Ridhiwani: Tumeishi na RC Makonda vizuri ila kutajwa kwenye madawa, kama familia tunamwachia Mungu

Ridhiwani: Tumeishi na RC Makonda vizuri ila kutajwa kwenye madawa, kama familia tunamwachia Mungu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Dar es Salaam. Baada ya kuitwa kuhojiwa kuhusu tuhuma za kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema taarifa hizo zilitingisha familia yake, lakini baba yake Jakaya Kikwete alimtia moyo.

Tofauti na watuhumiwa wengine waliohojiwa kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya, Ridhiwani hakutangazwa hadharani badala yake aliitwa kimyakimya na kuhojiwa na baadaye kuruhusiwa aendelee na shughuli zake baada ya kuonekana hana hatia.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi Digital yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Ridhiwani amesema JK hakushtushwa na badala yake alimpa nguvu ya kwenda kueleza ukweli .

“Pengine aliamua kuficha hofu yake ili kunitia nguvu,” amesema Ridhiwani.

Pia soma:
 
Kwenye orodha ya Makonda Ridhiwani hakuwepo. Sasa hapo Makonda anaingiaje?
Kwa sababu, umetumia busara kuuliza nkujibu, Ridhiwani jina lke lilikuepo kwny ile orodha ya mwsho aliyojimasibu mpk watoto wa viongoz wamo ila majina hayakusomwa na orodha ya watuhumiwa ilikabidhiwa kwa commissioner wa kupambana na drigs.
 
Mbona aliwahi kusema roho yake ilisuuzika kwa kuhojiwa, maana hiyo ilikata mzizi wa fitina wa tuhuma? Kwa maneno mengine alihitaji sana uwepo wa Tume ya kuwaambia ukweli watanzania juu yake na tuhuma zisizokuwa na kichwa wala miguu! Sasa anamlaumu vipi Makonda?
 
Back
Top Bottom