Ni hatua mbovu ambayo inaenda waumiza wakopaji ambao wengi ni wafanyakazi (bank za Tanzania faida kubwa ni mikopo ya wafanyakazi) na hawa mikopo yao ni kwa sababu ya matumizi muhimu.
Inflation inaweza sababishwa na mambo mengi lakini sababu kuu ni tatu. Demand pull inflation, cost pull inflation na negative externalities kama corruption.
Demand pull inflation ndio mara nyingi unaikabili kwa kuongeza interest rate ili kupunguza supply of money.
Hata hivyo demand pull inflation yenyewe inasababishwa na mambo mengi (mengine ni makusudi, mfano hoarding).
Sasa kabla ya kuongeza interest rate unatakiwa uangalie vitu viwili elasticity of demand. Kwanza, Je? bei ni sensitive kwa walaji, mfano bei pamoja na kupanda bado watu wananunua bidhaa kwa wingi ina maana hakuna price sensitivity bei ikipanda volumes ya manunuzi inatakiwa kupungua.
Criteria ya pili vipi equilibrium ya supply and demand. Mfano matumizi ya sukari Tanzania ni tonne 600,000 kwa mwaka au on average ni tonne 50,000 hiyo ndio equilibrium ya supply and demand ya mwezi on average (ignoring seasonal variations). Lakini unakuta kwa mwezi nchi inatumia mpaka tonne 70,000 huku bei ya sukari inapanda hapo sasa ndio shida ina maana watu wana hela nyingi.
Umevuka equilibrium (on many items za market basket) na bado hakuna dalili ya price elasticity sokoni dawa ni kuongeza interest riba ya mikopo iende juu na ku trigger mambo mengine ya kupunguza hela kwenye mzunguko wa uchumi.
Sasa wewe unaenda kuongeza interest rate wakati asilimia 75% ya walaji wako wanautapia mlo, wapo sensitive to price, supply ipo chini ya equilibrium kwa sababu kadhaa, kuongeza interests si unaenda kutesa walalahoi.
Badala ya kutatua tatizo unaenda tengeneza tatizo (story ni ndefu, kwenye chanzo cha inflation ya Tanzania) Ila walichofanya BoT ni kwa kukariri badala ya kutumia uelewa.