RC wa Kagera Chalamila hizo Milioni 10 za Rais Samia kwa Wavuvi Waokoaji ni za kuwapa Wagawane au Wafunguliwe Akaunti Benki?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Rais Samia alipotoa hizo Pesa Tsh Milioni 10 alisema wazi kabisa kuwa ni Asante kwa Wavuvi kwa Uokoaji wa Manusura wa Ajali ya Ndege Mkoani Kagera ya Precision Air na hakusema kuwa Wafunguliwe Akaunti Benki kama ulivyofanya Wewe.

Kwanini unakuwa na Kiherehere sana Wewe? Na kama kweli nia yako ni Kuwafungulia Akaunti Benki mbona kwa Muokoaji wenu wa Samjo Samjo ( Muongo Muongo ) Majaliwa Jackson hukusema kuwa zile alizopewa na Yeye akupe Ukamfungulie Akaunti Benki?

RC wa Kagera Chalamila ni lini hao Wavuvi Waokoaji walikuambia hawana Akaunti Benki au wanataka Kufunguliwa? Kwani Akaunti zao za Simu ungewapa hizo Pesa Wagawane wasingeziweka huko kisha waendelee na Maisha yao?

Na jana tena umerudia Upuuzi wako ule ule aliyekuwa Mfadhili wa Simba SC yangu Azim Dewji nae ametoa Shilingi Milioni Kumi ( Tsh 10,000,000/= ) na kutaka upeleke kwa hawa hawa Wavuvi ili Wakagawane kama kawaida yako na Kiherehere chako ukakataa Wasigawane na Kulazimisha Wafunguliwe Akaunti Benki na zikae huko.

Una bahati sana umekutana na Wavuvi Waokoaji Wapole kutoka kwa Watani zangu wakubwa Wahaya Mkoani Kagera ila ungekuwa ni RC wa Mkoani Kwangu Mara ( Musoma ) halafu ungekuja na hiki Kiherehere chako ndiyo ungejua ni kwanini Nyoka hana Ugoko na kwanini Wimbo wa Taifa hauna Kolabo.
 
We jamaa tayari mdudu keshaingia kwenye embe.!
 
Anataka wafungue account ili wakati wa kuzitoa serikali YA ccm ikate tozo.

Serikali isiyojali wananchi wake wanaona furaha wanavyotaabika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…