Records za Messi & Halaand 2022/23

kuwa MOTM KDB sio hoja kuwa nayeye haku perform. au kwenye mechi mchezaji aneperform vizuri huwa ni mmoja tu?
Kila mchezaji kwenye mechi ana perform sikatai ila mwenye MOTM ndio anakua ameinfluence game/ushindi wa team kwa kiasi kikubwa.
 
Top 5 league zote zina point sawa, watu hawamuongelei Lacazette sababu ni babu tayari, angekua ni Kinda wa miaka 20 timu zote kubwa zingekua zinamgombania.

Huko Serie A kina Immobile hawafungi 30? Ila kimya sababu tayari Age zimeenda, Osimhen ni mtoto na anatafuta next big move lazima aongelewe sana.

Mbape si amecheza Ligi ya Ufaransa miaka yake yote? Je yeye Hagombaniwi?
 
Kumbe issue ni kuwa na taji OK sawa!.

Messi na WC na League one msimu huu na ni Best player WC

Haaland ana CL ,EPL na FA na ni Best player EPL

Kwa hiyo tumpe Best player wa EPL tuzo ya Mchezaji bora wa Dunia si ndio??

kwahiyo yote hujaona zaidi ya hiyo best player wa EPL?

Chamion Leage Top Score
EPL Top Score
European Golden Shoe Top Score
European Club Season Top Score
EPL Best Player
Champion League winner
Fa CUP Winner
EPL Winner
50+ goals a Season (hakuna mwengine yoyote aliyeifika hii namba)
 

naona unaleta isue za kugombewa, mim nimezungumza kuongelewa.

Kwahiyo leo hii goals za french league zimekuwa nazo ni dili?

Mwakani naamini pia mtakuje kusema MLS nayo ni dili 😂😂😂
 
naona unaleta isue za kugombewa, mim nimezungumza kuongelewa.

Kwahiyo leo hii goals za french league zimekuwa nazo ni dili?

Mwakani naamini pia mtakuje kusema MLS nayo ni dili 😂😂😂
Mls haina coefficient nzuri, ila league 1 inayo. Uefa wana Coeficient za ligi kila mwaka timu za ligi husika zinavyo progress unapewa points ndio likatokea hilo neno Top 5 league.

Ukifunga Goli kwenye Top 5 league = 2 points, haijalishi ni Man city ama Psg, as long as ni Top 5 goli moja lina maksi sawa.
 
World Cup ni mechi 6 tu mzee, wakati mechi za ligi, uefa, fa ni karibia 60

Kipi kitumike kigezo? Mechi 6 au 60?
Ukiwa unacheza ligi ya English ni ngumu kupata balon d'Or.....!!
 
Unataka compare thamani ya Worldcup & Uefa??? Unajua soka kweli
WCup unalinganisha na uefa ? Au unaangalia kombe lenye pesa ?? Kwenye balon d'Or hyo ni tuzo ya dunia inaangazia mafanikio ngaz ya club na mafanikio ngazi ya timu ya Taifa boss .... Kwa taarifa yako WC ndo kombe lenye nguvu Zaid kuliko kombe lolote chini ya jua
 
Hv ni Nani anabishana na hvi viazi aisee... Kama hamjui kitu ni Bora ukatulia ukajifunza
 
Hao wote mafanikio Yao Kwa kiasi kikubwa yaliangazia mchango wao kwenye timu ya Taifa , hata kama haikuchukua kombe Ila mchango wao mpak timu inatolewa ( mara nyingi fainali) ulikuwaje + jina + mafanikio ngaz ya club
 
Niwaondoe wasiwasi kuwa tunzo itaenda kwa haalaand ila kwa mtazamo wangu!


Na kabla sjaandika sana niweke wazi mimi shabiki wa mpira wa messi


ile balon d or ya messi ya 7 alichukua
alishinda ubingwa wa la laiga
aalishinda ubingwa wa copa america
alikuwa mchezaji bora wa mashindano hayo ya copa america
alikuwa top scorer huko copa america na la liga kama skosei

ila sababu nyingine( though it's a conspiracy) ndio alikuwa amefanya move ya kwenda PSG na kumbuka tunzo alipewa akiwa ni mchezaji wa PSG sasa wanasema kumbuka BALLON D OR ni tunzo iliyoasisiwa na wafaransa na hadi leo wanaitoa hao wafaransa, kwahiyo ilikuwa ni kama siasa pia tunzo ibaki kwao maana skumbuki au sjui ni lini tunzo imeenda kwa mchezaji anaecheza league 1, sio mchezaji mfaransa hapana I mean mchezaji anaekiwasha league 1

Turudi kwenye point yangu kwanini mtazamo wangu ni kuwa halaand ana nafasi kubwa??

Ukiachana na nanmba zao yeye na messi nani anastahili zaidi, ila kitendo cha messi na Argentina yake kuchukua WC dhidi ya France wala hakikiwapendeza wafaransa walio wengi and it's something obvious, maana wenzetu utaifa upo juu kuliko vilabu, na wengine pia wanasabisha pia ndio maana messi ameondoka France kwa heshima ya chini ambayo alikuwa aki deserve kama mchezaji mkubwa sana duniani

Najaribu tu kuconnect dots, namna ambavyo hakuwafurahisha kuchukua WC mbele ya rais wao alienda Qatar since Quarter final, namna alivyoondoka PSG Pasi na treatment nzuri na hao mabwana we can simply say tunzo ni zao maana waandaji ni wao na mchakato wanafanya wao na nyingine zote ni blah blah hawajawahi kuweka mambo wazi kuwa wanatumia mfumo gani kumpata huyo mchezaji bora....

Hivyo naona ni rahisi sana kwenda kwa halaand kuliko lapulga na bora iende kwa halaand maana anaweza asiipate tena hahaha
 
Hao wote mafanikio Yao Kwa kiasi kikubwa yaliangazia mchango wao kwenye timu ya Taifa , hata kama haikuchukua kombe Ila mchango wao mpak timu inatolewa ( mara nyingi fainali) ulikuwaje + jina + mafanikio ngaz ya club

Hapo ndipo kwenye point, mafanikio ya club ni muhimu, kitu ambacho kinachompiga chenga Messi, Kufunga magoli kadhaa ligi ya France haiwezi kabisa kuwa ni kipimo cha mafanikio kwenye Club Season Barani Ulaya.
 

kwanini katika mashindano matatu yaliyopita hiyo world cup imeshindwa kutoa Baloon D'or winner?
 
Kuna jamaa nilimwambia Halaand anafunga sana sababu kazungukwa na viungo wazuri akanibishia sana.

Kwani hapo Norway Halland hafungi? habu katizame amechaza mechi ngapi na uone idadi ya magoli aliyofunga. Acha kuongea pumba ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…