Mtanda hawezi kuwajibika kwa matatizo ya wananchi, yeye amewajibika kwa Samia kwa kumsaidia kuua waandamanaji ili abaki madarakani kwa shuruti.Kwa hali inayo endelea katika jiji la Mwanza ambalo limezungukwa na maji ya Ziwa Victoria kukosekana maji na eti RC yupo anazunguka zunguka mjini mjini akipeperusha benders kwenye Gari yake ni aibu ya karne.
RC Said Mtanda anafahamika kuwa ni mtendaji mzuri, lakini nadhani atakuwa Sasa amechoka na anapaswa kupumzika au pengine sifa anazozipata ni mapambio yanayo tengenezwa na waandishi wa habari kwa sababu zao binafsi.
Mbona hili tatizo la maji linachukuliwa kwa udogo sana kuliko hali halisi?
Majumbani maji hakuna, mashuleni hakuna hata mahospitalini? Na bwana Said Mtanda kakaa tu ofisini? Hakuna ufuatiliaji kwa uzito au kuwajibishwa watu?
Soma Pia: Ukosefu wa Maji kwa Wiki 3 – Maeneo ya Chuo cha SAUT - Mwanza
Ila wakatimwingine ni kuifikiria serikali nzima katika suala la uwajibikaji na kutikisa kichwa tuu!
Poleni sana huko Mwanza, maana twaweza kuja huko na kuondoka bila kuoga! Labda watapaweza kina Pascal Mayalla maana nyumbani ni nyumbani
😀😀😀Yawezekana wanaogopa wakipunguza maji ya ziwani ili wananchi waneemeke samaki na vyura watakufa.
Maeneo mengi ya hili linaloitwa jiji hayana maji kwa zaidi ya wiki hizo mbili, yapo ambko maji hayajatoka hadi miezi minne.Bora ninyi hamjapata maji kwa muda wa wiki mbili kuna sehemu Dar es salaam panaitwa msakuzi wilaya ya ubungo hawajawahi kuona maji ya dawasa toka wapate uhuru mwaka 1962.ni kilomita tano tu kutokea mbezi stend.Hatari sana hii awamu ya wazanzbar.
Tatizo la Mwanza na Tanzania ni hili; kipaumbele chetu ni kipi? Vipi DC wa Nyamagana aliyeko mjini, ongeza na DED pamoja na watendaji wengine wa taasisi na idara za serikali, watumie( kila mmoja) gari lenye thamani ya tsh milioni 400, ilhali hakuna pampu za kusukuma maji?Kuna chawa linaitwa ChoiceVariable , alisema eti vijiji 85% na zaidi nchi nzima vimefikiwa na maji, nilihoji juu ya ukweli wa taarifa zake sikupewa majibu .
Sasa kama Mwanza iliyozungukwa na vyanzi vya maji kama mito na ziwa haina maji huko vijijini hali ipoje?
Ku step down sio utaratibu wa wana ccmKwa hali inayo endelea katika jiji la Mwanza ambalo limezungukwa na maji ya Ziwa Victoria kukosekana maji na eti RC yupo anazunguka zunguka mjini mjini akipeperusha benders kwenye Gari yake ni aibu ya karne.