Ridhiwani Kikwete: Maandalizi uzinduzi wa mwenge 2025 yamekamilika, kuzinduliwa Aprili 2, Pwan

Ridhiwani Kikwete: Maandalizi uzinduzi wa mwenge 2025 yamekamilika, kuzinduliwa Aprili 2, Pwan

Mwenge upelekwe kwenye makumbusho ya taifa. Hakuna Cha maana kinacholetwa na huu mwenge.
 
Haya ndiyo mambo tunayoyataka wananchi!

Lengo kuu la mwenge wetu ni kuhimiza amani ,umoja na mshikamano...

Kinyume na hayo hakuna maendeleo!

#Tanzania yenye amani milele dumu aaamin!
Mwenge ni madhabahu ya miungu iliyo kinyume na Mungu wa mbinguni aliye hai. Ni nichukizo kubwa sana mbele ya Mungu na ndio maana pia laana imesimama juu ya taifa na taifa haiendelei licha ya utajiri Mungu aliotupatia.
 
Mwenge ni madhabahu ya miungu iliyo kinyume na Mungu wa mbinguni aliye hai. Ni nichukizo kubwa sana mbele ya Mungu na ndio maana pia laana imesimama juu ya taifa na taifa haiendelei licha ya utajiri Mungu aliotupatia.
...karibia utaokota Makopo na kulala majalalani....
 
Mbio za Mwenge 2025 zitahimiza Wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amesema maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 yamekamilika, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikihimiza Watanzania kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana Machi 26, 2025, Ridhiwani alieleza kuwa vijana sita kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wameandaliwa kwa ajili ya kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika jumla ya Halmashauri 195 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa siku 195.

“Kwa kipindi chote hicho, Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kuhamasisha amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa, pamoja na kuwahimiza wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi,” alisema Ridhiwani.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni: “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.” Waziri alisisitiza kuwa falsafa ya Mwenge wa Uhuru imekuwa kiini cha historia muhimu ya taifa, ikiwemo Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka huo huo, na Azimio la Arusha la 1967.

Uzinduzi wa mbio hizo utafanyika Aprili 2, 2025, katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mkoani Pwani, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakar Kunenge, amesema maandalizi yako katika hatua za mwisho na yatakamilika ifikapo Machi 29, 2025.

Mwenge wa Uhuru, ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961, unaendelea kuwa alama ya mshikamano na maendeleo ya taifa.

View attachment 3285049
Mbio za mwenge zifutwe. Nguvu, pesa, akili zitumike kwa vitu vya maana zinazounganisha Taifa bila uchama, uchawa, undugu katika upigaji wa mali za umma.
 
Hizo mbio ndio zinachochea zaidi usijifanye hujui..
Auntie nimeshiriki mbio nyingi za Mwenge.....kati ya mambo ya hovyo yanayofanyika huwa ni HIYARI za watu.....

Sasa utamzuia mtu mzima kufanya alitakalo na linalohusu mwili wake ?!!
 
Auntie nimeshiriki mbio nyingi za Mwenge.....kati ya mambo ya hovyo yanayofanyika huwa ni HIYARI za watu.....

Sasa utamzuia mtu mzima kufanya alitakalo na linalohusu mwili wake ?!!
Nyie mnawakusanya watu mnaweekea miziki na pombe mnategemea nini kitatokea??
 
Kwanini wasizindue hiyo miradi bila mwenge, kwenye hiyo mikesha ina mambo mengi ya hovyo na kufanya ongezeko kubwa la maambukizi ya magonjwa ya zinaa..!!

Huwa unahamasisha ngono zembe tu.!
Mwenge ndio unakulazimisha kushiriki ngono zembe?
 
Back
Top Bottom