Ridhiwani Kikwete: Maandalizi uzinduzi wa mwenge 2025 yamekamilika, kuzinduliwa Aprili 2, Pwan

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
397
Reaction score
445
Mbio za Mwenge 2025 zitahimiza Wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amesema maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 yamekamilika, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikihimiza Watanzania kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana Machi 26, 2025, Ridhiwani alieleza kuwa vijana sita kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wameandaliwa kwa ajili ya kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika jumla ya Halmashauri 195 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa siku 195.

“Kwa kipindi chote hicho, Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kuhamasisha amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa, pamoja na kuwahimiza wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi,” alisema Ridhiwani.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.” Waziri alisisitiza kuwa falsafa ya Mwenge wa Uhuru imekuwa kiini cha historia muhimu ya taifa, ikiwemo Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka huo huo, na Azimio la Arusha la 1967.

Uzinduzi wa mbio hizo utafanyika Aprili 2, 2025, katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mkoani Pwani, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakar Kunenge, amesema maandalizi yako katika hatua za mwisho na yatakamilika ifikapo Machi 29, 2025.

Mwenge wa Uhuru, ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961, unaendelea kuwa alama ya mshikamano na maendeleo ya taifa.

FB_IMG_1743083993938.jpg
 
Kwanini wasizindue hiyo miradi bila mwenge, kwenye hiyo mikesha ina mambo mengi ya hovyo na kufanya ongezeko kubwa la maambukizi ya magonjwa ya zinaa..!!

Huwa unahamasisha ngono zembe tu.!
 
Haya ndiyo mambo tunayoyataka wananchi!

Lengo kuu la mwenge wetu ni kuhimiza amani ,umoja na mshikamano...

Kinyume na hayo hakuna maendeleo!

#Tanzania yenye amani milele dumu aaamin!
 
Mbio za Mwenge 2025 zitahimiza Wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amesema maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 yamekamilika, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikihimiza Watanzania kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana Machi 26, 2025, Ridhiwani alieleza kuwa vijana sita kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wameandaliwa kwa ajili ya kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika jumla ya Halmashauri 195 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa siku 195.

“Kwa kipindi chote hicho, Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kuhamasisha amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa, pamoja na kuwahimiza wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi,” alisema Ridhiwani.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.” Waziri alisisitiza kuwa falsafa ya Mwenge wa Uhuru imekuwa kiini cha historia muhimu ya taifa, ikiwemo Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka huo huo, na Azimio la Arusha la 1967.

Uzinduzi wa mbio hizo utafanyika Aprili 2, 2025, katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mkoani Pwani, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakar Kunenge, amesema maandalizi yako katika hatua za mwisho na yatakamilika ifikapo Machi 29, 2025.

Mwenge wa Uhuru, ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961, unaendelea kuwa alama ya mshikamano na maendeleo ya taifa.
Wangezifuta tuu maana humo hufanyika ngono zembe, huko vijijini wadogo zetu hunywesha bia na kuku kisha kutoa mapenzi ni usambasaji wa virus mwanzo mwisho
 
Kwanini wasizindue hiyo miradi bila mwenge, kwenye hiyo mikesha ina mambo mengi ya hovyo na kufanya ongezeko kubwa la maambukizi ya magonjwa ya zinaa..!!

Huwa unahamasisha ngono zembe tu.!
Ni sawa na kutaka kusiweko vinavyochangamsha(muziki,ngoma,maigizo) wahudhuriaji wa uzinduzi wa matamasha ya aina tofauti....

Uwepo wa wale askari shupavu,skauti,vijana wa hamasa na uzalendo wao maeneo uliopo Mwenge nako ni KICHANGAMSHI na kiburudisho....
 
Hakuna cha vichangamshi wala nini, vinachochea ngono na idadi ya maambukizi kuzidi..!!
 
Kwanini wasizindue hiyo miradi bila mwenge, kwenye hiyo mikesha ina mambo mengi ya hovyo na kufanya ongezeko kubwa la maambukizi ya magonjwa ya zinaa..!!

Huwa unahamasisha ngono zembe tu.!
Ngono inafanywa sehemu yyte ht huko kwenye mwenge ni uamuzi binafsi
 
Ni sawa na kutaka kusiweko vinavyochangamsha(muziki,ngoma,maigizo) wahudhuriaji wa uzinduzi wa matamasha ya aina tofauti....

Hakuna cha vichangamshi wala nini, vinachochea ngono na idadi ya maambukizi kuzidi..!!
Kumbe ngono zembe nchini hufanyika wakati wa mbio za Mwenge tu. .

Sawa mkuu!
 
Mbio za Mwenge 2025 zitahimiza Wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amesema maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 yamekamilika, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikihimiza Watanzania kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana Machi 26, 2025, Ridhiwani alieleza kuwa vijana sita kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wameandaliwa kwa ajili ya kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika jumla ya Halmashauri 195 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa siku 195.

“Kwa kipindi chote hicho, Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kuhamasisha amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa, pamoja na kuwahimiza wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi,” alisema Ridhiwani.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.” Waziri alisisitiza kuwa falsafa ya Mwenge wa Uhuru imekuwa kiini cha historia muhimu ya taifa, ikiwemo Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka huo huo, na Azimio la Arusha la 1967.

Uzinduzi wa mbio hizo utafanyika Aprili 2, 2025, katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mkoani Pwani, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakar Kunenge, amesema maandalizi yako katika hatua za mwisho na yatakamilika ifikapo Machi 29, 2025.

Mwenge wa Uhuru, ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961, unaendelea kuwa alama ya mshikamano na maendeleo ya taifa.
Kiongozi wa mbio za mwenge 2024, huwezi kuamini ,ameteuliwa kuwa DC, ila aliko miradi anayosimamia ni wizi mtupu
 
Back
Top Bottom