Ridhiwani: Mapambano na Madawa ni kama yameanza

Ridhiwani: Mapambano na Madawa ni kama yameanza

Sasa nimeanza kuamini kuna Mjinga moja alikurupuka na kuchafuwa Majina ya watu....hii inaonyesha dhahiri Mjinga huyo hakuwa na nia ya dhati ya kupambana na madawa ya kulevya
Kazi bado ni kubwa
 
Sasa unashangaa nini kama sio uchizi tuu? Hivi si ni nyie mliopinga Makonda kuwataja? Sasa nikuulize unashangaa nini? Kama una ushahidi na wewe peleka polisi....
Mlivyo sikia kuna Mapapa sijui mlidhani ni Papa Francis au Benedicto? Wametajwa Mapapa mmeanza kulia lia na mnataka wengine watajwe wakati wakitajwa mnapiga kelele.
Pole sana kijana kwa kupata shida kutetea
 
Taucheni na upambe wala ushabiki hapa...SASA HUYO MTUMBUA MAJIPU NDIO ILIKUA WAJIBU WAKE SASA MBONA AMEKULA GANZI???AU HIO NI UPELE???
HAMSHANGAI KUA WIZARA YA MAMBO YA NDANI IMEKAA KIMYA????(wizara nyeti nandohusika kwa usalama na amani)HALAF NYIE MNAMJADILI MTU..Ohhh mbona flani Hivi mbona flani hajakamatwa...ITS NONSENSE TUSIPOTEZEANE MDA KWA KUCHEZEWA AKILI ZETU....HUO NI UJANJA WA MKASI KUKATA MBELE HUKU VIDOLE............
 
Kumpongeza kwake ni kujipendekeza ili asitajwe maana nayeye kwenye msafala huo yumo, ni suala la muda kila kitu kitabaki hadharani
Issue yote hii ya madawa aliyekuwa anatetewa ni huyu Ridhwani na team yake ya GSM ambayo Makonda yumo ndani hapohapo ikaingizwa kuchafuana watu wa Upinzani na waliosupport upinzani.

Hakuna movie iliyoshinda ktk hizi sanaa zao.
Tupo hapa wataumbuana wenyewe
 
Issue yote hii ya madawa aliyekuwa anatetewa ni huyu Ridhwani na team yake ya GSM ambayo Makonda yumo ndani hapohapo ikaingizwa kuchafuana watu wa Upinzani na waliosupport upinzani.

Hakuna movie iliyoshinda ktk hizi sanaa zao.
Tupo hapa wataumbuana wenyewe
008c68ba2de9fd69f648368cda4c042d.jpg

Huyu jamaa naona anazidi kutusanifu watanzania
 
2 (1).JPG



Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete, amefunguka kuhusu sakata la dawa za kulevya na kuipongeza serikali hususani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha vita hiyo na kutaka wahusika wachukuliwe hatua.

Kikwete amefunguka hayo leo katika kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, kinachoruka kila siku saa 11:00 alfajiri hadi saa 3:00 asubuhi.

Ametumia nafasi hiyo kuishauri serikali kuifikisha mwisho vita hiyo, ili kulimaliza kabisa tatizo hilo kwa kuwa limepoteza vijana wengi wenye uwezo mkubwa na mchango katika taifa, huku akitolea mfano uwezo wa msanii wa Bongo Fleva, Langa ambaye kwa sasa ni marehemu ikidaiwa kuwa alipoteza maisha kutokana na dawa hizo, pamoja na shida alizokuwa akizipata msanii Ray C, za kutafuta dawa hizo hata usiku wa manane.

Ameitaka mamlaka mpya wa dawa za kulevya kuwachunguza watu 97 ambao majina yake yamekabidhiwa hivi karibuni na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na yeyote atakayethibitika kuhusika, achukuliwe hatua, huku akionesha imani kubwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Rogers William Sianga.

Chanzo Muungwana online
Alichosema Kikwete kuhusu sakata la dawa za kulevya - MUUNGWANA BLOG
 
Kweli watanzania ni wanafiki sana
Ni kweli mkuu, mfano halisi watu walililia Makonda awataje mapapa wa dawa za kulevya badala ya kuhangaika na dagaa, alipowataja wakageuka tena na kusema approach ya kutaja majina siyo nzuri na wengine wamekimbilia Mahakamani.
 
Hahahh anapoozea au anafunika?! Hii nchi ina vituko! Who will be next tupo masikio yanasubiri kusikia
 
Katika kikao cha Bunge, walijitokeza wabunge vinara wapinga Maendeleo wakamshambulia sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paulo Makonda kwa kuwataja hadharani watu maarufu wanaoshukiwa kujihusisha na baiashara haramu ya madawa ya kulevya.

Wapinzani wakiongozwa na Mhe John Heche, Mbunge wa Tarime vijijini walikuwa na agenda ya kumshambulia RC Makonda wakidai amewatukana Wabunge kwa kusema wanalala kazini. Mhe Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda mjini (Chadema) na Mhe Zitto Zuberi Kabwe mbunge wa Kigoma kaskazini na Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo waliongoza shutuma hizo. Kwa upande wa CCM waliungwa mkono na Mbunge wa Geita mjini, Joseph Kasheku Msukuma aliyetangaza vita ya wazi wazi dhidi ya RC Paul Makonda.


Mawaziri walipigwa Butwaa na kama ilivyokuwa kwa Wabunge wengi wa CCM, walinyamaza kimya ulipofika wakati wa kupiga kura kama Azimio dhidi ya Makonda lipitishwe au hapana. Azimio kwa hiyo likawa limepitishwa bila kupingwa na yeyote.

Lakini kitu cha kuangalia ni wabunge gani wa CCM walisimama kuunga mkono hoja hii ya wapinzani? Walikuwa wachache na kati ya wachache hao wa kwanza kuamka alikuwa Mhe Rizwan Kikwete, Mbunge wa Chalinze, aliyeonekana kuwa na furaha sana wakati Makonda akishambuliwa.


Rais Magufuli amesema bora Mchawi kuliko Mnafiki. Imeshangaza sana kuona sasa katika mitandao ya kijamii, baada ya Rais Magufuli kusimama kidete kumtetea Makonda na kusema vita inaendelea, anajitokeza Rizwan Kikwete huyohuyo akidai anaunga mkono Makonda katika vita yake jasiri ya kutokomeza madawa ya kulevya?


Unafiki wote huu wa nini? Kama unajua huungi mkono kitu si bora ukanyamaza. Hivi watu wanafikiri Tanzania ya Magufuli ni sawasawa na Tanzania ya Jakaya Kikwete?

NOTE:Hapa naongelea tu unafiki wa mbunge
 
Back
Top Bottom