Upumbavu Sana huu,
Tena UPUUZ Kama huu huu uliwai sababisha nmeish na mke miaka 12 sijafunga nae kabisa Ndoa,
Unakaa zako Unawaza ukishaweka mambo sawa Ubariki ndoa.
Unashangaa mwanamke anakuamsha usiku kukuambia
"Baba D, fanya tufunge ndoa mme wangu. Endapo ikitokea Mungu amekuchukua gafla nitabaki katika mazingira gani"
Unabaki unajiuliza,
"Ina maana uyu mtu anajua kabisa Mimi ndo ntakaetangulia?"
Unaghairi, Unafanya Mambo mengine.
Kuna siku niliwai kukosana na ba mkwe, kisa kunitumia tumia watu wanipush tufunge ndoa.
Ba mkwe anakuita kukuambia
"Mwanangu, fanyeni mfunge Ndoa,
Kuna kesho na keshokutwa Unaweza usiwepo wajukuu wangu uyu akakosa haki zao za msingi"
Nikamjibu TU kwa kifupi Kisha nikaondoka zangu,
"Nikiwa tayar nitakujuza mzee"
sikU moja ikatokea harusi ukweni, tumehudhuria shemej yangu mmoja anafunga Ndoa ya kimila.
Nashangaa Wazee wananiita chumba Cha kumuandaa bwana harusi, nakunikaribisha kiti jirani na bwana harusi mhusika.
Nashangaa kuona wanaingia waandaaji wanaanza kuniandaa Kama alivokua bw.harusi,
Nikamwambia,
"Ebu subiri, Nini kinaendelea hapa"
Wakajibu,
"Tumeelekezwa na mkwe wako tukuandae Kama P na wewe ufunge Ndoa leo leo."
Nikanyanyuka nikatupa makorokoro yao nikaondoka nje.
Niko nje ba mkwe ananifata,
"Vipi kijana mbona umetoka nje wkt Kila kitu Kisha kishaenda sawa"
Nikamwambia,
"Mzee mbona hamkuniandaa kwa zoezi la Ndoa, ninachojua nimekuja hapa kujumuika Kama wanafamilia wengine Kwenye harusi ya shemej yangu"
Akasema,
"Mi mbona mkeo nilimwambia na anajua na maandaliz yote anafahamu"
Nikamuita,
alipokutwa nae akaanza kujiuma Uma eti akajua kwa sababu Nilikua nawasiliana na mzee wake Basi alijua tayar ashaniambia, nikampuuza.
Nikamwambia mzee,
"Kwanza sijawai kufikiri kufunga Ndoa ya kimila, pia siwez kufungia Ndoa ya ukweni nilikooa na pia siwez funga Ndoa bila wazazi wangu au Ndugu zangu kuwepo"
Akasema,
" Sasa itakuaje, na tumeshatumia gharama"
Nikamwambia mzee,
"Mzee wangu Ilo la gharama zenu halinihusu,nnachojua Mimi siwez funga Ndoa sijajiandaa Kama nilivokueleza.
Maandaliz yangu yakiwa tayar nitakueleza na sitegemei kufunga Ndoa ya kimila,ilo sahau kabisa"
Nikapanda zangu usafiri nikarudi zangu KWANGU.
Niliporudi nyumban, na wife akarudi nikamuwakia Sana, nikamwambia
"Kwa mlichokua mnataka kunifanyia uko kwenu. Sitaki kuskia Tena habar za Ndoa nyumba hii, vinginevyo unatafuta ugomvi mkubwa Sana na mimi. hutak kuish na Mimi Basi Rudi kwenu wakakutafutie mwanaume mwingine"
Tangu hapo, Kulikaa kimya Kama Miaka 5 hivi mbele bila habar Tena za kupush Ndoa.
Na ndipo nilipoamua mwenyewe kufunga Ndoa rasmi kabisa ya KIDINI.
MWAKA WA 9 Sasa Kwenye Ndoa Rasmi