Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nimeshangaa na kutatizwa sana na kauli ya Ridhiwani Kikwete akijibu swali la Dr. Christina Mnzava pale Bungeni, alipoulizwa kuhusu nyongeza za marekebisho ya kikokotoo kwa wastaafu, na hata kurekebishwa kwa kikokotoo kutoka fungu linalotolewa kwa sasa.
Hebu angalia mwenyewe hapa chini;
Source: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/kikotooo-chaibuka-tena-bungeni-4920616
Mimi nadhani serikali iache danadana kuhusu kikokotoo kwa kukubali kwamba fedha ya pension sio ya serikali, ni fedha ya mstaafu aliyoweka ili kumsaidia atakapostaafu. Kama kuna uamuzi wa kikokotoo uwe ni uamuzi wa wastaafu wenyewe, serikali haipaswi kuwapangia wapewe kiasi gani. Kuna nchi ambazo ukitaka pension yako ilipwe yote 100% utalipwa, sasa kwa nini isiwe Tanzania?
Serikali ya CCM iache mara moja ujanja wa kujua wastaafu hawana muda mrefu wa kuishi na kuwaibia hifadhi yao ya pension kwa ujanja huu. Huu ni uovu mbaya sana, wizi usio na aibu kwa wastaafu, serikali ya CCM ikiminya fedha zao kwa kutumaini wakifa zitarudi serikalini. Hili ni jambo baya kuliko uchawi wa kuua watu, serikai ya CCM kuishi kwa matumaini kwamba mtu akistaafu atakufa baada ya muda si mrefu ili fedha zake zirudi serikalini. Mbona wabunge mnawapa 100% ya pension zao? Kama serikali ni ya haki kwa nini wabunge wasilipwe kwa kikokotoo wanacholipwa wastaafu wengine?
Na ikumbukwe kwamba, fedha nyingi sana za pension serikali ndio mkopaji mkuu, wakichukua fedha nyingi hadi kuidhoofisha mifuko ya hifadhi. Kama mifuko ya hifadhi haiko imara mhalifu wa jambo hili ni serikali yenyewe, sio wastaafu. Kwa nini serikali ichukue mabilioni ya fedha za mifuko ya hifadhi halafu iamue kuwanyima wastaafu fedha zao kwa sababu imechukua asilimia kubwa ya fedha za mifuko ya hifadhi na kuzifanyia ufisadi? Uhalifu ifanye serikali ya CCM, adhabu wapewe wastaafu?
Kama serikali ya CCM inataka kulifanya suala la mifuko ya hifadhi kuwa la kisiasa kwamba ni suala la hisani ya Raisi Samia, basi tunawaomba mbadala wa CCM, Chadema, mtoe ahadi kwa wastaafu na wanaotarajia kustaafu, kwamba nyie mtalipa kikokotoo cha hadi silimia 80% au hata 100% kama wastaafu wakitaka, ili jambo hili liingie kwenye ilani za uchaguzi, CCM na kikokotoo chao cha 40% na Chadema na kikokotoo cha hadi 100% kwa mstaafu anaetaka. CCM wanasema hamna sera, basi waonyesheni mna sera ya kikokotoo cha hadi 100%!