Restituta Mbogo: Wakina Mama hakikisheni Wanaume wanaandika majina yenu pindi wanaponunua ardhi

Restituta Mbogo: Wakina Mama hakikisheni Wanaume wanaandika majina yenu pindi wanaponunua ardhi

Je, wa kina mama wakinunua nao watuandikishe majina kina baba?!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
na wanaume tuhakikishe yanaandikwa majina yetu akinamama wanaponunia ardhi na mali myinginezo...au ndio "changu-chetu, chako-chako mwenyewe"...

Ni vyema akapambana ianzishwe sheria kila mali inayotafutwa mkiwa kwenye ndoa badi iandikwe majina ya watoto na mkiachana mali ibaki chini ya mahakama mpaka watoto wafikishe miaka 25.... kama mmeachana hamna watoto basi kila mtu achukue kile alichochuma kwa jacho lake....

Kuwe na mikataba kabla ya ndoa inayosema nani amekuja na nini kwenye ndoa, nani anafanya kazi gani, kila kipato cha mtu kiwe wazi...ili mwisho wa siku kila mtu abaki na chake...na ndoa iwe ni sehemu ya kuburudishana tu na kutafuta watoto.....
Binafsi yangu mimi huwa siyo muumini wa kuandika jina la Mtoto katika Mali zangu
Mtoto anastahili Malezi bora kutoka kwa wazazi lakini siyo kuandikana katika mali ili iweje kwanza.?
 
Ukweli ni kwamba, baada ya safari ngumu ya kutafuta na kulea watoto wakafikia utu uzima, siku za mwanaume huwa zinaanza kuhesabika.

Ndio maana wazee wa zamani ilikuwa mtoto wa kwanza, hasa wa kiume akielekea au akioa. Nae anaoa mke wa pili. Na kuhamishia kila kitu kwa mke mdogo.

Kwa sababu, wanawake wanajuana. Ndo maana wazungu wanakamsemo kao "it takes a monster to fight a monster". Mkubwa akitaka kukutoa relini, mdogo anajibu mapigo.

Siku chache zilizopita kuna jirani yetu kafariki kwa ukweli uliowazi. Akauawa na mkewe.

Tuishi nao kwa akili.
Hapo kwenye kuishi nao kwa akili ndio pa muhimu sana...
 
Naye Mbunge viti maalum Mhe. Sophia Mwakagenda akitoa taarifa bungeni ameungana na hoja iliyowasilishwa na Mhe. Restituta.
1622102097893.png
 
Nafikiri huyu Restituta anaongelea kina mama wanaokwapua waume za wau aka Nyumba ndogo, ni kweli hili wahakikishe hivyo.

Ila kwa Nyumba kubwa by defalt mali za baba / Mama zote kwa ujumla ni mali za familia - yeyote akitangulia anayebakia basi mali zote zinakuwa chini yake akisaidiana na watoto, sasa anaweza kuandika jina la mke ama la mtoto kama hobby tu lakini si lazima eti kwa kigezo cha kudhurumiana..
 
Na wao wakinunua ardhi watuandike majina yetu,au wao wakinunua ni ya kwao peke yao......?
Hii ni obvious mmoja wa wanandoa akinunua kitu mwenzake kuandikishwa siyo dhambi
 
Binafsi yangu mimi huwa siyo muumini wa kuandika jina la Mtoto katika Mali zangu
Mtoto anastahili Malezi bora kutoka kwa wazazi lakini siyo kuandikana katika mali ili iweje kwanza.?
inasaidia kutunza mali endapo utaondoka ghafla kabla yao
inaweza kuwasogeza katika maisha kama ukiondoka wakiwa hawajafikia kujitegemea
 
Kwani tatizo ni nini, alete kalamu aandikwe hapo pembeni, mambo mengi muda mchache...
 
Nafikiri huyu Restituta anaongelea kina mama wanaokwapua waume za wau aka Nyumba ndogo, ni kweli hili wahakikishe hivyo.

Ila kwa Nyumba kubwa by defalt mali za baba / Mama zote kwa ujumla ni mali za familia - yeyote akitangulia anayebakia basi mali zote zinakuwa chini yake akisaidiana na watoto, sasa anaweza kuandika jina la mke ama la mtoto kama hobby tu lakini si lazima eti kwa kigezo cha kudhurumiana..
Mkuu ni bora sheria ya mirathi itamke hivyo, vinginevyo wanawake huwa wanapambana na joto ya jiwe kutoka kwenye familia za wanaume.
 
Ahsante, na hii inatukuta wanaume wengi sana sema hatufahamu ila wana siri kubwa sana mioyoni mwao
Mzee ni mwendo wa usir na mfumo dume ndo utawaweza ukijidai una activate biashara ya Beijing home kwako, utakula upende wako mkuu 🤣🤣
 
Leo nilikuwa nafanya research ndogo ya maeneo niliokulia,wababa karibia wote wameshakufa ila wake zao wote wapo hai,hapa nimeangalia familia zaidi ya 20 za majirani zetu,nadhani wanalijua hili kuwa sisi tunatangulia kufa zaidi kuliko wao,ndio maana wanapambana sana inapokuja swala la mali...
Siyo kwamba wanatuua!?
 
Back
Top Bottom