Ripoti ya CAG 2021/2022. ATCL, NHIF, Deni la Taifa, Vyura wa Kihansi, risiti za kielektroniki, Biswalo. Vyazua Mjadala

Ripoti ya CAG 2021/2022. ATCL, NHIF, Deni la Taifa, Vyura wa Kihansi, risiti za kielektroniki, Biswalo. Vyazua Mjadala

Magufuli alikuwa anamchukia Assad. Sasa Magufuli ameondoka tuone jambo gani litawafika hawa watu wanaotiliwa mashaka na CAG.
Je,watu wanayo appetite ya hawa vigogo kusakwa mmoja baada ya mmoja na kutiwa pingu?
 
Tuna taka ukaguzi wa ofisi zifuatazo 1. Ikulu 2. TANROAD 3. TANESCO 4. Wizara(Maji, Fedha, Nishati, Ujenzi na Afya)
 
Hii nchi yetu ngumu sana aisee.

CAG anatusomea mambo ambayo yataishia hewani tu without any action.

Ukiwa na serikali zinazoingia madarakani kwa kunajisi chaguzi, tegemea mifumo ya nchi hiyo kufubaa, moja wapo ni hilo la ripoti za fedha kutofanyiwa kazi ipasavyo.
 
Haya mambo bora hata wangekuwa hawatuambii.
 
Adhabu iliishia hapo
Huyu hapendelei kutia watu kwenye roba au mlitaka afanye hivyo? Rais ameagiza Taasisi husika kuchukua hatua mnasema hajachukua hatua! Mlitaka avae mavazi ya Jaji awahukumu watu?

STUPID
 
Leo April 06, 2023 mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali, Charles Kichere ameongea na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Miongoni mwa mambo muhimu
CAG amewashukuru waandishi wa habari, wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge kwa kujimuika katika uwasilishaji wa taarifa hiyo. CAG amesema aliwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa Rais kwa mujibu wa katiba na leo zimewasilishwa Bungeni hivyo kuzifanya kuwa nyaraka zinazoweza kusambazwa kwa umma. Leo anatoa taarifa ya yaliyomo kwa ufupi.

Ripoti 22
CAG amesema aliwasilisha kwa Rais jumla ya ripoti 22 zikijumuisha mambo mambo mbalimbali kwa taasisi zilizokaguliwa na CAG miongoni zikiwemo ripoti ya Serikali kuu, TAMISEMI, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na nyinginezo.

Hati 1010 kati ya 1045 zinaridhisha(96.6%)
CAG ametoa jumla ya hati 1045 kwa mwaka wa fedha 2021/22. Katika hizo, hati zinazoridhisha ni hati 1010 sawa na asilimia 96.6, hati zenye shaka ni 29(2.78%) na hati mbaya ni 3(0.29%) na hati tatu zilizoshindikana kutoa maoni.

Malipo ya Bilioni 25.95 hayana risiti za kielektroniki
CAG ameona malipo bila kuomba risiti za kielekroniki ya Bilioni 25.95 kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Serikali, CAG amesema inadhohofisha juhudi za Serikali katika kukusanya kodi, wafanyabiashara wanaweza kutumia mwanya huu kukwepa kodi.

CAG amerejea ushauri wa awali wa maafisa masuuli wanapaswa kufanya shughuli na wafanyabiashara ambao wana mashine za risiti na kudai risiti za kielektroniki kwa mujibu wa sheria za kodi.

Ucheleweshaji malipo umesababisha riba ya bilioni 418.77
CAG amesema alibaini ucheleweshaji wa malipo na kuzaa riba ya bilioni 418.77 katika taasisi mbalimbali za Serikali. CAG amesema haya ni malipo yasiyo na tija na kuiingiza Serikali hasara. Sababu za ucheleweshaji inajumuisha mchakato wa malipo kuchukua muda mrefu bila kuzingatia mkataba.

Dawa za bilioni 3.5 muda wa matumizi ulikwisha bila kutumika
CAG alibaini baada ya kukagua rejesta katika hospitali dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya bilioni 3.5, hatari yake kuangukia kwa watu wasio waaminifu.

Pia bohari kuu ya dawa ina dawa zenye thamani ya milioni 235.84 zilizokwisha muda wake kabla ya kusambazwa.

Magari yenye thamani ya bilioni 35.29 hayajapokelewa
Magari yenye thamani ya bilioni 35.29 yaliyonunuliwa kupitia wakala wa huduma wa ununuzi Serikalini yalikuwa hayajapokelewa mpaka mwezi wa 12 wakati wanamalizia ukaguzi.

Mfuko wa wanawake, vijana na wenye ulemavu - Bilioni 88. 4 hazijakusanywa
Mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, mamlaka 180 za Serikali za mitaa zimeshindwa kukusanya bilioni 88.42 za mikopo iliyotolewa kutokana na kukosekana ujuzi, udhaifu kwenye upembuzi, udhaifu katika ufuatiliaji wa mikopo.

Mifumo ya usalama na utambuzi wa moto haifanyi kazi Uwanja wa Mkapa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG), Charles Kichere amesema “Nimebaini mapungufu kadhaa kuhusiana na utendaji wa Uwanja wa Mkapa, ambayo yanahitaji usimamizi makini.”

Ameongeza “Nimebaini miundombinu na vifaa duni, viti vimevunjika na havijarekebishwa, hali isiyoridhisha kuhusu miundombinu ya choo, hii inaweza kuleta athari za kiafya kwa watumiaji na kuathiri mapato."

Amesema “Viyoyozi hazifanyi kazi vizuri, usambazaji wa maji na mfumo wa usafi haufanyi kazi kwa njia inayoridhisha, mifumo ya usalama haifanyikazi kama wa utambuzi wa moto na wa tahadhari haifanyi kazi.”



Nitumie Copy la Report Mkuu
 
Kwa Report wanayo muda mrefu wangekuja na njia zilizochukuliwa wanasoma Report huku wezi wakisikiliza wakiwa Nje wakimcheka CAG maana wanajua hakuna kitakachofanyika...
 
Mbona arudia tena kusoma ripoti ileile?

Alipaswa kujiandaa kuja kujibu masuali mbalimbali ya waandishi na wapashaji habari.

Waandishi na wapashaji habari walipaswa kuja na masuali ambayo yametokana na kuchambua ripoti hiyo.

Hii nchi ngumu hii.
Waandishi na hao uliowaita "wapashaji" hasingeweza kufanya uchambuzi wa ripoti wasiyonayo, leo ndio imekuwa wazi kwa umma hivyo itachambuliwa sasa. Na kuhusu maswali, hasa hiyo ripoti ndiyo maswali yenyewe. Wanaotakiwa kuulizwa ili wajibu ni serikali.
 
Ucheleweshaji malipo umesababisha riba ya bilioni 418.77
CAG amesema alibaini ucheleweshaji wa malipo na kuzaa riba ya bilioni 418.77 katika taasisi mbalimbali za Serikali.
Kwa mtindo huu watanzania nawaambia hivi hatutoboi.
 
Back
Top Bottom