TUENDELEE...
Nikaona mambo yasiwe mengi, nikamwambia poa aende akamrudishe rafiki yake kwenye ndoa yake and mimi nitamfkiria kuhusu ombi lake, nilishajua tayari ashakuwa dhaifu kwangu so hawezi kunizid maujanja, hata km anasema uongo bado hauwez kuniathiri maana lazima nimzid akili, kwanza ananipenda kimapenz hivyo tayari yupo kwenye ugonjwa wa akili hawezi kushindana namimi mwenye akili timamu, and nikapanga kabisa kwamba siwezi kuwa naye yule manzi.
Akaenda akamdanganya kwamba nimepata ajali na nina hali mbaya nimekimbizwa India, na kwa jinsi hali ilivyo sijui km nikipona nitabaki na uwezo wa kufanya chochote Kwahiyo akamwambia rafiki yake akakomae tu na ndoa yake, na akaishi na yule mwanaume maana kwangu tena maji yameshamwagika, binti akaona hakuna jinsi akarudi kwa mume wake, jamaa ndo hivyo akampokea maana ndo km anakopatia ridhiki, nasikia kumbe kipindi anakuja huku alikuwa tayari kanasa ujauzito wa mshikaji, ndo huyu rafiki yake akawa ananiambia alikuja kugundua baadaye km ni mjamzito means km mimi ningejichangnya kuwa naye kipind hiki basi ningetupiwa hilo zigo kumbe la mume wake huko.
Japo binti hana amani kwenye ndoa ile so dizain km anapanga mbinu amtoroke aende akaishi maisha yake peke yake. Huyu rafiki yake akaniambia yupo kwenye process ya kutoa ile mimba maana hataki kuzaa na mshkaji wake, then apotee kokote akaishi mwenyewe. By the way hainuhusu hiyo sasa, azae asizae, aishi au aondole anajua yeye.
Maisha yangu yameanza upya na dizain km yule demu karidhika na kuamin kwamba sipo nchini nipo India kwa matibabu, maana baadaye ikanilazimu nibadili tena namba za simu, sasa mtihan ninao kwa huyu rafiki yake maana ananipenda na anataka nitimize ahad maana kazi ameshaifanya. Hadi leo sijamla na sitamla, na hili kwangu ni dogo sana na nitalimaliza tu kirahisi.
Nimepata aman sana na sikumbuki ubaya na maumivu yote aliyonitendea yule binti, nimeridhika kwa hiki.
Yapo mambo mengine nimeyaexclude maana stori ingekuwa ndefu sana, ahsanten kwa kunifuatilia tangu mwaka 2017 hadi leo 2021.
MWISHO,