Riba za mikopo kwa watumishi, CRDB na NMB

Duuuuuh, kumbeeee
riba I = PRT/100
kama R= 17%
p= 12000000
T= 5
12000000x0.17x5= 10200000
riba kwa miaka mitano= 10200000
kwa hiyo ukichukua 12,000,000
riba kwa mwaka 10200000/5=2040000/=

utarudisha hela za watu 22200000/=
kwa miaka mitano
 
Mfano me nilichukua mil 10 nakatwa 253,000 kws miaka mitano mkuu so kwenye mkataba inaonekana mwanzo mwenga,ila crdb is the best kwa wote
Sasa kama wanakata hiyo kwa miaka mitano it means riba ni 50%
 
Namaliza mkopo wa awali nmb ila naona Kama riba yao ni 31% miaka mitano naomba mnishauri nichukue bank gani yenye auweni na ambayo haina usumbufu kupata
 
Nenda Barclays, riba 22%, mkopo 1,000,000/= mpaka 80,000,000/=.
Muda mwaka mpaka mitano.
 
nahisi umekosea umezunguka kama unaanza kutunga formular au kutafiti wakati formular tayari zipo
 
riba I = PRT/100
kama R= 17%
p= 12000000
T= 5
12000000x0.17x5= 10200000
riba kwa miaka mitano= 10200000
kwa hiyo ukichukua 12,000,000
riba kwa mwaka 10200000/5=2040000/=

utarudisha hela za watu 22200000/=
kwa miaka mitano
Mkuu ulikuja vizuri sana lkn ulipochukua 10,200,000/5=2,040,000/- halafu ukaja kwenye hitimisho kuwa ukichukua 12,000,000/- utarejesha 22,200,000/- hapo nimepotea kabisa.

1. Sijaelewa kwa nini umegawia 10,200,000 kwa 5 kupata hiyo 2,040,000/-
2. Sijaelewa hiyo 2,049,000 inakusudia nini.
3. Nimeelewa 12,000,000+10,200,000= ndo huzaa hiyo 22,000,000 na ukitoa kwa mkopo halisi ni maana yake bank kwa 12,000,000 unawazalishia 10,200,000/-

Rudi ufafanue tena mkuu. Maana 17% ya 12,000,000 ni 2,040,000 ambazo ukijumlisha na 12,000,000=14,040,000/-
 
This mortgage loan calculator - also known as an amortization schedule calculator - lets you estimate your monthly loan repayments. It also determines out how much of your repayments will go towards the principal and how much will go towards interest. Simply input your loan amount, interest rate, loan term and repayment start date then click "Calculate".

BANK LOAN CALCULATOR


 
u best uko wapi? umekopa mil 10 na utalipa mil 15,180,000 hapo umewapa faida mil 5 na ushee. yani riba ni nusu ya ulichokopa.
Ni sawa sawa tu wamekukopesha million 5
Kwa hiyo kiuhalisia unarudisha mara mbili ya hela uliyochukua

Hapo kila mwaka wanakata asilimia 17% ya deni unalodaiwa kwa hiyo kwa miaka kama mitano inaweza hata kuzidi hiyo kutegemeana na makato
 
naomba ufafanu
naomba ufafanuzi hapo kwenye mkopo wa muda mfupi riba ni ndogo na mkopo wa muda mrefu riba ni ndogo nahisi unajichanganya
 
CRDB na NMB mikopo kwa watumishi ni asilimia 18 kwa mwaka..ukichukua milion kumi kwa miaka mitano utarejesha sh milion kumi na nne..kwa mwez watakukata wastani wa sh laki mbili na nusu.
Acha uwongo nimewatembelea wote Crdb wana 17.83 na Nmb wana 20 percent.
Nmb ni jipu kubwa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…