Ripoti Kamili ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

View attachment 1067472
View attachment 1067459

Wakuu,

Mnaweza kuipakua ripoti kamili hapa:

Lakini, endapo tovuti itakuwa na shida basi naambatanisha hapa mafaili yote

NB: Ripoti imesainiwa na Prof. Assad

Kwa ufupi...

BUNGENI Ofisi ya CAG imetisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma. Inatarajiwa kuwa CAG, Prof. Mussa Assad, atawaeleza waandishi wa habari kuhusu mukhtasari wa kile kilichomo kwenye ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka 2017/18.

Miaka iliyopita, CAG alikuwa anatoa mukhtasari huo kwa waandishi wa habari bungeni mara tu baada ya ripoti yake kuwasilishwa kwenye chombo hicho.
Bunge limeshaazimia kutofanya kazi na Prof. Assad, hivyo ni wazi kwamba hawezi kuzungumza na waandishi wa habari bungeni.

=> CAG assad: Tumezoa kufanya mkutano huu mara tu baada ya ripoti hii kuwasilishwa.

=> CAG assad: Mimi nimetazama kwa TV ripoti imewasilishwa bungeni na 'order paper' (karatasi yenye orodha ya shughuli za kikao cha Bunge) ninayo hapa inaonyesha ripoti imekabidhiwa bungeni leo asubuhi na nimetazama ikiwasilishwa.

=> Prof Assad: Mwaka huu tumetoa ripoti yetu kwa CD ili kuepuka gharama nyingi za uchapishaji.

=> Prof Assad: Mapendekezo yetu tuliyotoa katika ripoti iliyopita yalikuwa 350 lakini ni 80 tu yaliyotekelezwa kikamilifu.

=> Prof Assad: Serikali kuu kulikuwa na mapendekezo 91, mawili tu ndiyo yametekelezwa kikamilifu.

=> Prof Assad: Halmashauri za Kigoma Ujiji na Nyng'wale zimepata hati zisizoridhisha na hati mbaya katika mwaka wa fedha 2017/18.

=> CAG Assad: Tumebaini kuwapo kwa malipo hewa ya mabilioni ya shilingi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

=> Prof Assad: Pia tumebaini Wilaya ya Hanang' haikuwasilisha vitabu vya fedha na kuna upotevu wa mapato ya Sh. bilioni 1.4 na walilipa fedha kwa wakandarasi kwa kazi ya dharura pasipo kuwapo kwa kazi ya dharura.

=> Prof Assad: NEC ilinunua BVR 8,000 lakini mashine 5,000 kati ya hizo zilikuwa haziendani na mfumo uliotakiwa hivyo kuisababisha serikali hasara ya mamilioni ya shilingi.

=> Prof Assad: Kuna mafunzo kwa maofisa wa NEC hayakufanyika licha ya mzabuni kulipwa.

=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lililipa Sh. bilioni 16 kwa ajili ya ununuzi wa sare za polisi bila kuwapo kwa ushahidi wa ununuzi.

=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lilipa Sh. milioni 600 kwa ajili ya mafunzo ambayo hayakufanyika.

=> CAG Assad: Tumebaini Chadema ilinunua gari jipya aina ya Nisan Patrol kwa Sh milioni 147.5 lakini lililisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya Wadhamini.

=> CAG Assad: Tumebaini CCM haijawasilisha NSSF makato ya Sh. bilioni 3.74 ya wanachama wake.

=> CAG Assad: Majengo ya ofisi za CUF yamesajiliwa kwa majina ya watu badala ya Bodi ya Wadhamini.

=> CAG Assad: Kuna miradi 27 serikali za mitaa imekamilika lakini haitumiki licha ya kugharimu mabilioni ya shilingi.

=> Prof Assad: Tumebaini mashirika 14 yana matatizo makubwa ya kifedha na yanaendelea kutengeneza madeni makubwa.

=> CAG Assad: Tumebaini mradi wa umeme wa REA umetekelezwa kwa asilimia 36 tu ndani ya miaka mitano.

=> CAG Assad: Tunaishukuru Ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge kwa kutusaidia kukamilisha ripoti hii.

=> Prof Assad: Deni la Taifa limeongezeka lakini bado ni himilivu.

=> Prof Assad: Tumewaalika wenyeviti wa kamati za Bunge (PAC na LAAC) lakini hawajaja hapa. Tutawapatia nakala hizi.

=> Prof Assad: Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma.

=> CAG: Neno 'dhaifu' naendelea kusisitiza ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. Na tutaendelea kulitumia.

=> Prof Assad: Kampuni ya Uhuru Publications haina mfumo mzuri wa udhibiti wa fedha.
Mwenyezi Mungu akupe uwezo mkubwa zaidi wa kusimamia maslahi ya wanyonge mtukufu CAG.
Mioyo ya wananchi ilikuwa inakufa lakini sasa imepata mwanga mpya kutoka kwako.
Mungu mbariki bwana huyu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taifa hili lishukuru kuwa na kiongozi muadilifu CAG Assad, anayefanya kazi kwa haki, na kuwafahamisha bila kuficha walipa kodi matokeo ya tathmini za ukaguzi wao.
 
View attachment 1067472
View attachment 1067459

Wakuu,

Mnaweza kuipakua ripoti kamili hapa:

Lakini, endapo tovuti itakuwa na shida basi naambatanisha hapa mafaili yote

NB: Ripoti imesainiwa na Prof. Assad

Kwa ufupi...

BUNGENI Ofisi ya CAG imetisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma. Inatarajiwa kuwa CAG, Prof. Mussa Assad, atawaeleza waandishi wa habari kuhusu mukhtasari wa kile kilichomo kwenye ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka 2017/18.

Miaka iliyopita, CAG alikuwa anatoa mukhtasari huo kwa waandishi wa habari bungeni mara tu baada ya ripoti yake kuwasilishwa kwenye chombo hicho.
Bunge limeshaazimia kutofanya kazi na Prof. Assad, hivyo ni wazi kwamba hawezi kuzungumza na waandishi wa habari bungeni.

=> CAG assad: Tumezoa kufanya mkutano huu mara tu baada ya ripoti hii kuwasilishwa.

=> CAG assad: Mimi nimetazama kwa TV ripoti imewasilishwa bungeni na 'order paper' (karatasi yenye orodha ya shughuli za kikao cha Bunge) ninayo hapa inaonyesha ripoti imekabidhiwa bungeni leo asubuhi na nimetazama ikiwasilishwa.

=> Prof Assad: Mwaka huu tumetoa ripoti yetu kwa CD ili kuepuka gharama nyingi za uchapishaji.

=> Prof Assad: Mapendekezo yetu tuliyotoa katika ripoti iliyopita yalikuwa 350 lakini ni 80 tu yaliyotekelezwa kikamilifu.

=> Prof Assad: Serikali kuu kulikuwa na mapendekezo 91, mawili tu ndiyo yametekelezwa kikamilifu.

=> Prof Assad: Halmashauri za Kigoma Ujiji na Nyng'wale zimepata hati zisizoridhisha na hati mbaya katika mwaka wa fedha 2017/18.

=> CAG Assad: Tumebaini kuwapo kwa malipo hewa ya mabilioni ya shilingi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

=> Prof Assad: Pia tumebaini Wilaya ya Hanang' haikuwasilisha vitabu vya fedha na kuna upotevu wa mapato ya Sh. bilioni 1.4 na walilipa fedha kwa wakandarasi kwa kazi ya dharura pasipo kuwapo kwa kazi ya dharura.

=> Prof Assad: NEC ilinunua BVR 8,000 lakini mashine 5,000 kati ya hizo zilikuwa haziendani na mfumo uliotakiwa hivyo kuisababisha serikali hasara ya mamilioni ya shilingi.

=> Prof Assad: Kuna mafunzo kwa maofisa wa NEC hayakufanyika licha ya mzabuni kulipwa.

=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lililipa Sh. bilioni 16 kwa ajili ya ununuzi wa sare za polisi bila kuwapo kwa ushahidi wa ununuzi.

=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lilipa Sh. milioni 600 kwa ajili ya mafunzo ambayo hayakufanyika.

=> CAG Assad: Tumebaini Chadema ilinunua gari jipya aina ya Nisan Patrol kwa Sh milioni 147.5 lakini lililisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya Wadhamini.

=> CAG Assad: Tumebaini CCM haijawasilisha NSSF makato ya Sh. bilioni 3.74 ya wanachama wake.

=> CAG Assad: Majengo ya ofisi za CUF yamesajiliwa kwa majina ya watu badala ya Bodi ya Wadhamini.

=> CAG Assad: Kuna miradi 27 serikali za mitaa imekamilika lakini haitumiki licha ya kugharimu mabilioni ya shilingi.

=> Prof Assad: Tumebaini mashirika 14 yana matatizo makubwa ya kifedha na yanaendelea kutengeneza madeni makubwa.

=> CAG Assad: Tumebaini mradi wa umeme wa REA umetekelezwa kwa asilimia 36 tu ndani ya miaka mitano.

=> CAG Assad: Tunaishukuru Ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge kwa kutusaidia kukamilisha ripoti hii.

=> Prof Assad: Deni la Taifa limeongezeka lakini bado ni himilivu.

=> Prof Assad: Tumewaalika wenyeviti wa kamati za Bunge (PAC na LAAC) lakini hawajaja hapa. Tutawapatia nakala hizi.

=> Prof Assad: Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma.

=> CAG: Neno 'dhaifu' naendelea kusisitiza ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. Na tutaendelea kulitumia.

=> Prof Assad: Kampuni ya Uhuru Publications haina mfumo mzuri wa udhibiti wa fedha.
wewe huna akili za kuelewa ripoti ya CAG Mkuu uwezo wako wewe ni uzushi , majungu na umbea
 
Mm ni mtumishi katika wilaya fulan hapa TZ. Naomba kuuliza wanajukwaa hivi CAG anakagua na idara na taasisi zilizopo chini ya halmashauri zetu mfano shule za serikali msingi na sekondari na vituo vya afya, zahanati au hospitali kwani kuna manunuzi katika hizo taasisi nimeshudia ukiukwaji mkubwa wa sheria ya manunuzi unavyofanywa ni balaa. Je CAG huwa anakagua na hizi taasisi au ni lini ataanza kukagua?
 
1068155
 
Assad badala ya kuwa mwanataaluma wa kutoa facts za mahesabu ya serikali, yeye amekuwa mwanasiasa wa kukosoa bunge. Assad siyo CAG wa kwanza Tanzania, wamekuwapo wengi sana waliomtangulia lakini yeye naona kawa wa kwanza kufanya kazi ya CAG kuwa ni political. Angetoa facts halafu awaachie wanasiasa washindane kuliko yeye mwenyewe ndiye kuwa kinara wa malumbano. Wakati mwingine anasababisha hata hesabu zake zitiliwe mashaka kwa vile anakuwa kama ana agenda binafsi !!.
 
Huyu profesa ni moja ya watu wachache waliobaki wnaotumia elimu yao vizuri, wengine wote ni kama hawakusoma wamegeuka kua cult. Jamaa anawapa makavu iwe bunge, rais, ccm, chadema ukibugi anakwambia ukweli bila kuficha.
 
Back
Top Bottom