Rest in peace Juve'nal Habriymana 1937-1994 (kumbukumbu zangu)

Rest in peace Juve'nal Habriymana 1937-1994 (kumbukumbu zangu)

Ilikua usiku wa tarehe 16/04/1989 ulikua pale Kicukiro safe house kama sikosei zilikuja taarifa kutokea Gisenyi safe house kua usipobadilisha circle ya watu wanaokuzunguka basi utaiingiza nchi kwenye maafa makubwa ya uhasama wa kijamii ama kikabila kuliko ilivyowahi kutokea huko nyuma..Watu uliowaamini walikuangusha sababu walikua na uchu wa madaraka na wapinzani wa serikali yako hasa vikundi vya waasi walikua na uchu wa madaraka pia..Wananchi walikua wamechoshwa na siasa za upendeleo wa kikabila zilizokua zinaendeshwa waziwazi na watu uliowakabidhi madaraka ya kuisimamia kiutendaji serikali yako.

Watu uliowaamini walikuangusha na wakakuondosha mapema sababu ulikua tayari kwa maridhiano ya kitaifa kwa faida ya Taifa la Rwanda sababu ulijua madhara ya vita kwa wananchi wa kawaida hasa hasa wanawake na wazee na wagonjwa na watoto.Rafiki pekee aliyekua na wewe ni Mzee Mobutu Seseseko na hakua mnafiki na wewe unalijua hilo,wengine wooote walikaa kwako kimasilahi..

Nachosikitika mjomba hukupata nafasi ya kuishi mda mrefu ili uone jamii ya watu wanaokuzunguka hasa familia yako wakikua na kua watu wazima uliondoka mapema..Hakuna aliyekamilika ila pamoja na mapungufu yako unakumbukwa kwa mazuri yako pia kama baba,kama mjomba,kama kiongozi,kama rafiki,kama mlezi pia.Unakumbukwa kwa tabasamu lako,utani wako na jina lako la utani""KINANI""ubishani wako,haiba yako na tabia yako ya kuwajali watu wa familia yako (Ukoo wako) haijalishi wamezaliwa na kukulia wapi,,,

Iwe USA au Tanzania au Kenya au Belgium au Ufaransa au Burundi au Zaire(Congo DRC) au Rwanda uliwakumbuka wote kwa hali na mali....Mjomba ni mama ,mjomba ni rafiki ndio maana inakua vigumu kututoka akilini na moyoni......Pumzika kwa amani unakumbukwa na wengi comrade..
Ninakumbuka nilikuwa darasa la kwanza,siku hiyo tulikwenda shule tukarudishwa.Ndege ya marais imetunguliwa walikuwa wanatoka Arusha kwenye mkutano wa mapatano.Kweli Kagame ni hatari
 
Alionekana kwenye ka clip anachechemea yaani unakaa madarakani hadi miguu inagoma kwenda!!?hawakujifunza KWA nyerere baba YAO!!?

Hawa jamaa wanatia aibu!!
Juzi Kaguta katembelewa na COVID-19 je ni mwanzo wa mwisho wake? Anything is possible under the Sun. Hakuna atakayeishi milele angalia walivyomsingizia Amin akaishi muda mrefu kuliko hata Nyerere mwenyewe
 
Wanajeshi wake aliowaamini kabisa ndio walimgeuka na ndio walihusika na mauaji ya kimbari kwa asilimia kubwa wakishirikiana na vikundi vya wanamgambo na vikundi vya waasi
Mauaji yake kwa theme yanafanana na ya Waziri Mkuu wa Istael Yitzhak Rabin aliepigwa risasi na Mhafidhina wa Kiyahudi Amir Yigal aliekuwa anapinga maridhiano na Israel ambae nae alipigwa Risasi mwaka huo huo
 
Juzi Kaguta katembelewa na COVID-19 je ni mwanzo wa mwisho wake? Anything is possible under the Sun. Hakuna atakayeishi milele angalia walivyomsingizia Amin akaishi muda mrefu kuliko hata Nyerere mwenyewe
Museveni anaumwa wiki ya pili sasa....amelazwa ila kapata nafuu
 
Mauaji yake kwa theme yanafanana na ya Waziri Mkuu wa Istael Yitzhak Rabin aliepigwa risasi na Mhafidhina wa Kiyahudi Amir Yigal aliekuwa anapinga maridhiano na Israel ambae nae alipigwa Risasi mwaka huo huo
Yeah huo mfano sahii kabisa mkuu
 
Ebu fafanua kidogo mkuu

Maana yangu ni hii ,niionavyo rwanda na Maendeleo iliyonayo kwa Sasa huwezi kumtenganisha nayo huyu Nkole/Kagame.

Na Kwa sasa ni kama vile kuna usawa kati ya Hizo jamii mbili apa Rwanda (Tusi na Hawa majority walioko Burundi/Wahutu), ubaguzi sio mkubwa kama vile ulikuwa kipindi hicho cha Mjomba Wako.
 
Nakumbuka nilikua mkura huko Bariadi aiseh!redio free inatangaza usiku!BBC!!
Some of my close relative,s kwenye ukoo walikua kigali tht day...Then walipokea order tu kijeshi jeshi toka kwa Kanali PF """Kimbieni haraka"""mjomba wenu is no more up here and we dont recognize you as rwandese!!!!!So sad for
 
Juzi Kaguta katembelewa na COVID-19 je ni mwanzo wa mwisho wake? Anything is possible under the Sun. Hakuna atakayeishi milele angalia walivyomsingizia Amin akaishi muda mrefu kuliko hata Nyerere mwenyewe

Hivi kwa hilo kwa nini Burundi haikumshitaki Kagame katika mahakama ya kiuhalifu the hague kwa Kumua Rais wa watu wa Burundi ambae hakuwa na hatia ?
 
Maana yangu ni hii ,niionavyo rwanda na Maendeleo iliyonayo kwa Sasa huwezi kumtenganisha nayo huyu Nkole/Kagame.

Na Kwa sasa ni kama vile kuna usawa kati ya Hizo jamii mbili apa Rwanda (Tusi na Hawa majority walioko Burundi/Wahutu), ubaguzi sio mkubwa kama vile ulikuwa kipindi hicho cha Mjomba Wako.
Kuna mengi huyajui mkuu ila vile vile sikupingi sababu mimi nimezaliwa Tanzania...na labda kipindi hicho nilikua dogo janja na mahusiano yangu na uncle yalikua ya kifamilia zaidi kuliko siasa......ila ubaguzi upo sema hapo Rwanda mnaogopa kusema ukweli sababu ya serikali ya RPF.
 
Back
Top Bottom