Los técnicos
JF-Expert Member
- Sep 14, 2014
- 3,012
- 2,637
Mwenyezi Mungu akupe uwezo mkubwa zaidi wa kusimamia maslahi ya wanyonge mtukufu CAG.View attachment 1067472
View attachment 1067459
Wakuu,
Mnaweza kuipakua ripoti kamili hapa:
National Audit office of Tanzania (NAOT)
The National Audit Office (NAO) is an independent Parliamentary body in Tanzania which is responsible for auditing central government departments, government agencies and non-departmental public bodieswww.nao.go.tz
Lakini, endapo tovuti itakuwa na shida basi naambatanisha hapa mafaili yote
NB: Ripoti imesainiwa na Prof. Assad
Kwa ufupi...
BUNGENI Ofisi ya CAG imetisha mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma. Inatarajiwa kuwa CAG, Prof. Mussa Assad, atawaeleza waandishi wa habari kuhusu mukhtasari wa kile kilichomo kwenye ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka 2017/18.
Miaka iliyopita, CAG alikuwa anatoa mukhtasari huo kwa waandishi wa habari bungeni mara tu baada ya ripoti yake kuwasilishwa kwenye chombo hicho.
Bunge limeshaazimia kutofanya kazi na Prof. Assad, hivyo ni wazi kwamba hawezi kuzungumza na waandishi wa habari bungeni.
=> CAG assad: Tumezoa kufanya mkutano huu mara tu baada ya ripoti hii kuwasilishwa.
=> CAG assad: Mimi nimetazama kwa TV ripoti imewasilishwa bungeni na 'order paper' (karatasi yenye orodha ya shughuli za kikao cha Bunge) ninayo hapa inaonyesha ripoti imekabidhiwa bungeni leo asubuhi na nimetazama ikiwasilishwa.
=> Prof Assad: Mwaka huu tumetoa ripoti yetu kwa CD ili kuepuka gharama nyingi za uchapishaji.
=> Prof Assad: Mapendekezo yetu tuliyotoa katika ripoti iliyopita yalikuwa 350 lakini ni 80 tu yaliyotekelezwa kikamilifu.
=> Prof Assad: Serikali kuu kulikuwa na mapendekezo 91, mawili tu ndiyo yametekelezwa kikamilifu.
=> Prof Assad: Halmashauri za Kigoma Ujiji na Nyng'wale zimepata hati zisizoridhisha na hati mbaya katika mwaka wa fedha 2017/18.
=> CAG Assad: Tumebaini kuwapo kwa malipo hewa ya mabilioni ya shilingi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
=> Prof Assad: Pia tumebaini Wilaya ya Hanang' haikuwasilisha vitabu vya fedha na kuna upotevu wa mapato ya Sh. bilioni 1.4 na walilipa fedha kwa wakandarasi kwa kazi ya dharura pasipo kuwapo kwa kazi ya dharura.
=> Prof Assad: NEC ilinunua BVR 8,000 lakini mashine 5,000 kati ya hizo zilikuwa haziendani na mfumo uliotakiwa hivyo kuisababisha serikali hasara ya mamilioni ya shilingi.
=> Prof Assad: Kuna mafunzo kwa maofisa wa NEC hayakufanyika licha ya mzabuni kulipwa.
=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lililipa Sh. bilioni 16 kwa ajili ya ununuzi wa sare za polisi bila kuwapo kwa ushahidi wa ununuzi.
=> Prof Assad: Jeshi la Polisi lilipa Sh. milioni 600 kwa ajili ya mafunzo ambayo hayakufanyika.
=> CAG Assad: Tumebaini Chadema ilinunua gari jipya aina ya Nisan Patrol kwa Sh milioni 147.5 lakini lililisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya Wadhamini.
=> CAG Assad: Tumebaini CCM haijawasilisha NSSF makato ya Sh. bilioni 3.74 ya wanachama wake.
=> CAG Assad: Majengo ya ofisi za CUF yamesajiliwa kwa majina ya watu badala ya Bodi ya Wadhamini.
=> CAG Assad: Kuna miradi 27 serikali za mitaa imekamilika lakini haitumiki licha ya kugharimu mabilioni ya shilingi.
=> Prof Assad: Tumebaini mashirika 14 yana matatizo makubwa ya kifedha na yanaendelea kutengeneza madeni makubwa.
=> CAG Assad: Tumebaini mradi wa umeme wa REA umetekelezwa kwa asilimia 36 tu ndani ya miaka mitano.
=> CAG Assad: Tunaishukuru Ofisi ya Rais na Ofisi ya Bunge kwa kutusaidia kukamilisha ripoti hii.
=> Prof Assad: Deni la Taifa limeongezeka lakini bado ni himilivu.
=> Prof Assad: Tumewaalika wenyeviti wa kamati za Bunge (PAC na LAAC) lakini hawajaja hapa. Tutawapatia nakala hizi.
=> Prof Assad: Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma.
=> CAG: Neno 'dhaifu' naendelea kusisitiza ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. Na tutaendelea kulitumia.
=> Prof Assad: Kampuni ya Uhuru Publications haina mfumo mzuri wa udhibiti wa fedha.
Mioyo ya wananchi ilikuwa inakufa lakini sasa imepata mwanga mpya kutoka kwako.
Mungu mbariki bwana huyu
Sent using Jamii Forums mobile app