Richard Nzagi: Mafinga ina Watoto wengi wa Kichina, Wachina wanaacha Watoto wengi wanapopita kwenye miradi

Richard Nzagi: Mafinga ina Watoto wengi wa Kichina, Wachina wanaacha Watoto wengi wanapopita kwenye miradi

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa, Richard Nzagi anajibu swali kuwa “Endapo Mtanzania atapata ujauzito na raia wa kigeni, iwe ni mtalii au ameingia nchini kwa njia nyingine halali—halafu huyo mgeni akaondoka kabla mtoto hajazaliwa, je mtoto huyo anakuwa raia wa wapi?”

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa imeeleza kuwa mtoto anayezaliwa na mzazi mmoja Mtanzania na mwingine wa kigeni, anaruhusiwa kuwa na uraia wa nchi zote mbili hadi afikishe miaka 18.

Baada ya hapo, atalazimika kuchagua uraia wa upande mmoja, kwani sheria za Tanzania haziruhusu uraia pacha kwa watu wazima. Akikana uraia wa Tanzania, atatambulika kama mgeni anaporejea nchini.

Pia soma ~ Richard Nzagi: Muhamiaji Haramu akiingilia Uchaguzi Faini Sh Milioni 5 au kifungo cha Miaka mitatu au vyote
 
Kwahiyo mtoto wangu niliyezaa na binti wa kichina akaondoka na mtoto bado naweza kwenda kumchukua kusiwe na shida?
 
Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Iringa, Richard Nzagi anajibu swali kuwa “Endapo Mtanzania atapata ujauzito na raia wa kigeni, iwe ni mtalii au ameingia nchini kwa njia nyingine halali—halafu huyo mgeni akaondoka kabla mtoto hajazaliwa, je mtoto huyo anakuwa raia wa wapi?”

Kama ilivyokuwa Temeke wakati wa ujenzi wa uwanja wa Taifa
 
CCM na Tumbili, karibuni wataorodhesha hayo kama mafanikio ya mama. Watasema kuwa kabla ya mama wamama wa kitanzania waliokuwa wanapata mimba za wachina walikuwa chini ya 50, kwa sasa ni zaidi ya 1000, ongezeko la zaidi ya asilimia 1000. Watamaliza kwa kusema, mama apewe mitano tena ili atengeneze China ndani ya Tanzania.

watasema huo ni mpango madhubuti wa mama kuweza kubadilisha macho ya watanzania.
 
Huo ni mkakati maalum wa China kuhakikisha Wachina wanasambaa dunia nzima na kuitawala.
Unamaanisha mchina na uchina wao au rangi tu? Maana hao hawarudigi kulea wala kuangalia mtoto alie zaa na mweusi wako wengi mtaani hawana utafauti na mtu mweusi maana hajapewa miundombinu ya kuwa mchina
 
Wana haki ya kudinda,hawawabaki wanapewa kiroho safi tena kavu.
 
Back
Top Bottom