G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Wadaiwa sugu benk ya Twiga Bancorp iliyochukuliwa na BoT wanaendelea kuhenya na kuhenyeshwa mitaani, imefahamika. Watu hawalali, watu hawanywi na watu hawali!
Zipo taarifa nyeti kutoka vyanzo vya uhakika kabisa kuwa mjengo wa Ridhiwan ulioko maeneo ya Sinza Mori huenda ukakumbwa na kimbunga kama dhamana juu ya deni analodaiwa kijana huyo na benki hiyo iliyofilisika hivi karibuni.
Hata hivyo thamani halisi ya jengo hilo bado haijajulikana.

Awali Rais wangu John Pombe Magufuli aliposema kuwa kuna wanasiasa wanaongea sana ilhali ni wadaiwa sugu kwenye mabenki hakika sikuelewa. Ila kadri siku zinavyoenda, inazidi kudhihiri kuwa hakika maneno ya Rais wetu ni kweli kabisa.
Taarifa rasmi nilizonazo ni kwamba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Kawe Halima Mdee ni miongoni mwa watu waliochangia kufilisika kwa Benki hiyo. Taarifa hizo zinasema kuwa Freeman Mbowe peke yake anadaiwa mkopo wenye thamani ya shilingi bilioni saba hii ikijumuisha mkopo wenyewe na riba. Taarifa hizo zinasema kuwa kwa sasa Freeman Mbowe anahaha kuhakikisha anapata fedha za kulipa deni hilo ili kunusuru mali anazomiliki.
Taarifa hizo pia zinasema kuwa Halima Mdee alikopa Twiga Bancorp Juni 2011 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Ghorofa mbili ambalo hata hivyo halijafahamika liko wapi. Kwamba, Halima Mdee alikopa shilingi Bilioni 2.3 kwa ajili ya mradi huo deni ambalo mpaka sasa halijalipwa.
Niwasihi tu wale ndugu zangu wakopaji, dawa ya deni ni kulipa. Basi. Kuruka ruka haijawahi kuwa dawa ya kukwepa ulimbo.