Ridhiwan Kikwete atumia siku yake ya kuzaliwa kusambaza upendo kwa wengine, afikisha miaka 45

Ridhiwan Kikwete atumia siku yake ya kuzaliwa kusambaza upendo kwa wengine, afikisha miaka 45

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Kila ifikapo Aprili 16 ni Kumbukizi ya Kuzaliwa ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete. Kwenye Siku yake hii ya Kuzaliwa mwaka huu 2024, Kikwete ameitumia kusambaza upendo kwa wananchi mbalimbali kwa kutoa vyakula mbalimbali.

Kikwete ametumia siku hii kumshukuru Mungu na Wazazi wake wawili Mhe. Jakaya Kikwete (Rais Mstaafu wa Awamu ya 4) na Mama yake Aziza Binti Saburi kwa kumleta kwenye uso wa dunia na kuwa baraka siku zote kwenye maisha yake. "Miaka Mingi iliyopita, Baraka za Allah ziliangaza Nyumba ya Baba Jakaya Kikwete na Mama Aziza Bint Saburi na nilianza safari katika Uso Wa Dunia.

Naendelea Kumshukuru Allah na kuwashukuru sana Wazazi wangu wawili kwa Mazazi Yangu. Siku zote mmekuwa ni Baraka kwangu. Nawashukuru sana zaidi ninaposherehekea Siku nyengine katika Maisha haya. Allahu Akbar." Ameandika Kikwete kwenye ukurasa wake wa Twitter

20240417_045710.jpg
FB_IMG_1713366431934.jpg
FB_IMG_1713366427865.jpg
FB_IMG_1713366404422.jpg
 
Kila ifikapo Aprili 16 ni Kumbukizi ya Kuzaliwa ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete. Kwenye Siku yake hii ya Kuzaliwa mwaka huu 2024...
Mungu akulinda KIONGOZI wetu
 
Back
Top Bottom