Katika kikao cha Bunge, walijitokeza wabunge vinara wapinga Maendeleo wakamshambulia sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paulo Makonda kwa kuwataja hadharani watu maarufu wanaoshukiwa kujihusisha na baiashara haramu ya madawa ya kulevya.
Wapinzani wakiongozwa na Mhe John Heche, Mbunge wa Tarime vijijini walikuwa na agenda ya kumshambulia RC Makonda wakidai amewatukana Wabunge kwa kusema wanalala kazini. Mhe Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda mjini (Chadema) na Mhe Zitto Zuberi Kabwe mbunge wa Kigoma kaskazini na Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo waliongoza shutuma hizo. Kwa upande wa CCM waliungwa mkono na Mbunge wa Geita mjini, Joseph Kasheku Msukuma aliyetangaza vita ya wazi wazi dhidi ya RC Paul Makonda.
Mawaziri walipigwa Butwaa na kama ilivyokuwa kwa Wabunge wengi wa CCM, walinyamaza kimya ulipofika wakati wa kupiga kura kama Azimio dhidi ya Makonda lipitishwe au hapana. Azimio kwa hiyo likawa limepitishwa bila kupingwa na yeyote.
Lakini kitu cha kuangalia ni wabunge gani wa CCM walisimama kuunga mkono hoja hii ya wapinzani? Walikuwa wachache na kati ya wachache hao wa kwanza kuamka alikuwa Mhe Rizwan Kikwete, Mbunge wa Chalinze, aliyeonekana kuwa na furaha sana wakati Makonda akishambuliwa.
Rais Magufuli amesema bora Mchawi kuliko Mnafiki. Imeshangaza sana kuona sasa katika mitandao ya kijamii, baada ya Rais Magufuli kusimama kidete kumtetea Makonda na kusema vita inaendelea, anajitokeza Rizwan Kikwete huyohuyo akidai anaunga mkono Makonda katika vita yake jasiri ya kutokomeza madawa ya kulevya?
Unafiki wote huu wa nini? Kama unajua huungi mkono kitu si bora ukanyamaza. Hivi watu wanafikiri Tanzania ya Magufuli ni sawasawa na Tanzania ya Jakaya Kikwete?
NOTE:Hapa naongelea tu unafiki wa mbunge