Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Kumbe tupo wengi:
Nina rekodi kama yako. Nilikuwa na ufaulu mzuri sana na advance nilichaguliwa moja ya shule za vipaji.
Historia ya ufaulu chuoni miaka mitatu nina C moja tu kwenye cheti changu, zilizobaki ni B kwenda juu. Hivyo vyeti vyangu vimeshiba.
Nina vyeti vya taaluma na uongozi.

Popote nilipopata nafasi ya kujitolea au kuajiriwa kwa muda nimekuwa mfanyakazi bora, vyeti ninavyo kama vyote.

Cha ajabu sasa, mwaka wa 10 sijawahi pata ajira rasmi na sasa nipo mtaani najipambania navyojua mwenyewe.

NB: Mimi ndo msomi wa kwanza kutokea kwenye ukoo wetu kwahiyo connection hakuna kabisa.
 
Muangalie na course za kusoma. Kuna course za watu wa kishua wenye connection na za watoto wa maskini wasio na connection.

Ungesoma education au afya I hope ungekuwa umeajiriwa au uko kwenye nafasi nzuri ya kuajiriwa. Tena na hiyo pcm huko kwenye education ingekuwa zamani sana.
 
Ukiangalia record yako ya ufaulu kwa maoni yangu inaonesha trend mbovu ya mahusiano tangu shuleni.

O-level umepata div one peke yako kati ya watu 138
A-level mmepata div one wawili tu
Na chuo trend ni the same.

Connections huwa zinaanza kujengwa level za primary, mtu anaweza asiwe na uwezo mzuri sana class ila ana connections ambazo ukiwa na mahusiano mazuri anaweza kukuconnect na watu ukapata unacho hitaji.

Matokeo na ufaulu wako yanaakisi kiwango flani cha ubinafsi wa kujitenga na kutotaka kushare knowledge na wenzio nao wakafanya vizuri nadhani ni sababu kubwa unastruggle kupata japo ajira pamoja na ufaulu mzuri.

Watu wa aina yako mara nyingi ikitokea hawajabebwa na matokeo yao kwenye kazi/maisha huwa wanapitia unachopitia.

Hujachelewa, change mindset yako, ongeza kiwango chako cha interaction na watu mtaani bila kujali status zao sana ilimradi unaona wanaweza kukuvusha kwa jambo lako.

Ile mindset ya shule kutaka kufaulu prke yako mtaani haiko relevant. Mtaani we ukifanikiwa haizuii mtu mwingine kufanikiwa bali ili ufanikiwe zaidi unahitaji kuzungukwa na walio fanikiwa zaidi pia.

Ukiwa matured utagundua kuwa Maisha ya mtaani ni about improving and helping each other na si kushindana. Mtaani, matokeo ya jitihada za mtu yanategemea zaidi volume ya watu ulionao (network) wakati shule unaweza komaa kivyako na ukatoka na flying colors.
 
M
Miaka 27 bado sana, subiri ufike 45.
 
Record hii ilifanywa na jirani angu mmoja kipindi hcho ni broo.
Nae alisoma Engineering in geology now yuko GGM japo kahustle Ile mbaya.

Nafkiri hizi Faculty ni nzuri na nizawenye uwezo mkubwa ila hazina soko kabisaa.

Huyu jamaa pia alibahatika akapata schoollership Norway akasoma Petroleum engineering.
Ila Bado alipata tabu tuu.
 
Useful post
 
Umeeleza vyema sana mkuu,
Nadhani ukijitia kichwa sana na ubinafsi shuleni si rahisi kutoboa .
 
Mpango wako umekaa vizuri lakini je huyo mtoto wako ana ndoto kama za kwako au unalazimisha afate ndoto zako.
Watoto wengi wa kizazi hiki hawataki kuamuliwa cha kufanya unakuta tayari ana plans zake...na kama anajitambua basi plans zake zinaeleweka.
 
  • Hongera kwa kuhitimu.​
  • Kwa ujuzi ulionao, unaweza ukaangalia aina fulani ya mwamba na kuutambua kuwa una madini?​
  • Kama ni ndiyo, njoo tuanze kukagua miamba miwili mitatu; baada ya hapo tunaweza kupata mtaji ata wa milioni mia mbili, kwa sababu tutauza hayo madini na mtaji utapatikana.​
  • Kama ni hapana, elimu itakuwa haitatui kero zaidi ya kuwa na wingi wa karatasi.​
 
pole sana mkuu,,,,
Mimi Nina record Kama yako mkuu,,,
Usikate tamaaa utapata,,,, ila kwa kipindiiii hikiiii tafutaaa Shule au chuo cha kati,,, nenda upige mapindiii hata kwa nusu mshahara….
Kakaangu alimaliza chuo na course ya telecommunication engineering na akaishia kufundisha mathematics kwa miaka 5 mpk alipopata kazi inayohusu fani yake
Kwa sasa anakula kuku kwa mrija ila joto ya jiwe aliipata
 
Mkuu kama ulivyosema kwenye haya maisha mara nyingine unaamua tu kusoma kitu flani ili mradi usije ukateseka kwenye maisha... Back in 2009 nilikua na one but niliamua tu kusoma education pale udsm ilimradi tu nisije hangaika baadae nibaki kujilaumu kwamba nilikua vizuri darasani but Leo Sina KAZI.... Sasa mtu akisikia jamaa ni teacher basi anajua huyu ni kilaza alifeli kumbe ni kuchekecha maisha...
 
Halafu utakuta kuna mitoto ya wanasiasa tena ni vilaza tu mida hii imeajiriwa inakula kiyoyozi ofcn inasubiri mwisho wa mwezi ufike idake maokoto ya maana hahahhha
 
Kijana, kwanza hongera.
Pili, usikate tamaaa hata siku moja. Kaa chini mshukuru Mungu bado unanguvu na akili. Unaweza kuishi kwa namna yoyote ile na sio lazima uajiriwe. Fikiria cha kufanya mbali na kufikiri kuajiriwa. Wewe ni mpambanaji... kama uliweza pambana darasani naamini hutashindwa pambana katika chochote mbele yako. Waza cha kufanya na Mungu atakuwa upande wako. Mara nyingi Shetani huzuia riziki za mtu.... mtumainie Mungu ukiendelea kupambana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…