Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Wasomi na watumishi wa dini hizi mbili yaani (Uislamu na njia ya Kristu), naomba jibu ya swali langu hili dogo tu,.
Kila linapotajwa jina la YESU au la MUHAMMAD
Huwa mnaongezea na maneno tena kwa unyenyekevu au kwa molali ya hali ya juu huwa mnasema
(REHMA NA AMANI ZIMFIKIE)
Swali langu kwa waislamu
Je, ni Amani gani mnayotaka Muhammad imfikie?
Je, ni Rehma gani hizo mnazomuombea Muhammad kwa Mungu ili ZIMFIKIE?
Na je ni nani huyo aliyetoa ilo agizo?
Yaani ni Muhammad mwenyewe akitaka kuombewa Rehma kutoka kwetu, au ni Mungu mwenyewe ndio anataka tuwaombee mitume yake mwenyewe?
Je kati ya Muhhammadi na sisi yupi wa kumuombea mwenzie REHMA na AMANI kwa Mungu.?
Ukisoma biblia na quran tukufu imetanabaisha kuwa
MUHAMMAD na YESU ni binadamu watakatifu na ni binadamu wasio wahi kutenda dhambi katika maisha yao yote ya duniani.
Maana yake ni watu wa peponi moja kwa moja.
Sasa kuna haja gani ya kuwaombea REHMA NA AMANI.?
Je huko waliko kwani wanahitaji Rehma au Amani?
Nawasilisha.,
Sio kwa ubaya wala kubeza nahitaji kupata tu elimu.
Hiyo ni amri ya Allah SW
Zaidi soma hapa kwenye hii link
Surah Al-Ahzab Ayat 56 (33:56 Quran) With Tafsir