Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kwa kushirikiana na wakuu wa wilaya zote zilizopo ndani ya mkoa wa Katavi wameeleza mafanikio yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongoziwake ambayo yameleta matokeo chanya katika jamii
Wakizungumzia miradi mbalimbali iliyotekelezwa ndani ya mkoa wamesema Serikali ya Rais Dkt Samia Suluh Hassan imetoa fedha zaidi ya Trilion moja ambazo zimekamilisha baadhi ya miradi katika sekta mbalimbali huku mingine ikiendelea na ujenzi
Akizungumza kwa niaba ya MKuu wa wilaya ya Mpanda mstaiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya Samia wanaendelea kuboresha miondombinu ya afya huku Chifu wa kabila la Wakonongo akidai Rais Samia ameweza kusimamia amani ya nchi toka amekabidhiwa madaraka ya uongozi.
Kongamano la kuelezea mafanikio ya miaka mitatu ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta samia Suluh Hassan limehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali pamoja na wananchi wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi.