Chanzo: www.trt.net.tr
Wanajeshi 4 wa China wadaiwa kufariki kwenye mapigano ya mpaka wa India mwaka 2020
Wanajeshi 4 wa China wameripotiwa kufariki mwaka jana kwenye mzozo wa mpaka wa India katika Bonde la Galvan.
Kulingana na ripoti ya Jeshi la Ukombozi wa Umma (PLA) ya gazeti la siku, ilielezea mapigano ya China na India katika mpaka wa Bonde la Galvan ya Juni 2020 kwa kuandikwa,
"Tangu Aprili 2020, jeshi la kigeni lililohusika limevuka mpaka ili kujenga madaraja na barabara, na kwa makusudi ya kusababisha matatizo kwa kubadilisha hadhi ya mpakani."
Ripoti hiyo pia ilidai kwamba India iliwashambulia jeshi la China na wanajeshi 4 walifariki, ambao ni miongoni waliokuwa wametumwa kwa ajili ya mawasiliano na India.
Katika vyombo vya habari vya China, majina ya wanajeshi yalitangazwa kuwa Çın Hongcün, Çın Şiangrong, Şiao Sıyüen na Vang Cuoran.
Kwa mara ya kwanza, serikali ya China ilitangaza kupoteza wanajeshi katika mapigano ya mpakani.
India ilikuwa imepoteza wanajeshi 20 katika mapigano yaliyotokea mwezi Juni 2020 na kudai kuua wanajeshi 45 wa China na wengine kujeruhiwa, lakini China ilikanusha madai haya.
Katika taarifa baada ya mapigano, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Cao Licien alisema kuwa Bonde la Galvan ni mali ya China, na Cang Shuili ambaye ni Msemaji wa Kikosi cha Ukombozi cha Wananchi wa China Magharibi alisema, "Eneo la Bonde la Galvan daima ni mali ya China."
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Wu Zian alitangaza mnamo Februari 10 kwamba wanajeshi wa China na India walianza kujiondoa kutoka Ziwa la Pangong wakati huo.