Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Yaani Bina inahuzunisha
Sasa alikuwa anakuambia mambo yake ya hovyo jamani...Kwa style hiyo ashindwe kudundwa kweli[emoji23]
Mtu una mwanaume ana nia thabiti na anakuhudumia vizuri, sijui unataka nini tena jamani!
Ila wanawake sisi[emoji1544]

Jamaa amefanya sahihi kumuacha, Sema kaumiza pia na wazazi wake ambao hawana Hatia na sidhani kama walikuwa wanajua chochote kuhusu upuuzi wa huyo binti Yao.
Kweli mchuma janga hula na wakwao.
Yaani hivi vitoto vya siku hivii hovyoo Sanaa
Kabisa mchumba janga hula na Wa kwao na huyo dada km inawezekana amkve on kabisa aachane kabisa na story za visasi na mshikaji itamcost Sanaa....ni Bora akubali yaishe tu afanye mengine

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Yaani hivi vitoto vya siku hivii hovyoo Sanaa
Kabisa mchumba janga hula na Wa kwao na huyo dada km inawezekana amkve on kabisa aachane kabisa na story za visasi na mshikaji itamcost Sanaa....ni Bora akubali yaishe tu afanye mengine

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ngoja tuone picha linaelekea wapi
Mungu awaepushie mabalaa maana visasi mwisho wake huwa siyo mzuri.
 
nina roho ngumu kama ya mkuu KOROE
nilimtimua mwanamke akiwa na ujauzito miezi tisa kabisa nikamrudisha kwao na ndoa ikafa.

alifika akakaa wiki moja akajifungua

Nilikataa kabisa kushauriwa na.mtu yeyote kuanzia mama, kaka zangu n.k

nikaonekana mi mbaya sana ila cha ajabu na yeye akaolewa tena ndoa haikukaa hata mwezi ikafašŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…

mpaka sasa ni single mother at the age of 24
 
TUENDELEE..

Jioni ile binti alizinduka, lakin Daktari akaomba binti abaki wodin maana mapigo yake ya moyo hayapo vizuri na presha ipo juu kupita maelezo, lakin kutokana na nature ya tatizo lenyewe ni bora binti abaki kwa uangalizi na counseling maana anaweza kuchukua maamuzi mabaya, binti akabaki hospital na mama yake, wengine wakarudi home. Jioni ikafika kikao kikaitishwa.

Baba wa binti akaongea mengi km kunilauma mim, nikaon ananiletea uhuni, nikamchana kwamba nilishamweleza kwamba akifanya ushenzi namim nitafanya ushenz na hizo msg kwenye simu zipo na kama binti atakataa nazionesha vile vile jinsi tulivyokubaliana, basi ikabid busara zitumike, hasa mjomba wake ambaye alijitahidi kutuomb radhi kwa binti yao kukosa maadili kiasi kile japo limekuja wakat mbaya lakin lmesaidia sana kuelewa uhalisia wa binti yao ambao walikuwa hawaujui.

Baada ya dk kidogo mama yake akaja kutoka hospital akatukuta kwenye kikao, akaomba sana niende hospital nikamuone binti yake maana hakuna anachotaka zaid ya mimi na hayupo tayari kuishi km sitamsamehe, akaniomba sana niende hospital nikamtamkie msamaha hata wa kinafiki, nikakataa na sikwenda, nikawaambia wazee tusepe hapa hakuna jipya tena, hapakuwa na jins maana nilikaza kila kona, moyo wangu kwa dhati ulikusudia kulipa kisasi.

Nikatoka nje nikawaacha wazee wakiongea ongea, usiku ulikuwa umeshaingia tukaingia kwenye gari safari ya kwenda hom ikaanza.

Nyumban taarifa zilikuwa zimeshafika, kuna ambao waliona sawa na kuna wajinga na dhaifu wakasema ningesamehe tu nimuoe, wapuuzi.

Maisha mapya yalianza, siku moja nikawa nipo porini huko kwenye mishe zangu zikiwa zimepita km siku 4 hivi nikapigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwamba ni mwasaikolojia, akanambia kuhusu lile tukio na kwamba anaomba niongee na yule binti chochote kwa kuwa hataki kula na muda wote anachungwa maana anaonesha dalili zote za kutafuta namna ya kujinyonga, nikakataa. Nikamwambia aachane namimi kabisa.

Simu zilikuwa nying, mama yake, baba, na ndugu zake wengine lakin sikuwa na mpango tena, nikaona nibadili laini za simu zote. Nikajua nimesolve tatizo sasa, of course wakawa wanaongea na mzee wakiomba aongee namim niongee chochote na binti yao, nikakataa. Miezi kadhaa ikapita, siku moja nikiwa Tanga huko nikapokea simu ya rafik yangu akanijuza kwamba yule binti amekuja ghafla kwake, amekonda na kuchakaa. Kumbe alikuwa ametoroka kwao ili aje anitafute, alikuja kwangu kukawa kumefungwa akaona aende kwa mshikaji.

Nikamwambia kifupi tu, aishi naye pale kwake km anamhitaji ila mim kwa upande wangu ni hapana, jamaa akasema ameoa na ana familia so nafasi pale kwake ni ndogo na binti hataki kuelewa na amekataa kutoka pale kwake akaniomba niongee na yule binti, nikakataa.

Kumbe yule binti aliiba hela za baba ake dukan maana baba ake aliamua kumuweka auze duka la jumla la vifaa vya ujenzj ili angalau apunguze mawazo, akatoka na million 4 akatoroka na kuja kwa mshkaji, akakatalia kutoka hadi anione.

Jamaa akanisimulia mengi kwa kadri binti alivyomuelekeza, Na akaniomba nionane naye ili nimsaidie, nikakataa

Baada ya kukaa km wiki pale jamaa akashindwa ikabid amfukuze kwa nguvu, binti akaamua asafiri aende kwetu kwa wazazi wangu. Muda wote huo kwao hawajui binti yupo wapi, wakaenda kutoa taarifa polisi..

ITAENDELEA WAKUU.

Mrejesho: Sehemu ya tatu
Safi sana huo ndio uanaume.
 
Mzee akanipigia simu na kunieleza ujio wa yule binti pale nyumbani, nikamwambia ampeleke polisi arudi kwao sina muda wa kupoteza kuongelea kitu ambacho jibu lake linajulikana.
šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚
 
baada ya kufika binti akaanza kuangua kilio akisistiza asemehewe, akaomba km itashindikana kbs basi aishi namim km mfanyakazi wangu hata wa ndani, alikuwa anaongea upuuzi.
Bora ulivyomkataa angeweza hata kukuwekea sumu au kufanya kisasi chochote kile kukuadhibu.
 
Nikamwambia aingie kweny gari nimpeleke kwake anakoishi akaanza mapozi yake ya kingese, mara ooh amefanya usafi amechoka, so anaomba apumzike kidogo pale kwangu, sijui nyumba kubwa km ile why aniache peke yangu, mara sijui nina mawazo meng so aniliwaze tupige story then ataenda, nilishajua anataka nin but nikawa namuona km ndezi tu maana sinaga muda na kufanya mapenz na mwanamke nisiye na mpango naye.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
2022-2024, kuna vitu kimetokea very interesting. Kumbe yule jamaa aliyetembea naye aliyekuwa anataka na side B alikuwa HIV+. Na km mnakumbuka tang nigundue kwamba simuelew elewi sikuwahi kulala naye tena, so nipo salama kbs sina VVU..

Ilikuwaje nimejua? Nani alinambia? Kuna mambo yalitokea hapa katikati pia.. kuna msala mzito sana ulitokea wa Polisi kupewa pesa na baba ake binti waje wanifanyie kitu mbaya, labda mzee alijua mi ni mwepesi, ***** moto uliowaka plan ikabackfire hadi polis wakajuta kujiingiza kweny mambo ya kifala, ikapelekea msala kumrudia yule mzee hadi akataka kujinyonga, hii nayo ilikuwaje??

Kuna demu wa JF alikuja PM alijua mim ni Pimbi, ni jimama lina pesa pesa hv kdg, huyu naye ana mkasa wake.. aliyakanyaga huyu, hii naye ilikuwaje?

Wengine pia wanatak kujua yule binti wa Kimburu kiunaga ubaga jinsi nilivyomalizana naye Hadi nikampiga chini, hapa napo pana balaa lake zito pia.

Mambo yapo mengi, nipo chaka sana kwasasa nafanya project moja hivi tough sana.. but Nitarudi niwape mikasa yote hii.

Andaa popcorn zako.

NB: kuna ambao wanadhan huu mkasa ni uongo, siku moja mbele ya safari nitafanya interview na nitawajuza, ila sio hv karibuni.
Hatari sana
 
Back
Top Bottom