Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Ameonyesha unyenyekevu wa kiwango cha Juu sana ambacho hakijawahi kutokea.
Hii Ni Baada ya Kuhudhuria kikao cha Shina kilichoitishwa na Balozi wa Shina Chamwino mkoani Dodoma. ieleweke ya Kuwa Balozi wa Shina ni Mwenyekiti ngazi ya Shina. Na huko kwenye Mashina ndiko kuliko na Wananchi na wanachama wetu wa CCM na ndiko mipango mbalimbali huanzia huko na hata ushindi wetu wa CCM huanzia huko. Huko ndiko kuliko na kunakopimwa Uhai na uimara wa chama chetu cha Mapinduzi.
Lakini cha kufurahisha na Kugusa ni kitendo na hatua ya Rais wetu Mpendwa na Moyo wa Taifa letu kuketi pamoja na wanachama wengine na kuendelea kusikiliza kikao hicho. Yaani Mama yetu Mpendwa na Nuru ya Taifa letu hakukaa mbele yaani meza kuu.
Bali aliheshimu mamlaka ya Mwenyekiti ama Balozi wa Shina aliyekuwa akiendesha Kikao hicho na kukaa na wanachama wengine licha ya kuwa yeye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama
Huu ni unyenyekevu wa hali ya Juu sana ambao utaupata kwa watu wachache sana viongozi hapa Duniani. Ndio Maana tunasema ya kuwa RAIS Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe Aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu. Hakuna wa kumshusha Rais wetu Mpendwa. Hakuna anayeweza kuondoa upendo wa Rais wetu uliokatika Mioyo ya watanzania.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
View attachment 3585725View attachment 3585725