Mwanaume wa kweli haumizwi na mwanamke hata siku moja, unajinyima unampa yeye huyo mkeo? Haya ni maneno ya kishujaa tu sio chochote unachoweza kumfanyia maana dume kamili huwezi lialia huku mbele ya Umma ila ungefanya tu kwa kitendo ukutane na sheria ukavunje mawe maweni tanga kwa ujenzi wa Taifa.
Wewe umekutana na mtu keshapendeza unataka kujimilikisha kirahisi kimikwara unajua alikotokea mpaka akakuvutia? Kila mtu na uhuru wake, sio mkeo huyo na hakukutongoza wala hajakutuma kumgarimikia, tumia akili wakati mwingine badala ya ujinga.