Mkuu 'Mashilatu', unajuwa tatizo linapoanzia?
Hili siyo swala la Mwanza pekee, ni maeneo yote nchini.
Tatizo linaanzia kwa viongozi wa ngazi za chini kabisa katika maeneo hayo. Hawatimizi wajibu wao.
Hata huko kwenye Halmashauri ni uozo mtupu
Ukiyaweka pamoja utakuta kuwa ni uozo uliomo ndani ya Chama na serikali katika ngazi zote
Wabunge wapo kulinda maslahi binafsi; wakitegemea chama kiendelee kuwapa fursa. Bunge zima lile, ni wateule wa chama hakuna waliopigiwa kura na wananchi; kwa hiyo hawajishughulishi na maswala ya wananchi. Wajibu wao wa kwanza ni kukilinda chama na serikali yake.
Viongozi wote toka chini hadi juu, kazi yao kubwa ni kulinda maslahi ya chama na kwa namna hiyo ya kwao binafsi.
Ndiyo maana akina Luhaga Mpina hawamo Bungeni; lakini akina Bulaya, Waitara na wengine wote wamo Bungeni; na katika Halmashauri, hali ni hiyo hiyo, na wakurugenzi wote.
Maswala ya wananchi yataanzia wapi katika hali ya namna hii?