tucker carlson
Senior Member
- Oct 5, 2025
- 182
- 759
Naona Rio Ferdinand amejibu mapigo wakuu baada ya wabongo kumpelekea sana 'moto' huko Instagram
Akizungumza leo jijini Dar amesema kuwa yuko Tanzania kwa ajili ya kazi ya kusaka vipaji na kwamba ana uhuru wa kufanya maamuzi yake bila kupangiwa na mtu yeyote.
"Sababu yangu pekee, sababu yangu binafsi, na msimamo wangu kabla sijaja hapa ulikuwa ni kitu ambacho siku zote ni cha kweli kwangu: na hiyo ilikuwa ni kuja kusaidia kuwatia moyo vijana na kizazi kipya kupitia mchezo ninaoupenda ambao ni mpira wa miguu. Na hilo halitabadilika kamwe.
Kwa hiyo tena, napenda kusisitiza pia; mimi si mwanasiasa. Siko hapa kuzungumzia siasa. Sijawahi kufanya hivyo katika nchi yangu mwenyewe, na nisingefanya hivyo popote pengine. Lakini lazima nisisitize tena, vijana wanastahili kutiwa moyo. Nilicheza kwenye ligi, nilicheza katika enzi ambayo wachezaji wa Kiafrika walikuwa sehemu kubwa ya mfumo huo"