Ridhiwani Kikwete yuko live, anaongea kama Jakaya Kikwete. Like father like son, atatufaa sana in future baada ya zamu yetu!

Ridhiwani Kikwete yuko live, anaongea kama Jakaya Kikwete. Like father like son, atatufaa sana in future baada ya zamu yetu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,

Kwanza watch TBC Live Mubashara
View: https://www.youtube.com/watch?v=wMOElr9lFGI

Japo enzi za Rais Jakaya Mrisho Kikwete, sisi humu JF, tulimpiga spana za kutosha zikiwemo spana zangu, za kumkosoa JK, Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

Pia JK, alikuwa na mazuri yake pia tulimpongeza Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour" haya mazuri ya Kikwete pia Ridhiwani Kikwete anayo!, ni mtu rahimu sana, cool, humble na down to earth!, japo ni mtoto wa rais, sio mtu wa kujimwambafy kama nanii!. Mungu ambariki sana!.

Siku Jakaya anaaga alisema tutamkumbuka, kiukweli aliyefuatia, tulimkumbuka JK! Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma na kuna watu wa JK walishughulikiwa Hii Tumbua Tumbua ya Rais Magufuli, Hivi Kikwete Anajisikiaje?!. Anajisikia Sifa Au Anajuta?!. pia niliwahi kuuliza, Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete?!

Hakuna Tanzania nzuri kwa uhuru wa vyombo vya habari uhuru wa kujieleza kama Tanzania ya JK!, ni kipindi hiki PPR ndio ilizaliwa, na kuneemeka!. Media tulikuwa huru hadi kumpiga biti rais wa JMT, enzi za JK Ushauri wa bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya October 25!, just imagine media tulivyokuwa huru!, leo lile tukio la October 29, watu 518 wamethibitishwa kufa, kuna media yoyote inaweza kujitokeza hata kuuliza tuu, aliyetoa amri ile ni nani?, ukiondoa JF kuulizia hoja kaa hii PostGE2025 - Voices from Within: Mauaji ya wananchi Dar, tusiwalaumu Polisi. Je Amri ya kuua Ilitoka kwa muuaji huyu? kuna media yoyote imeweza kukohoa na kufanya IJ yoyote ya kilichotokea au hata kumwambia Rais Samia ili angalau kuonyesha ameguswa, awaombe radhi Watanzania kwa kilichotokea, awafariji waliofiwa kwa mauaji ya makosa kama wale watoto wadogo au wale wa kibanda umiza kule Mwanza?, enzi za Kikwete, hili lingewezekana, tungemshuhudia JK akitembelea majeruhi Muhimbili, JK angewaomba wasaidizi wake watatu, CDF, IGP na DGIS, wakae pembeni kupisha uchunguzi, hivyo ikitokea akaja Ridhiwani, enzi za uhuru huu wa habari na uhuru wa kujieleza, zitarudi kama enzi za Jakaya, na tukio kama la October, lisingeweza kutokea!, na labda hata PPR chini Pasco Jnr pia itafufuka!.

Sasa leo nIkImuangalia Ridhiwani Kikwete live mubashara, kupitia TBC Ridhiwani Kikwete , nimegundua Jakaya Kikwete hapa alijizaa!, Jamaa ni copy right like father like son!, wanafanana mpaka sauti na jinsi anavyoongea, ni kama Jakaya, na vile vineno vya JK hadi raha kumsikiliza!, kitu kikubwa kumhusu Ridhiwani, ana karama ya uongozi, ana kipawa cha uongozi na ana uwezo wa uongozi kama baba yake!, ama kweli mwana wa nyoka ni nyoka!.

Kufuatia Abedi Karume Amani Karume, Ali Hassan Mwinyi, Dr Hussein Mwinyi, then in future huyu Ridhiwani Kikwete atatufaa sana latika lile jambo letu baada ya kukamilika, kwa zamu yetu kwenye lile jambo letu, ili pia tuje kumpata Jakaya Kikwete Ridhiwani Kikwete!
1780337544183.png

Hii sio marayangu ya kwanza, kuwanenea watu huwa, wawe na wakawa,
Japo mimi Pasco Mayalla nimeisha mfanyia endorsement yangu huyu kijana kwa kushauri awamu ijayo apelekwe MFA kumpatia an international exposure, mimi ni nobody, na ninachofanya hapa ni ku proposes tuu, anayeamua nani awe, sio mimi, sio wewe wala sio yeye, ni YEYE!, kama huyu yeye ameandikiwa na YEYE, kuwa siku moja atakuwa, then no one can do anything kuzuia asiwe!.

Mungu Mbariki Ridhiwani Kikwete

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
UPDATE
Wanabodi, ukisikia mabandiko yana impact, ndio bandiko kama hili, kuna mdada wa JF, inaonekana alikuwa anamzimikia sana huyu dogo, kafa kaoza, alitamani dogo amtokee, ili awe nanii wake, kwa vile jamaa katulia sio ile type ya pita pita, hivyo huyu binti sasa amemjengea chuki kijana wa watu, ili kuficha chuki zake, akaamua kunianzishia mimi thread Paschal Mayala acha kutumika na Ridhiwan Kikwete maji yamekorogeka
Kwa taarifa za uhakika ni kwamba mwandishi nguli wa habari Paschal Mayala amenasa kwenye kundi la ccm mtandao ambalo kazi yao ni moja tu kubagaza na kubananga rasilimali za Watanzania.
Mkuu Binti Mrembo Etwe, Etwege , kwa vile umesema una taarifa za uhakika, nakuomba weka na uthibitisho!, niliwahi kushauri humu, Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho
naomba usichafue jina langu na jina la mtoto wa watu. Nitakushukuri pia ukionyesha jinsi huyu dogo kubagaza na kubananga rasilimali za Watanzania.
Paschal Mayala amepewa kazi maalum ya kumnadi na kumsafishia njia Ridhiwan Kikwete ili apate taswira nzuri mbele ya macho ya watanzania ili kwenye uchaguzi mkuu wa 2030 achaguliwe kuwa Rais wa awamu ya 7 ya jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo kufuata nyayo za baba yake Jakaya Kikwete.
Hii si kweli, rais wetu wa 2030 tayari yupo anasubiri. tuu kukamilisha taratibu, na bahati nzuri mimi namjua na sio huyu dogo!, Trends Reading: Japo Rais wa 2030 Namjua, Simtaji ili Kumlinda!. Be The First to Know Good News Kawe-2030, MB.ni Mwanamke!, Kawe Itapaa kwa Maendeleo!
Kwa sisi wapenda maendeleo na wazalendo wa nchi yetu Tanzania tunamuonya Paschal Mayala kuwa Ridhiwan Kikwete hana hadhi wala maadili ya kuwa Rais wa nchi yetu,
Eleza ni kivipi Ridhiwan Kikwete hana hadhi wala maadili ya kuwa Rais wa nchi yetu?
madudu na machafu aliyoyafanya baba yake yanatosha kabisa kumwondolea sifa ya kuchaguliwa kwani hataenda kufanya kazi za Watanzania badala yake ataenda kulinda biashara na masilahi ya baba yake.
Unaweza kututajia hayo madudu na machafu aliyoyafanya baba yake?. Je unamhukumu mtoto kwa makosa ya Baba yake?.

We Etwe, kama unampenda dogo umekosa sasa unaugulia wivu, na ili kujifariji, ndio unaona bora umchafulie na kunichafulia na mimi?.

Kwa mabandiko yangu humu jf na makala zangu, mimi naweza kutumwa na mtu yeyote?.
Mimi huwa situmwi na yeyote bali najituma tuu, na ukiona kuna kitu nimekiandika, hicho kitu ni cha kweli!.

Na kumhusu huyu dogo, nimesema nIkImuangalia Ridhiwani Kikwete, nimegundua Jakaya Kikwete hapa alijizaa!, Jamaa ni copy right like father like son!, wanafanana mpaka sauti na jinsi anavyoongea, ni kama Jakaya, na vile vineno vya JK hadi raha kumsikiliza!, kitu kikubwa kumhusu Ridhiwani, ana karama ya uongozi, ana kipawa cha uongozi na ana uwezo wa uongozi kama baba yake!, ama kweli mwana wa nyoka ni nyoka!.

Japo mimi Pasco Mayalla nimeisha mfanyia endorsement yangu huyu kijana kwa kushauri awamu ijayo apelekwe MFA kumpatia an international exposure, mimi ni nobody, na ninachofanya hapa ni ku proposes tuu, anayeamua nani awe, sio mimi, sio wewe wala sio yeye, ni YEYE!, kama huyu yeye ameandikiwa na YEYE, kuwa siku moja atakuwa, then no one can do anything kuzuia asiwe!.

Mzee Pasco.
 
Wanabodi,

Watch TBC Mubashara, Ridhiwani Kikwete Yuko Live, Anaongea Kama Jakaya Kikwete!, Like Father Like Son, Atatufaa Sana In Future Baada ya Zamu Yetu!.

P
Ridhiwani Kikwete anafaa, sasa hivi amekomaa, kuna mambo mengi sana amejifunza nahisi hata akija pewa nafasi ata fix ambapo baba yake alikosea na hao wengine.. Naungana na wewe 100%
 
Kwani nchi ya watu zaidi ya milioni 60 ni lazima itawaliwe na watu wale wale miaka nenda? Mbona tunapenda sana kuyatukuza mambo yasiyo na mashiko kwa maendeleo ya nchi yetu!!

Shemeji kuna wakati unazingua sana.
 
Kwani nchi ya watu zaidi ya milioni 60 ni lazima itawaliwe na watu wale wale miaka nenda? Mbona tunapenda sana kuyatukuza mambo yasiyo na mashiko kwa maendeleo ya nchi yetu!!

Shemeji kuna wakati unazingua sana.
Watu walewale akina nani?..hivi kati ya Hussein mwinyi na makalla nani kiongozi mzuri?..uache kumtumia mwinyi kama kiongozi kisa baba yake alikua kiongozi umuweke lema kuwa kiongozi kwa kuwa hakuna mwana familia alikua kiongozi?
 
Back
Top Bottom