RC wa Dar es Salaam kutoa usafiri kwa Ombaomba wanaotaka kurudi makwao mwezi wa 6

RC wa Dar es Salaam kutoa usafiri kwa Ombaomba wanaotaka kurudi makwao mwezi wa 6

Mapendekezo haya hayajagusa tatizo la msingi . Kifupi ombi hilo limefeli hata kabla ya kuanza kutekelezwa.
 
Mtu anayeomba ili apate pesa ya kula akirudi kijijini atakua na mipango gani? Kuomba?

Depression and death
Km Ni mzima akalime na km Ni mlemavu basi huenda wanawezs kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujikimu
 
M juzi kuna vijana wa hapa mjini nilikuwa nawaambia we sa hivi una miaka 30 huna hata sehemu ya kulala wala huna jitihada zozote za kutafta maisha yeye akiamka anaunga unga akipata buku ya chakula hiyo imeisha sasa mtu wa hivo unafikiri akizeeka ndo atarudi kijijini kwao?

Jibu ni hapana badala yake ataanza kuomba,utasikia mjukuu wangu nisaidie wakati hata kuoa hajawahi kuoa,jamani ombaomba wengi ni wa hapo mjini ni wenyeji wa mji kumrudisha kwao ni vigumu mno
 
Hivi mimi huwa najiuliza kwani mtu ukiwa mpole huna sifa ya uongozi? Kuna kahusiano gani kati ya ukali na utawala..? Sio tu kwa rc! Namaanisha hata ngazi nyingine za uongozi na hta maisha ya uraini.
Mbona jk sio mkali na alikuwa poa tu
 
Kwa sasa warudi kwao idodomya, nyumbani kumenoga...
 
Marehemu alikataza kuombaomba alisemaga asiyefanya kazi asile

Ila aliheshimu wapambanaji halali
Kwahiyo hao omba omba mnaotaka kuwatoa sasahivi walikuwa ni wapambanaji halali wakati wa utawala wa marehemu?
 

Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam imesema ipo tayari kutoa usafiri kwa ombaomba wanaotaka kurudi kwao kwa hiari ifikapo mwezi wa sita mwaka huu. Huku akiwataka Wakuu wa wilaya kuratibu zoezi hilo ikiwamo pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria mawakala wanao waleta kutoka mikoani.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala amewataka ombaomba wote walipo Dar Es Salaam kujiandikisha kwa hiari majina yao pamoja vijiji wanavyo toka ili ofisi yake iweze kuwarudisha nyumbani na kuwaepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia ifikapo mwezi wa sita mwaka huu ofisi yake iweze kuwapa usafiri wa kuwafikisha makwao suala ambalo ameleza limewapa usumbufu wakuu wa mikoa waliopita akiwemo Mzee Yusufu Makamba.

Aidha Mhe. Makala ameongezea kuwa suala la ombaomba limekuwa mradi kwa mawakala ambao uwasaidia ombaomba hao kuwasafirisha kutoka makwao na kuwapagishia vyumba pamoja na kuwapa chakula na kuwataka walelete pesa wanazoomba kila siku.

Katika hatua nyingene Mkuu wamkoa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye madhimisho ya siku ya kujenga uwelewa juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa mgeni rasmi.


ITV

Wa kuanza nao ni hao mawakala kwa kuwafungulia kesi ,kisha ndio hao omba omba wanrudishwa kwao huku kijijini wakalime.
 
Hivi mimi huwa najiuliza kwani mtu ukiwa mpole huna sifa ya uongozi? Kuna kahusiano gani kati ya ukali na utawala..? Sio tu kwa rc! Namaanisha hata ngazi nyingine za uongozi na hta maisha ya uraini.
Kwa jamii yote ya kiafrica hasa Tanzania ukiwa mpole sana mambo hayaendi.

Upole unafiti zaidi kwenye jamii ya watu waliostaarabika hasa uko ulaya.

Kwangu mimi pamoja na Kunenge kuwa ni kiongozi Mzuri ila kwa upole wake jiji la Dar asingelimudu.
 
Back
Top Bottom