Sasa kombe la dunia ni shindano kubwa kwa sababu za kisiasa ila halina mechi ngumu, na wala sio kipimo sahihi cha ubora wa mchezaji, mfano Argentina alicheza mechi za maana zilikuwa 2 tu, dhidi ya France Fainali na kidogo dhidi ya Croatia
Nyingine ni dhidi ya timu nyepesi kama Poland, Saudi Arabia, Australia n.k
Tofauti na Champions league ambako kuna timu ngumu zenye mkusanyiko wa wachezaji bora duniani kama Madrid, Bayern Munich, Inter Milan ambazo City kazifunga ,
Kuthibitisha hilo tazama Messi na Mbape, wachezaji waliofanya vizuri zaidi kombe la Dunia lakini hawakuweza kuifunga timu kama Inter Milan na Bayern Munich na kupelekea kutolewa mapema UEFa
kwenye ligi ngumu yenye ushindani kama Uingereza kulikuwa na timu ngumu kama Arsenal, Man Utd, Newcastle ambazo City kuzifunga na kuchukua kombe kwa msaada wa Haaland na alivunja rekodi ya ufungaji