Chakaza
Platinum Member
- Mar 10, 2007
- 41,034
- 74,732
- Thread starter
- #21
Asante sana kwa kuligusia hili! Yaani Mwanza kumbe ndio maana inadhaMuache huyo kwanza. Tatizo liko kwa wakazi wake, ni mabingwa wa kunung'unika lakini kama walivyo nyuki wa mashineni.
Inawezekana vipi maji hayapatikani kwa watu walio kando ya ziwa, kisha wakazi wake wanaendelea na maisha kama hakuna kinachotokea huku akina mama na watoto, wakichangia maji ya visima vya mababu na nguchiro?
Inawezekanaje mamlaka ya maji Mwanza, iwe na jengo zuri la vioo, wao wakiliita MAJI HOUSE, watumishi kedekede na magari lukuki, lakini wababchi hawapati maji?
Inawezekana vipi mamlaka ifanye jukumu la kuuza maji kwenye malori" bowser" lakini wanashindwa kusukuma maji ya bomba na wakazi wanashuhudia bila kuchukua hatua?
Inawezekana vipi Chakaza, kutoka nje ya Mwanza uanzishe uzi huu kuhusu tatizo la maji Mwanza, lakini watumiaji wa JF mwanza wapo na hawachukui hatua?
Inawezekana vipi, kuwe na tatizo hilo kwa zaidi ya mwezi na hakuna taarifa zinazotolewa au kama wametoa kwenye vyombo ambavyo siku hizi havina wasikilizaji, lakini wanaweza kukutumia bili kila mwezi ila hawawezi kutumia njia hiyo hiyo kutotaarifa juu ya ukosefu wa maji.
Kwani ninyi wakazi wa Mwanza ni nani aliyewaloga?
0