Asante sana kwa kuligusia hili! Yaani Mwanza kumbe ndio maana inadhaMuache huyo kwanza. Tatizo liko kwa wakazi wake, ni mabingwa wa kunung'unika lakini kama walivyo nyuki wa mashineni.
Inawezekana vipi maji hayapatikani kwa watu walio kando ya ziwa, kisha wakazi wake wanaendelea na maisha kama hakuna kinachotokea huku akina mama na watoto, wakichangia maji ya visima vya mababu na nguchiro?
Inawezekanaje mamlaka ya maji Mwanza, iwe na jengo zuri la vioo, wao wakiliita MAJI HOUSE, watumishi kedekede na magari lukuki, lakini wababchi hawapati maji?
Inawezekana vipi mamlaka ifanye jukumu la kuuza maji kwenye malori" bowser" lakini wanashindwa kusukuma maji ya bomba na wakazi wanashuhudia bila kuchukua hatua?
Inawezekana vipi Chakaza, kutoka nje ya Mwanza uanzishe uzi huu kuhusu tatizo la maji Mwanza, lakini watumiaji wa JF mwanza wapo na hawachukui hatua?
Inawezekana vipi, kuwe na tatizo hilo kwa zaidi ya mwezi na hakuna taarifa zinazotolewa au kama wametoa kwenye vyombo ambavyo siku hizi havina wasikilizaji, lakini wanaweza kukutumia bili kila mwezi ila hawawezi kutumia njia hiyo hiyo kutotaarifa juu ya ukosefu wa maji.
Kwani ninyi wakazi wa Mwanza ni nani aliyewaloga?
Broo hii picha usiendelee kuipost please,Kufanya maamuzi magumu hakuhitaji vikao aisèe View attachment 3606732
Watu wa Aina yako wana mchango mdogo sana katika ustawi wa binadamu.RC ni Fundi Bomba?
Sawa mkuu sanaBroo hii picha usiendelee kuipost please,
Nakuunga mkono, Mwanza Kuna maisha ya kinafiki sana. Wao ni kukimbizana kusifia viongozi. Sio watendaji, watumishi na hasa WAANDISHI WA HABARI labda tumtoe ALOYCE NYANDA pekee ndio mwandishi pekee anayeweka UOZO hadharani bila woga.Shida ya maji mwanza haijaanza leo labda serikali yote ya mwanza ifutwe.
Sahihi kabisa, mwanza sio barabara, maji, ukusanyaji taka, mipango miji kwa ujumla kila kitu kinajiendea hovyo hovyo tu miaka na miaka.Nakuunga mkono, Mwanza Kuna maisha ya kinafiki sana. Wao ni kukimbizana kusifia viongozi. Sio watendaji, watumishi na hasa WAANDISHI WA HABARI labda tumtoe ALOYCE NYANDA pekee ndio mwandishi pekee anayeweka UOZO hadharani bila woga.
Hata watendaji wengine nilichokigundua wanatenda kwa sifa tuu pale wamuonapo RC anakuja maeneo yao na meishoni ni hayo ya wakishindwa wanasingizia taasisi nyingine kama Tanesco.
Huyu RC Mtanda naye full time kuwazia Uyanga wake tu, lakini kazi aaah! (Joke)
Suala la unafiki umepiga penyewe, hakuna cha mwandishi aliyebaki salama, tena utashangaa kuna chuo kikuu kinachozalisha waandishi wa ngaxi mbalimbali, lakini, hakuna aliye salama.Nakuunga mkono, Mwanza Kuna maisha ya kinafiki sana. Wao ni kukimbizana kusifia viongozi. Sio watendaji, watumishi na hasa WAANDISHI WA HABARI labda tumtoe ALOYCE NYANDA pekee ndio mwandishi pekee anayeweka UOZO hadharani bila woga.
Hata watendaji wengine nilichokigundua wanatenda kwa sifa tuu pale wamuonapo RC anakuja maeneo yao na meishoni ni hayo ya wakishindwa wanasingizia taasisi nyingine kama Tanesco.
Huyu RC Mtanda naye full time kuwazia Uyanga wake tu, lakini kazi aaah! (Joke)
Hapo ishu unakuta mzabuni ana supply vifaa ana malimbikizo ya hela nyingi anazowadai unakuta amegoma kusupplyTatizo la Mwanza na Tanzania ni hili; kipaumbele chetu ni kipi? Vipi DC wa Nyamagana aliyeko mjini, ongeza na DED pamoja na watendaji wengine wa taasisi na idara za serikali, watumie( kila mmoja) gari lenye thamani ya tsh milioni 400, ilhali hakuna pampu za kusukuma maji?
Halafu watu bado wako ofisini!Ila mwanza...🚮🚮🚮 mwakajana mwishoni dumu lilifika 1500 mamaee
"Katikati ya maji mengi, mpumbavu ana kiu"Ziwa jirani na kuna shida ya maji
Vituko haviwezi Isha
Ova