HOJA RC Mwanza, Said Mtanda, Kwa Huu Ukosefu wa Maji Wiki Zaidi ya 2 Hustahili Kuendelea Kuwa Kazini. Wajibika

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Chakaza

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
41,034
Reaction score
74,732
Kwa hali inayo endelea katika jiji la Mwanza ambalo limezungukwa na maji ya Ziwa Victoria kukosekana maji na eti RC yupo anazunguka zunguka mjini mjini akipeperusha benders kwenye Gari yake ni aibu ya karne.

RC Said Mtanda anafahamika kuwa ni mtendaji mzuri, lakini nadhani atakuwa Sasa amechoka na anapaswa kupumzika au pengine sifa anazozipata ni mapambio yanayo tengenezwa na waandishi wa habari kwa sababu zao binafsi.

Mbona hili tatizo la maji linachukuliwa kwa udogo sana kuliko hali halisi?

Majumbani maji hakuna, mashuleni hakuna hata mahospitalini? Na bwana Said Mtanda kakaa tu ofisini? Hakuna ufuatiliaji kwa uzito au kuwajibishwa watu?

Soma Pia: Ukosefu wa Maji kwa Wiki 3 – Maeneo ya Chuo cha SAUT - Mwanza

Ila wakatimwingine ni kuifikiria serikali nzima katika suala la uwajibikaji na kutikisa kichwa tuu!
Poleni sana huko Mwanza, maana twaweza kuja huko na kuondoka bila kuoga! Labda watapaweza kina Pascal Mayalla maana nyumbani ni nyumbani
 
Kufanya maamuzi magumu hakuhitaji vikao aisèe
20260612_141140.jpg
 
Muache huyo kwanza. Tatizo liko kwa wakazi wake, ni mabingwa wa kunung'unika lakini kama walivyo nyuki wa mashineni.

Inawezekana vipi maji hayapatikani kwa watu walio kando ya ziwa, kisha wakazi wake wanaendelea na maisha kama hakuna kinachotokea huku akina mama na watoto, wakichangia maji ya visima vya mababu na nguchiro?

Inawezekanaje mamlaka ya maji Mwanza, iwe na jengo zuri la vioo, wao wakiliita MAJI HOUSE, watumishi kedekede na magari lukuki, lakini wababchi hawapati maji?

Inawezekana vipi mamlaka ifanye jukumu la kuuza maji kwenye malori" bowser" lakini wanashindwa kusukuma maji ya bomba na wakazi wanashuhudia bila kuchukua hatua?

Inawezekana vipi Chakaza, kutoka nje ya Mwanza uanzishe uzi huu kuhusu tatizo la maji Mwanza, lakini watumiaji wa JF mwanza wapo na hawachukui hatua?

Inawezekana vipi, kuwe na tatizo hilo kwa zaidi ya mwezi na hakuna taarifa zinazotolewa au kama wametoa kwenye vyombo ambavyo siku hizi havina wasikilizaji, lakini wanaweza kukutumia bili kila mwezi ila hawawezi kutumia njia hiyo hiyo kutotaarifa juu ya ukosefu wa maji.

Kwani ninyi wakazi wa Mwanza ni nani aliyewaloga?
 
Huyo RC sina uhakika kama anafahamu mqmbo yanayotokea nje tu ya ofisi yake.

Nitakupa mfano, kuna kipande cha barabara cha mita 500 kutoka Buhongwa kwenda Bulale, ujenzi wake ulipaswa kukamilika April 2025, mpaka sasa haieleweki tatizo nini nini katika varabara huyo muhinu yenye kituo kikubwa cha Afya ambko magari ya wagonjwa yabapata shida kupita hapo.

Sina uhakika kama anafikiri baada ya kutoka Mwanza ataacha kumbukumbu gani nzuri kama ya akina Daniel ole Njoolay.

Vinginevyo, akiri kuwa tatizo la maji katika mkoa anaoongoza na uliozungukwa na ziwa viktoria, ni mlima mrefu kwake.
 
Kwa hali inayo endelea katika jiji la Mwanza ambalo limezungukwa na maji ya Ziwa Victoria kukosekana maji na eti RC yupo anazunguka zunguka mjini mjini akipeperusha benders kwenye Gari yake ni aibu ya karne.

RC Said Mtanda anafahamika kuwa ni mtendaji mzuri, lakini nadhani atakuwa Sasa amechoka na anapaswa kupumzika au pengine sifa anazozipata ni mapambio yanayo tengenezwa na waandishi wa habari kwa sababu zao binafsi.

Mbona hili tatizo la maji linachukuliwa kwa udogo sana kuliko hali halisi?

Majumbani maji hakuna, mashuleni hakuna hata mahospitalini? Na bwana Said Mtanda kakaa tu ofisini? Hakuna ufuatiliaji kwa uzito au kuwajibishwa watu?

Soma Pia: Ukosefu wa Maji kwa Wiki 3 – Maeneo ya Chuo cha SAUT - Mwanza

Ila wakatimwingine ni kuifikiria serikali nzima katika suala la uwajibikaji na kutikisa kichwa tuu!
Poleni sana huko Mwanza, maana twaweza kuja huko na kuondoka bila kuoga! Labda watapaweza kina Pascal Mayalla maana nyumbani ni nyumbani
Mtanda hawezi kuwajibika kwa matatizo ya wananchi, yeye amewajibika kwa Samia kwa kumsaidia kuua waandamanaji ili abaki madarakani kwa shuruti.
 
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Bora ninyi hamjapata maji kwa muda wa wiki mbili kuna sehemu Dar es salaam panaitwa msakuzi wilaya ya ubungo hawajawahi kuona maji ya dawasa toka wapate uhuru mwaka 1961 ni kilomita tano tu kutokea mbezi stend.Hatari sana hii awamu ya wazanzbar.
 
Bora ninyi hamjapata maji kwa muda wa wiki mbili kuna sehemu Dar es salaam panaitwa msakuzi wilaya ya ubungo hawajawahi kuona maji ya dawasa toka wapate uhuru mwaka 1962.ni kilomita tano tu kutokea mbezi stend.Hatari sana hii awamu ya wazanzbar.
Maeneo mengi ya hili linaloitwa jiji hayana maji kwa zaidi ya wiki hizo mbili, yapo ambko maji hayajatoka hadi miezi minne.

Nimedokezwa eti shida ni umeme kucheza cheza hivyo kuunguza pampu za kusukuma maji!

Najiuliza katika zama hizi kweli hilo linaweza kuwa tatizo? Na vipi yale maeneo ambako maji hayakosi wao wanatumia umeme kutoka wapi?
 
Kuna chawa linaitwa ChoiceVariable , alisema eti vijiji 85% na zaidi nchi nzima vimefikiwa na maji, nilihoji juu ya ukweli wa taarifa zake sikupewa majibu .

Sasa kama Mwanza iliyozungukwa na vyanzi vya maji kama mito na ziwa haina maji huko vijijini hali ipoje?
 
Tatizo la Mwanza na Tanzania ni hili; kipaumbele chetu ni kipi? Vipi DC wa Nyamagana aliyeko mjini, ongeza na DED pamoja na watendaji wengine wa taasisi na idara za serikali, watumie( kila mmoja) gari lenye thamani ya tsh milioni 400, ilhali hakuna pampu za kusukuma maji?
 
Kwa hali inayo endelea katika jiji la Mwanza ambalo limezungukwa na maji ya Ziwa Victoria kukosekana maji na eti RC yupo anazunguka zunguka mjini mjini akipeperusha benders kwenye Gari yake ni aibu ya karne.

RC Said Mtanda anafahamika kuwa ni mtendaji mzuri, lakini nadhani atakuwa Sasa amechoka na anapaswa kupumzika au pengine sifa anazozipata ni mapambio yanayo tengenezwa na waandishi wa habari kwa sababu zao binafsi.

Mbona hili tatizo la maji linachukuliwa kwa udogo sana kuliko hali halisi?

Majumbani maji hakuna, mashuleni hakuna hata mahospitalini? Na bwana Said Mtanda kakaa tu ofisini? Hakuna ufuatiliaji kwa uzito au kuwajibishwa watu?

Soma Pia: Ukosefu wa Maji kwa Wiki 3 – Maeneo ya Chuo cha SAUT - Mwanza

Ila wakatimwingine ni kuifikiria serikali nzima katika suala la uwajibikaji na kutikisa kichwa tuu!
Poleni sana huko Mwanza, maana twaweza kuja huko na kuondoka bila kuoga! Labda watapaweza kina Pascal Mayalla maana nyumbani ni nyumbani
Ku step down sio utaratibu wa wana ccm
 
Back
Top Bottom