Rev. Moses Maghembe ajitoa T.A.G

Rev. Moses Maghembe ajitoa T.A.G

Kimsingi mitandao ni mizuri ila wa mitandaoni ni changamoto kubwa sana mnaandika vitu bila kuhoji pande usika ambazo zingesaidia kupata habari sahihi na mkaandika ili uma upate kitu cha msingi, nimesoma hapa mwingine anasema TAG imekwisha sasa unajiuliza kwa lipi TAG imekwisha? Naomba niwape hapa ukweli kilichotokea:-
1, Mzee magembe kaanzisha dhehebu lake linaitwa PCC na lina matawi mpaka Kanada na huko msumbiji

2) kamsimika mke wake kuwa Askofu mkuu hapa Tanzania na kijana wake kuwa senior pastor

3) makao makuu ya Dunia ya dini hii yatakuwa mwenge Dar es salaam

4) yeye ndo mwanziliishi wa hilo dhehebu Duniani,
Kwa mazingira hayo mnategemea atabaki TAG?

Jambo lingine Mzee kawaita viongozi kakabidhi Mali zote za TAG kwa amani bila msuguano wowote sasa mlitaka viongozi wasipeleke mchungaji hapo T. A. G Majumba sita?

Hebu msipende kuandika vitu bila taarifa sahihi.
Asante kwa ufafanuzi mzuri
 
moderator weka hii video kwenye post
 
Attachments

  • AQNqwJz93FI3L1X83Zm22fsqFlzVZv9RrezR1WDx9U427zvypp0fUgX_z3uu51AhgWzLhqSNvkK5UKaeefAT1mIy.mp4
    32.7 MB
Magembe hakuwa vizuri alitofautiana sana na viongozi wenzie alikuwa hahubiri Yesu alikuwa akihubiri dhehebu la TAG kuwa limepotoka na mapungufu yake

Yesu kila anayemtuma humtuma kuwa akahubiri habari za Yesu sio za dhehebu limepotoka au kuhubiri habari za wanakwaya au madhehebu mengi mabovu nk au wachungaji wabovu,au masskofu wabovu nk

Alitoka kwenye line ya kuhubiri Yesu muda mrefu tu

Pili shida yake pia aliamini dìni ndio huokoa na dini bora ni Tanzania Assemblies of God tofauti na Askofu Mtokambali ambaye muda wote amekuwa akisisitiza kuwa haya madhehebu ikiwemo TAG yanatambuliwa tu na msajili mbinguni ni wale tu watakatifu ndio hutambuliwa

Moses Magembe kosa lingine alifanya ni kumponda Moses Kulola tena atubu amvaye hata viongozi wakuu wa TAG wengi waliopo juu huwa hawataki kumuongelea vibaya sababu waliokoka mikononi mwake

Lingine Moses Magembe ni mtu wa kwenye Holliness Movement lakini hayuko strong magotini kuomba kwa nguvu Mungu alete Holliness kanisani .Yuko very strong mdomoni kukemea unholliness kanisani sio magotini kama revivalists waliopita wawe akina Martin Luther nk Magembe mdomoni yuko very strong kukemea maovu sio magotini.Matengenezo ya kanisa hataji kwa mdomo strong bali kwa magoti strong

Yeye matengenezo yake ya kanisa yako mdomoni sio magotini.Matengenezo ya kanisa yalianzia magotini sio mdomoni abaongea sana magotini kuomba matengenezo yuko zero Kutwa kusoma matabu ya apologetics kukesha maktaba badala ya kukesha magotini kuwa ohh Mungu leta uamsho na matengenezo ndani ya kanisa

Anashinda kutwa kuzurura na mahubiri ya mapungufu ya kanisa la TAG na viongozi

Anyway huko aendako kuna vitu atajua kuwa kuanzisha dhehebu sio mbadala wa magoti kwenye uamsho

Hakuna dhehebu lililopo au jipya lake laweza leta uamsho na matengenezo ya kanisa nje ya magoti

Asome upya historia za revivalists zilianzia magotini sio mdomoni kuponda waliopo
Magembe anaongelea sana uamsho mdomoni hamfikii hata Robo Moses kulola wala former Revivalists waliokuwa wakijikita magotini ndio maana wengi mno waliokoka huduma ya Kulola nk japo hakuwa mhubiri mzuri kama Magembe mtheolojia mbobezi msoma mitabu kama yote ya apologetics na mdini mbobezi wa TAG kutetea TAG kama dini bora ya kwenda mbinguni kinyume hata na msimamo wa Askofu wake Mtokambali

Huko aendako ajirekebishe hakuna uamsho huja kwa kuchonga mdomo na kuponda wengine ..Huja kwa kupitia magotini sio mdomoni pekee kwenye mahubiri
 
Mchungaji mwenye msimamo mkali inapokuja suala la kumtumikia Mungu aliye hai Rev. Moses Maghembe ameamua kujiondoa kuwa chini ya usimamizi wa kanisa la mahali pamoja laTanzania Assemblies of God T.A.G

Kama ilivyokuwa kwa wajina wa Maghembe, alikuwepo Moses Kulola ambaye alijitenga na T.A.G na kuanzisha E.A.G.T kwa kutokukubaliana na baadhi ya misingi ya kanisa haswa inapokuja suala la kumtumikia Mungu ipasavyo. Wengi tunafahamu uhodari wa Moses Kulola na huduma yake katika kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Rev. Maghembe ndiye mchungaji pekee alikuwa na uthubutu wa kukosoa uongozi wa askofu Mkuu wa kanisa la T.A.G Dr. Barnabas Mtokambali. Alikosoa kitendo cha kanisa la kiroho kutoa tuzo ya amani kwa mwendazake wakati matukio ya mauaji yalikuwa juu.

Pia alikosoa waziwazi maadhimisho ya chama cha vijana ndani ya kanisa C.A.S yaliyofanyika Iringa kwa kufanya bonanza la mpira wa miguu. Maghembe alidai ile siyo njia ya kuhubiri injili ila ni kuishiwa kwa maono na kanisa kuanza kuiga mambo ya kidunia, kanisa linatakiwa kuleta athari duniani na siyo dunia ilete athari kanisani

Kuwa na ministry binafsi au kuwa chini ya uongozi. Wewe uko upande gani?

View attachment 3180718

View: https://www.youtube.com/live/P2ZQ2HTr3ug?si=4aiaZq64KUPIuN6r
 
Magembe hakuwa vizuri alitofautiana sana na viongozi wenzie alikuwa hahubiri Yesu alikuwa akihubiri dhehebu la TAG kuwa limepotoka na mapungufu yake

Yesu kila anayemtuma humtuma kuwa akahubiri habari za Yesu sio za dhehebu limepotoka au kuhubiri habari za wanakwaya au madhehebu mengi mabovu nk au wachungaji wabovu,au masskofu wabovu nk

Alitoka kwenye line ya kuhubiri Yesu muda mrefu tu
Si kweli, amekuwa akihubiri Uamsho na Matengenezo. Na amekuwa akisema ni wapi kanisa lilipokosea na pia amemhubiri sana Yesu, katika mwaka huu hapa Tanzania simjui mhubiri aliyezunguka mikoani kumhubiri Yesu na watu wengi wakaokoka kama Moses Magembe. Kwa hiyo Yesu anamhubiri sana lakini pia ndani ya mikutano yake amekuwa akilieleza kanisa lilipopotoka na hicho ndicho alichopewa na Mungu.

Pili shida yake pia aliamini dìni ndio huokoa na dini bora ni Tanzania Assemblies of God tofauti na Askofu Mtokambali ambaye muda wote amekuwa akisisitiza kuwa haya madhehebu ikiwemo TAG yanatambuliwa tu na msajili mbinguni ni wale tu watakatifu ndio hutambuliwa
Labda kama umeweka tafsiri yako juu ya kile ambacho huwa anakisema, Ningekuwa na video clip ningekuwekea mara kadhaa amekuwa akisema madhehebu ni kama kampuni za mabasi lakini akionya yako mabasi ambayo Engine ikiharibika using'ang'anie kubaki humo. Anachoonya mzee ni Imani potofu zilizoibuka siku za leo lakini hajawahi kuhubiri kwamba dini bora ni TAG. Na nimeshamsikia zaidi ya mara moja akisema hakuna uamsho wa dhehebu moja akimaanisha ili uamsho uitwe uamsho, lazima ihusishe mwili wa Kristo wote

Moses Magembe kosa lingine alifanya ni kumponda Moses Kulola tena atubu amvaye hata viongozi wakuu wa TAG wengi waliopo juu huwa hawataki kumuongelea vibaya sababu waliokoka mikononi mwake
Hapa sio tu unamsingizia bali nakushangaa, maana ilifika mahali mpaka nikawaza kuna uwezekano viongozi wake wakajisikia vibaya kwa jinsi alivyokuwa akimsifia Moses Kulola, nasema hivi kwa sababu mara nyingi amehubiri kwamba zamani Tanzania ilikuwa na wainjilisti watatu Kulola, Lazaro na Kiwia na nchi ilitikisika lakini leo kuna mamia ya wainjilisti na hakuna matokeo. Amemtaja kwa kumsifia sana Kulola mara nyingi, sijawahi kukutana na video akimsema vibaya.

Lingine Moses Magembe ni mtu wa kwenye Holliness Movement lakini hayuko strong magotini kuomba kwa nguvu Mungu alete Holliness kanisani .Yuko very strong mdomoni kukemea unholliness kanisani sio magotini kama revivalists waliopita wawe akina Martin Luther nk Magembe mdomoni yuko very strong kukemea maovu sio magotini.Matengenezo ya kanisa hataji kwa mdomo strong bali kwa magoti strong
Hili la kukaa magotini sijui umejuaje kama Magembe sio mwombaji, labda kama unaishi naye. Lakini kwa ninavyomfahamu na nilivyomsikia yule ni mwombaji aisee. Kuna wakati alisema kuna vijana wakiona namna anavyomtafuta Mungu kwa kufunga huwa wanaogopa kufikiria kupokea kijiti. Ni mwombaji na siku za karibuni nilimsikia akilitaka kanisa lake kuwa na maombi ya siku 40 kwa ajili ya uamsho na kama uamsho haujatokea bado ataitisha tena mpaka uamsho utokee. Kabla sijasikiliza pande zote mbili nilifikiri labda hii inaweza ikawa ni sababu ya TAG kutaka ajiondoe lakini kumbe sio, kwa hiyo ni mwombaji ila binafsi siko naye karibu kuthibitisha anatumia masaa mangapi kila siku magotini labda kama wewe unamfahamu zaidi.

Asome upya historia za revivalists zilianzia magotini sio mdomoni kuponda waliopo
Magembe anaongelea sana uamsho mdomoni hamfikii hata Robo Moses kulola wala former Revivalists waliokuwa wakijikita magotini ndio maana wengi mno waliokoka huduma ya Kulola nk japo hakuwa mhubiri mzuri kama Magembe mtheolojia mbobezi msoma mitabu kama yote ya apologetics na mdini mbobezi wa TAG kutetea TAG kama dini bora ya kwenda mbinguni kinyume hata na msimamo wa Askofu wake Mtokambali
Mungu akurehemu, Hakuna mashindano kwenye kazi ya Mungu. Kulola alikuwa chombo cha Mungu kwa wakati wake na Magembe ni chombo cha Mungu kwa wakati huu. Mwenye kupima kazi ni Mungu atakayegawa taji, Magembe pia amezaa wachungaji na watumishi wengi, makanisa ndani na nje ya nchi na mpaka amefungua chuo cha Biblia nje ya nchi. Shida ya Magembe inayowatesa wengi ni kuwa transparent sana, inapotokea anakosoa imani potofu huwa hana kupepesa macho.
 
M

Msikilize kwenye hiyo link
 
Si kweli, amekuwa akihubiri Uamsho na Matengenezo. Na amekuwa akisema ni wapi kanisa lilipokosea na pia amemhubiri sana Yesu, katika mwaka huu hapa Tanzania simjui mhubiri aliyezunguka mikoani kumhubiri Yesu na watu wengi wakaokoka kama Moses Magembe. Kwa hiyo Yesu anamhubiri sana lakini pia ndani ya mikutano yake amekuwa akilieleza kanisa lilipopotoka na hicho ndicho alichopewa na Mungu.

Labda kama umeweka tafsiri yako juu ya kile ambacho huwa anakisema, Ningekuwa na video clip ningekuwekea mara kadhaa amekuwa akisema madhehebu ni kama kampuni za mabasi lakini akionya yako mabasi ambayo Engine ikiharibika using'ang'anie kubaki humo. Anachoonya mzee ni Imani potofu zilizoibuka siku za leo lakini hajawahi kuhubiri kwamba dini bora ni TAG. Na nimeshamsikia zaidi ya mara moja akisema hakuna uamsho wa dhehebu moja akimaanisha ili uamsho uitwe uamsho, lazima ihusishe mwili wa Kristo wote

Hapa sio tu unamsingizia bali nakushangaa, maana ilifika mahali mpaka nikawaza kuna uwezekano viongozi wake wakajisikia vibaya kwa jinsi alivyokuwa akimsifia Moses Kulola, nasema hivi kwa sababu mara nyingi amehubiri kwamba zamani Tanzania ilikuwa na wainjilisti watatu Kulola, Lazaro na Kiwia na nchi ilitikisika lakini leo kuna mamia ya wainjilisti na hakuna matokeo. Amemtaja kwa kumsifia sana Kulola mara nyingi, sijawahi kukutana na video akimsema vibaya.

Hili la kukaa magotini sijui umejuaje kama Magembe sio mwombaji, labda kama unaishi naye. Lakini kwa ninavyomfahamu na nilivyomsikia yule ni mwombaji aisee. Kuna wakati alisema kuna vijana wakiona namna anavyomtafuta Mungu kwa kufunga huwa wanaogopa kufikiria kupokea kijiti. Ni mwombaji na siku za karibuni nilimsikia akilitaka kanisa lake kuwa na maombi ya siku 40 kwa ajili ya uamsho na kama uamsho haujatokea bado ataitisha tena mpaka uamsho utokee. Kabla sijasikiliza pande zote mbili nilifikiri labda hii inaweza ikawa ni sababu ya TAG kutaka ajiondoe lakini kumbe sio, kwa hiyo ni mwombaji ila binafsi siko naye karibu kuthibitisha anatumia masaa mangapi kila siku magotini labda kama wewe unamfahamu zaidi.

Mungu akurehemu, Hakuna mashindano kwenye kazi ya Mungu. Kulola alikuwa chombo cha Mungu kwa wakati wake na Magembe ni chombo cha Mungu kwa wakati huu. Mwenye kupima kazi ni Mungu atakayegawa taji, Magembe pia amezaa wachungaji na watumishi wengi, makanisa ndani na nje ya nchi na mpaka amefungua chuo cha Biblia nje ya nchi. Shida ya Magembe inayowatesa wengi ni kuwa transparent sana, inapotokea anakosoa imani potofu huwa hana kupepesa macho.
Yesu hakutuma mhubiri yeyote akahubiri kanisa lipi zuri au baya alisemal wahubiriwe watu ndio wawezao kuokoka na kuacha dhambi sio dhehebu liwe TAG au lolote wameokoka au hawajaokoka

Injili ni habari njema kwa watu sio kwa madhehebu yawe katoliki,lutheran ,pentecoste nk

Kuzaa makanisa ndani ya nchi na nje haina maana kanisa limeongezeka

Kipimo kikubwa cha kukua kwa kanisa sio idadi ni quality za kiroho za waumini hata wawe mia

Kipimo sio kuwa na mabilioni wajati kiroho wako zero
 
Yani bora wale wazee wa vibegi na makofia yao makubwaa bila kusahau kimkoba wanaitwa mashahidi wa Jehova wale ni bampa tu bampa wakikutembelea siku moja sahau kuwakwepa hata ukijificha juu ya dar utapewa mahubiri huko huko darini ,

Wanatembea kimakundi makundi hivi hao kupiga kilometa 30 40 kwao sio ishu kabisaaa , hutawahi wasikia wanagombana [emoji1787][emoji1787][emoji1787] alafu nilitaka kusahau wanakua na wazungu wao nao kwa kusaga kwato hawajambo.

Wanajua kung’ang’ania wale.. nakumbuka enzi nikiwa mdogo wakija mama ananiambia niseme hayupo [emoji23]
 
Yesu hakutuma mhubiri yeyote akahubiri kanisa lipi zuri au baya alisemal wahubiriwe watu ndio wawezao kuokoka na kuacha dhambi sio dhehebu liwe TAG au lolote wameokoka au hawajaokoka

Injili ni habari njema kwa watu sio kwa madhehebu yawe katoliki,lutheran ,pentecoste nk

Kuzaa makanisa ndani ya nchi na nje haina maana kanisa limeongezeka

Kipimo kikubwa cha kukua kwa kanisa sio idadi ni quality za kiroho za waumini hata wawe mia

Kipimo sio kuwa na mabilioni wajati kiroho wako zero
Mkuu, jaribu kutafuta video zake akiwa anahubiri. Hajawahi kuhubiri kanisa gani zuri au kanisa gani baya. Anamhubiri Yesu na miaka ya hivi karibuni amehubiri sana kuhusu siku za mwisho na kurudi kwa Yesu. Lakini pia anawaonya watu kuhusu imani potofu, sasa watu wakishaokoka lazima walelewe chini ya kanisa, wakilelewa chini ya kanisa lenye imani potofu au misingi mibaya hao watu watarudi nyuma tena. Mtu anaweza kuokoka akiwa dhehebu lolote lakini sio kila dhehebu ni salama kulelewa kiroho. Kama unasema unamjua Moses Kulola fuatilia uone hata Kulola alionya waumini wake kuhusu hili kabla ya kuondoka duniani.

Nimekwambia Magembe amezaa makanisa na watumishi wengi kukuonesha kwamba anafanya kazi kubwa kwenye ufalme wa Mungu na anamhubiri Yesu sana, sijamaanisha watu kujaa kwenye kanisa peke yake ndo kwamba automatically kanisa linakuwa na quality nzuri. Katika hali ya kawaida kama unazaa kisicho bora ni ngumu wale unaowazaa kuaminika kuwa wachungaji au maaskofu. Asilimia kubwa ya wanaotokea kwenye kanisa lake wanakuwa na kiroho kizuri na wanakuwa baraka hata kwenye makanisa mengine. Sijui hata kama unayemtuhumu unamfahamu vizuri.
 
Mchungaji mwenye msimamo mkali inapokuja suala la kumtumikia Mungu aliye hai Rev. Moses Maghembe ameamua kujiondoa kuwa chini ya usimamizi wa kanisa la mahali pamoja laTanzania Assemblies of God T.A.G

Kama ilivyokuwa kwa wajina wa Maghembe, alikuwepo Moses Kulola ambaye alijitenga na T.A.G na kuanzisha E.A.G.T kwa kutokukubaliana na baadhi ya misingi ya kanisa haswa inapokuja suala la kumtumikia Mungu ipasavyo. Wengi tunafahamu uhodari wa Moses Kulola na huduma yake katika kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Rev. Maghembe ndiye mchungaji pekee alikuwa na uthubutu wa kukosoa uongozi wa askofu Mkuu wa kanisa la T.A.G Dr. Barnabas Mtokambali. Alikosoa kitendo cha kanisa la kiroho kutoa tuzo ya amani kwa mwendazake wakati matukio ya mauaji yalikuwa juu.

Pia alikosoa waziwazi maadhimisho ya chama cha vijana ndani ya kanisa C.A.S yaliyofanyika Iringa kwa kufanya bonanza la mpira wa miguu. Maghembe alidai ile siyo njia ya kuhubiri injili ila ni kuishiwa kwa maono na kanisa kuanza kuiga mambo ya kidunia, kanisa linatakiwa kuleta athari duniani na siyo dunia ilete athari kanisani

Kuwa na ministry binafsi au kuwa chini ya uongozi. Wewe uko upande gani?

View attachment 3180718
Ahamie ccm
 
Back
Top Bottom