Huruma za kipumbafu huwa mara zote zinapelekea kuleta neno Ningejua. Hivi unayemtetea huyu binti unadhani angesema tu kikaoni pale ninamuacha sitoendelea tena na utoaji wa mahari pangeeleweka!? Baba mtu alikuwa keshaanza kuwaka moto na kumtishia jamaa atampeleka kwenye vyombo vya sheria, wewe unaetetea unaona ni sawa!?
Jamaa alishamtahadharisha binti tangu siku ya kwanza juu ya misimamo yake ila binti akaona, wewe nae ni wale wale tu. Na uzuri wangu huu utachomoka hapa!? Kuna watu huwa wanasema sijui usifuatilie simu ya mkeo sijui mchumba wako, huwa nawaona hawana akili timamu. Nihusike katika kila kitu chako, halafu simu tu, nisihusike nayo!?
Sisi wenye misimamo ya namna hiyo tupo na nilishagasema mimi sinaga rivasi kama pikipiki. Jumamosi moja niligombana na mwanamke nlokuwa naishi nae, akawa anarusha maneno hasa ya kejeli na dhihaka, nikawa namsikiliza tu baadae mi nikalala. Nimeamka hiyo jpili ya kimbunga Jobo nikajiandaa nikaenda mzigoni, narudi jioni nikakuta nyumba yote giza. Nikaangalia tunapowekaga funguo nikaiona, nikaingia ndani sikumkuta na kuna vitu akawa kaondoka navyo bila kunitaarifu wala kuniomba. Nilipoona ile hali nikasikitika tu kisha nikatoa tabasamu ya Uchungu kisha nikasema Sawa, nikafuta namba zake zote. Sijamtafuta mpaka leo wala sina mpango wa kumtafuta maisha.