Riba za mikopo kwa watumishi, CRDB na NMB

Nyumba na viwanja vya wananchi vinaumia kwa haya mariba makubwa, achana na salary slip za wafanyakazi ambao nao inawaumiza haya mariba yapunguzwe kuwe na riba elekezi vinginevyo ni vilio tu kwa wananchi.
Sasa riba zisizidi 10% kwa Mwaka naona sababu ya Wananchi kushindwa kulipa madeni benki sasa.
Nyumba na viwanja vingi vinauzwa kwa sababu ya riba kubwa lazima kutokee ugumu Kwenye kulipa tu.
Serikali iweke riba elekezi hakuna namna nyingine
 
riba I = PRT/100
kama R= 17%
p= 12000000
T= 5
12000000x0.17x5= 10200000
riba kwa miaka mitano= 10200000
kwa hiyo ukichukua 12,000,000
riba kwa mwaka 10200000/5=2040000/=

utarudisha hela za watu 22200000/=
kwa miaka mitano
Mkuu kumbuka riba inakata kwa salio la mkopo lililopo kwa maana ni diminishing balance method.
 
Mkuu kumbuka riba inakata kwa salio la mkopo lililopo kwa maana ni diminishing balance method.
Pamoja na hiyo bado riba ni kuwa kiasi kwamba Mwananchi anashawishika kukimbia deni sio kulipa deni na hapa ndio unapoona nyumba zinapigwa minada.
Hata kama ni mpambanaji kiasi gani hii ni ngumu kumeza
RIBA ELEKEZI IJE
 
haya mabenk ni jipu lililoshindikana maana wenye hisa umo ni haohao viongozi wenu wao wanataka faida tu na sio hasara
 
Nimeona wengi wanashindwa kuelewa kidogo kuhusu hizi riba,,,kina mtu apo juu kasema kuwa 18% riba ukiiweka kwenye hesabu ni sawa na 50% au marejesho ni almost mara mbili,,kuna mwingine akajaribukupiga hesabu ya interest(riba)=prt,ntagusia kwa juu juu

Nadhani Mabenki yanavyokokotoa riba ya mikopo ya miaka kadhaa(3,5,etc)wanatumia riba inayozaa riba au compound interest kwa kiingereza na sio simple interest ya i=prt,hii compound interest ni kwamba ile riba inayozalishwa na principal amount inaongezwa kwenye principal amount over time,,hiyo inakua inajiaccumulate na kujiongeza kwenye principle then the new principal ambayo ni (p+i)inazidishwa na riba tena,,,hivyo uo mchezo unaendelea kujirudia na kujirudia over time ya term ya mkopo wako thats y tunaona hicho kiasi ni kikubwa
Kama una muda pitia pitia online ujielemishe kidogo kuhusu "compound interest"
 
haya mabenk ni jipu lililoshindikana maana wenye hisa umo ni haohao viongozi wenu wao wanataka faida tu na sio hasara
Hamna anayetaka hasara ila watengeneze win win situations ambapo wao watapata kidogo na wakopaji watapata vinginevyo itakula sehemu.
Kuna haja maafisa mikopo kutengeneza wateja wao kwa mafunzo na pia kurasimisha mali zao hasa vijijini ili kuwa na wateja wengi kwa riba nafuu pia.
 

Riba ni kwa mwaka wewe,

Pia ogopa taasisi inayotoza riba kwa mwezi, ie bayport utalia!
 
Kwa hiyo kiuhalisia unarufisha mara mbili ya hela uliyochukua

Hapo ndo hapaeleweki.... Sasa mmi niliambiwa na branch manager kwamba nikichukua 12m kwa 5yrs, riba plus principal itakua 18,680,000/=
 
Km huna hiyo m45 unaanzaje?

Lazima ukope.

Mimi pia nilikopa M10 nimeiwekeza duka la mazaga,mpesa simu na spea zake kijijini nakamua faida ya wastani wa 1.5 kwa mwezi (ukitoa gharama zote za uendeshaji)

Naanzia wapi kumshauri mtu asichukue mkopo benki?

Maana kiuhalisia unashindwaje kuzalisha 255,000 kwa mwezi toka mtaji wa m10? Mbona fursa ni nyingi?

Tatizo kila mtu anataka kufanya kitu kilekile mahala palepale siku zote!

Basi we dunduliza chako hata kwa miaka mitano ufanye yako
 

Pamoja na hayo Kiongozi bado Riba ni Mzigo, jana tu nilikua nipo Babati huko basutu kufuatilia mikopo kwa wakulima ni shida kuna baadhi wanajitahidi kwa shida sana na wanaweza ila bado wengi wanaonekana kabisa kwamba ngoma ni ngumu.
Huwezi kutoka bila Mikopo hata kidogo ila lazima tuzungumzie wazi Riba ni kubwa
 

Nchi gani wanatoza riba nafuu kuzidi hapa kwetu?
(obvious zipo)

Unayajua mazingira ya wao kutoza riba ndogo na changamoto za uwekezaji ktk nchi hizo?

Ni kweli nchini kwetu siku zijazo riba itashuka lakini usidhani utaweza kufanya biashara kirahisirahisi kama miaka hii ndugu.
 
Hapo ndo hapaeleweki.... Sasa mmi niliambiwa na branch manager kwamba nikichukua 12m kwa 5yrs, riba plus principal itakua 18,680,000/=
6.68=12x(%)x5
riba kwa hapo ni ndogo
sana mkuu
hizo hiyo ni bank gani
11%
 
Ukweli ni.kuwa riba ni tatizo na ndio maana watu wengi wanaishia.kupoteza nyumba na viwanja vyao. Sasa kwa mazingira hayo kweli kurejesha mkopo hasa ukute ni wakibiashara ambao utakuwa na riba kubwa zaidi si ndio itakuwa ishu zaidi.
ya biashara unakuta mara nyingi riba sio kubwa sana kwasababu mingi ni ya mwaka mmoja na ndio maana riba yake haizidi 24% kwa mwaka
 
Mfano me nilichukua mil 10 nakatwa 253,000 kws miaka mitano mkuu so kwenye mkataba inaonekana mwanzo mwenga,ila crdb is the best kwa wote

kama wanakata 253,000 kwa mwezi, kwa miaka mitano watakuwa wamevhukua 253000 *12*5 ambayo ni sawa na 15180000.

riba=(makato kwa mwaka - mkopo)/mkopo

riba= (15180000-10000000)/10000000=51.8% kwa miaka 5 ambayo ni kama 10% kwa mwaka..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…