kumshangilia mitandaoni hata kwa maamuzi na kauli za kukurupuka.

Hivi kweli RC ni mtu wa kumjibu vile Waziri ambaye ndio mwenye sera ya kitaifa ya Elimu? Wazir anapozungumzia suala la elimu anazungumza kama mtu mwenye uzoefu wa kutosha kwenye kada hiyo na uwezo mkubwa wa kitaaluma lakini maamuzi na uwezo wake unabezwa na RC na mbunge kama Msukuma? Ifike mahali watu waheshimu taaluma za watu. RC anafikri kwa mtazamo wake wa makambi unaweza kuwa sera mbadala ya elimu?

Uwezo wa Prof.Ndalichako wa kitaalumu na uzoefu ni mkubwa sana kulinganisha na wa RC Mtaka, asitake sifa za kushangiliwa mitandaoni huku ukweli halisi ukijulikana.
Ndalichako bhana, nikikumbuka kile kingereza chake enzi za Jiwe nabaki mdomo wazi
 
Mtaka ni mshamba mshamba mmoja aliyejaza theory kichwani na kuishi maisha ya kusadikika, Theory watu wengi huku mitaani tunazijua sana kuziongeaongea.

Tujitahidi sana kuwa na watu wenye exposure kwenye mifumo, ambao wanajua mambo practically yanavyofanya kazi.

Uongozi unawafaa sana watoto wa mjini watu wa magumashigumashi kama MALIMA JNR, MAKAMBA JNR, RIZ JK, MSECHU NHC, FREEMAN MBOWE, LEMA, SUGU, PROP JAY na baba yao JK.

Kuwapa uongozi watu washambawashamba waliojaza theory za shule kichwani ni hatari sana.
 
Siku akimpinga rais wake ndio watajua kwamba mtaka ni takataka.
Hii comment nayo ni takataka!.Rais hayuko juu ya Sheria kama kuna mahali amekosea kumpinga sio kosa mkuu.Suala linakuja njia na utaratibu utakaoweza kuutumia kumpinga Rais
 
Hii comment nayo ni takataka!.Rais hayuko juu ya Sheria kama kuna mahali amekosea kumpinga sio kosa mkuu.Suala linakuja njia na utaratibu utakaoweza kuutumia kumpinga Rais
Nilikuwa naongelea mtaka mkuu wa mkoa.

Ungekuwa na ufahamu kiduchu ungejua kuwa mkuu wa mkoa hawezi kumpinga rais aliyempa huo ukuu wa mkoa na akabaki kuwa mkuu wa mkoa.

You either have to resign, or shut up. That simple.
 
Back
Top Bottom