Ripoti juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini: hakuna gazeti hata moja lililoandika habari hiyo!

Ripoti juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini: hakuna gazeti hata moja lililoandika habari hiyo!

Wanabar Makada? ndio maana kwa sasa hivi Idhaa za Kiswahili za Kinataifa kama BBC, VOA, DWD na wengineo wanaendelea kuchukua Wakenya pekee.
Sahihi.Wanahabari wa Tanzania wana maono na mipango hafifu sana kwa sababu ya ukada,kisingizio cha uzalendo feki,uoga na kuogopa vitisho,kupenda bahasha,weledi hafifu,kutofuata maadili.ndoto za kupata utajiri na ujinga sugu.Wanalemaza tasnia yao (crippling the industry)kwa mikono na uwezo mdogo wa akili zao.Nini kimewashinda hadi washindwe kukopi na kupeisti taarifa walizoandaliwa na wenye uwezo na akili chanya?
 
Tatizo lakwaza je hiyo report inamnufaisha nani? Kama ni mwananchi wa kawaida vyombo vya habari havinufaiki sana na Wananchi wa kawaida kwenye kuuza habari zao kuliko matangazo wanayo pewa na wizara mbalimbali pamoja na serikali kwa ujumla. Kwa mfano gazeti la uhuru ukienda ofisi zote za serikali utalikuta nchi nzima sasa ikiandika habari zinazo husu ukiukwaji wa haki za binadamu na mara nyingi habari hizi zinaegemea upande wa serikali nani atakuwa mteja wake mkubwa. Ukitaka kujua kuwa usipo pata matangazo uwezi kuendesha vjombo cha habari, Chukulia Tanzania Daima la Mbowe lipo wapi
Kwahiyo njaa ndiyo inafanya habari ngumu wasiziandike.
 
Jana vyombo vya habari vya kimataifa vilitangaza taarifa iliyotolewa na taasisi ya kimataifa ya human right watch juu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea nchni. Nimepita magazeti karibu yote habari hiyo haikuandikwa popote. Paskali mara nyingi huwa unajitokeza kutetea wanahabari wenzio tunaposema hakuna professionalism na uhuru wa habari nchini. Tunaomba ujitokeze tena utufafanulie hili.
Tuna Nchi ya kipumbavu mno wapendwa
 
Sahihi kabisa mdau mkubwa wa biashara za habari ni serikali inabajeti kabiasa.
Mdau mkubwa wa biashara za habari mwenye bajeti kubwa ya habari ambaye umiliki na uendeshaji wa sectors muhimu za uzalishaji mali zimemshinda hadi akaamua kuziuza au kukodisha kwa wenye akili timamu?
 
Sasa hapo paskali hapo anahusika vipi mkuu ikiwa ripoti haikutolewa na vyombo vyovyote basi ujue ndio hivyo wenye mchi wameamua hivyo..
Maana yake haviko huru
 
Unataka watoe habari inayoelezea ukiukwaji wa haki za binadamu wakati mama mwenye nyumba ameshajitanabaisha kwa wanainchi wake kwamba serikali yake ni serikali inayojali watu na Haina uonevu Wala ukandamizaji wa aina yeyote...

Unataka Wana habari wamchonganishe mama na wanae?? Wewe vipi
 
Back
Top Bottom