Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Alichoandika Mdau ~ Barabara ya Mwanza Mjini kwenda Kangaye ni mbovu sana, ina tu cost Watumiaji wengi
Mkuu wa Mkoa, Said Mtanda amesema “Naishukuru platform hii (JamiiForums) kwa kuwapa Wananchi wa Mwanza fursa kueleza changamoto zao na sisi viongozi wa Mwanza tunapata kujua na kufuatilia.
“Barabara hii ya MECCO-KANGAYE imeharibiwa sana na mvua, Mkoa wa Mwanza hupata wastani wa mvua mm 140 lakini kwa Mwaka 2026 tumefikia mm 170, hivyo tuna uharibifu mkubwa wa miundombinu mbalimbali kutokana na mafuriko.
“Serikali ya mkoa imeomba fedha ya dharura Milioni 408 kwa ajili ya ukarabati wa barabara hii kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa TARURA ili kuikarabati na kuweka mifereji katika barabara hii, tutaendelea kutoa taarifa hatua kwa hatua mpaka ikikamilika.
“Tunawaomba radhi Wananchi na watumiaji wa barabara kwa usumbufu wanaopitia. Asanteni pia mtoa hoja.”
Wakati huohuo upande wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), kupitia kwa Catherine Sungura ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma ametoa tamko kwa kueleza:
“TARURA tunawashukuru Wananchi kwa uvumilivu wao na tunaendelea kufuatilia ili kuhakikisha huduma inaboreshwa zaidi. Tayari tumeshachukua hatua ya muda mfupi ili eneo liweze kupitika huku tukisubiri matengenezo makubwa yaliyopangwa kufanyika kwenye bajeti ijayo.
“TARURA tunawashukuru Wananchi kwa uvumilivu wenu na tunaendelea kufuatilia ili kuhakikisha huduma inaboreshwa zaidi. Kwa mawasiliano zaidi piga bure 0800110807.