Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?

Walio usika na walio sababishia taifa hasara kwa uzembee yao wafikishwa kweny vyombo vya sheria ili wapate haki yao.
 
Petro E. Mselewa
Bw Petro , hapo kuna maigizo tu kwenda mbele, sidhani kama kuna nia njema

1. Kwanini Wabunge hawakukemea ''ufujaji' pesa kwa malipo ya Wenza wa Viongozi?

Yaani wenza wanafurahisha ndani ya nyumba tunazolipia kodi halafu tunawapa mafao ya kukidhi matamanio yao! Huu ufisadi upo Tanzania, Wabunge walikaa kimya. Ufisadi wa kulipa Wapenzi mafao!

2. Taarifa ya CAG ipo, Sirro IGP anatuhuma za Bilioni 4 akiwa signatory, anasema askari katoweka.
Sirro aliwaambia Watu serikali ina mkono mrefu hakuna anayeweza kujificha hata nje ya nchi.
''Aliyeingia ofisini kwakwe'' akakwapua Bilioni 4, Sirro yule yule wa I hajui mwizi yupo wapi na hawezi kumkamata

Sirro kazawadiwa Ubalozi ili akajifiche kwasababu moja tu '' kufichiana madhambi'' .
Sirro anajua uhalaifu wote dhidi ya Wananchi watamshtaki vipi? Mbona hajaitwa kuhojiwa?

Tena alizaiwadiwa V8 licha ya ku sign bilioni 4 , mtu akatoweka nazo

Waziri Mchengerwa kasimamia Wakurugenzi wa Halmashauri. Uonevu tu! mbona hatusikii SGR
Hakuna Mbunge aliyepata jibu la KADCO. Spika kalificha hilo kwa maelezo ya ' kutatolewa taarifa na mawziri''

Halafu mawaziri ambao ni Wabunge wanatetea ufisadi eti pesa zimekwenda nyingi majimboni.
Kwamba zilizoibwa si kitu muhimu zipo zilizowafikia.

Waziri mwingine anasimama kupingana na Rais. Mh Rais kasema ripito ya CAG ina wizi ''stupid'
Waziri katika ofisi yake anateta wezi akisema serikali inafanya vizuri. Yaani kuibwa ni jambo jema kwake

Miaka 60 ni CCM, na hakuna mwaka CAG hajatoa mauza uza. Hivi tumesahau vijisenti na mboga mboga!

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Chini ya serikali sikivu na imara ya Dr.SSH.ni imani ya waTanzania walio wengi kwamba,
hakuna muhuusika hata moja alie tajwa kwenye report ya CAG na kulalamikiwa na waheshimiwa wabunge atasalimika na mkono wa Sheria, wote watawajibika na kuwajibishwa kulingana na makosa yao...
Usikivu wa serikali na Samia mwenyewe ni upi? Hii ripoti siyo mpya, Samia anayo siku nyingi, je amekuwa akisubiri nini kuchukuwa hatua kwa wahusika? Hakuna cha kuwajibishana hapo, imepita hiyo, hakuna Cha serikali sikivu wala Samia imara.
 
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG).

Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye Ripoti ya CAG. Wabunge wamesikika hata wakishauri adhabu kali wapewe wahusika.

Bunge limehitimisha mjadala wa Ripoti husika. Nini kitafuata? Wahusika wa ufisadi na ubadhirifu huo mkubwa watafanywa nini na ni nani hasa mchukua hatua hizo?

Kiukweli, sisi walipa kodi wa nchi hii tungependa kuona hatua kali zinachukuliwa dhidi ya mafisadi na wabadhirifu waliotajwa au kuhusishwa na mambo hayo ndani ya Ripoti ya CAG.

Tunalipa kodi kwa maendeleo yetu. Kutumiwa isivyo kwa kodi na wale tuliowapa dhamana ya matumizi ya kimaendeleo ya kodi zetu kunaumiza sana. Tunatamani na kutaka hatua zichukuliwe. Wabunge wameona na kusema; wachukua hatua wafanye hivyo.
Mkuu Petro E. Mselewa, kwanza asante kwa bandiko hili Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?
Very objective, mimi msimamo wangu kuhusu Bunge letu, kwenye hoja ya bunge kuisimamia serikali, bado haujabadilika ni ule ule wa bunge lililopita Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?
Na hapa Je, Bunge letu ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza lenye meno linavyong'ata Serikali. Je, Kuna ubaya tukiiga?
Japo Rais Samia ametoa maelekezo makali kwa maofisa masuhuli, hii ni kesi ya nyani kumpelekea ngedere!.
Kilichopaswa kufanywa on the first place ni kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG, alipaswa apishe kwanza, akiwa cleared ndipo arudishwe!.
P
 
Yaan unavyoandika naona moyoni unavyoweweseka na unachokiandika
 
sure,
naweweseka sana kwasababu hakuna yeyote alietajwa kwenye repoti ya CAG hata moja, ambae yuko salama.
Lazima hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.
wanachi wanashauku na wana imani na serikali sikivu chini ya Rais Dr.SSH...
 
Usikivu wa serikali na Samia mwenyewe ni upi? Hii ripoti siyo mpya, Samia anayo siku nyingi, je amekuwa akisubiri nini kuchukuwa hatua kwa wahusika? Hakuna cha kuwajibishana hapo, imepita hiyo, hakuna Cha serikali sikivu wala Samia imara.
Usikivu wa Dr.SSH unadhirika zaidi na uko wazi na bayana.
Taifa ni tulivu haijawahi kutokea, ulinzi na usalama ni madhubuti kupindukia, uhuru wa maoni, habari na uwazi serikalini ni vya kupigiwa mfano, umoja na utangamano miongoni mwa waTanzania imeimarika mara dufu.

Kwenye Maendeleo sasa heheeheee,
Dr.SSH anaonekana kwa uwzi zaidi kwenye maji, afya, elimu, kilimo, biashara,miundombinu, michezo, usafirishaji nakadhalika nakadhalika dah.....
unamkosa wapi na kenye nini Dr. SSH nchin Tanzania.....
 
Ngoja tuone,kama kuna usikivu upande wa Serikali,kwasababu sauti ya bunge ni sauti ya wananchi,kudharau maoni ya bunge ni kutudharau sisi wananchi

Kwani bunge limeanza kipindi hiki?

Ripot ya CAG hii ni ya kwanza? Ama hizo za nyuma zilikuwa nzuri?

Usisubiri kuona kipya.
 
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG).

Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye Ripoti ya CAG. Wabunge wamesikika hata wakishauri adhabu kali wapewe wahusika.

Bunge limehitimisha mjadala wa Ripoti husika. Nini kitafuata? Wahusika wa ufisadi na ubadhirifu huo mkubwa watafanywa nini na ni nani hasa mchukua hatua hizo?

Kiukweli, sisi walipa kodi wa nchi hii tungependa kuona hatua kali zinachukuliwa dhidi ya mafisadi na wabadhirifu waliotajwa au kuhusishwa na mambo hayo ndani ya Ripoti ya CAG.

Tunalipa kodi kwa maendeleo yetu. Kutumiwa isivyo kwa kodi na wale tuliowapa dhamana ya matumizi ya kimaendeleo ya kodi zetu kunaumiza sana. Tunatamani na kutaka hatua zichukuliwe. Wabunge wameona na kusema; wachukua hatua wafanye hivyo.
Subiria MV kivukoni JNIA mkuu
 
Cha kwanza ilitakiwa Baraza la Mawaziri livunjwe na baadhi wakamatwe na kufikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi haswa hawa(Majaliwa, Makamba, Ummy, Bashe, Mwigulu, Nape, Angela, Aweso, Kijachu, Jafo, Mbarawa na Masauni).
Subutu ..imetaja mgongo wa CCM .
 
Mkuu Petro E. Mselewa, kwanza asante kwa bandiko hili Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?
Very objective, mimi msimamo wangu kuhusu Bunge letu, kwenye hoja ya bunge kuisimamia serikali, bado haujabadilika ni ule ule wa bunge lililopita Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?
Na hapa Je, Bunge letu ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza lenye meno linavyong'ata Serikali. Je, Kuna ubaya tukiiga?
Japo Rais Samia ametoa maelekezo makali kwa maofisa masuhuli, hii ni kesi ya nyani kumpelekea ngedere!.
Kilichopaswa kufanywa on the first place ni kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG, alipaswa apishe kwanza, akiwa cleared ndipo arudishwe!.
P
P hivi nani hajui kwamba Bilioni 4 za Polisi anayeidhinisha ni IGP. Badala ya kumleta ajibu, anazawadiwa Ubalozi.

Wizara ina Waziri, naibu Waziri, Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo kuanzia makao makuu hadi Wilayani.
Wizara ina internal auditor.
Hivi watu hawa wote inawezekanaje kwa miezi 11 wasione wezi eti mwezi wa 12 CAG anakuja kuona madudu?

Shirika lina CEO na Board halafu internal auditor, eti wote hawa hawajui wizi hadi CAG aje kufichua mauza uza

Halafu si huyu Spika alisema kazi ya Bunge ni kumsaidia Rais!

Kama kweli wapo serious kuna mambo ya kufanya
1. Futa kazi vigogo siyo vidagaa halafu wafikishe mahakamani
2 Wakikutwa na hatia Taifisha mali zao
3. Wizara yenye uozo, Waziri awajibike mara moja
4. CEO mwenye mauza uza futilia mbali yeye na Board yake, wachunguzwe na ikibainika wafilisiwe
5., Taarifa za Bunge ziwe wazi siyo Spika afiche kama tunavyoona

Vinginevyo ni kudanganyana tu, ni maigizo pale Dodoma !
 
sure,
naweweseka sana kwasababu hakuna yeyote alietajwa kwenye repoti ya CAG hata moja, ambae yuko salama.
Lazima hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.
wanachi wanashauku na wana imani na serikali sikivu chini ya Rais Dr.SSH...
Hata hao ccm wenyewe hawana imani nae
 
We jitoe ufahamu ila ndo ushanielewa
sasa endelea kuamini wanadamu upate makwazo na maradhi ya Moyo.

Amini Mungu, na umtumainie yeye pekee.
Jiombee wewe mwenyewe na uwaombee maadui zako na watenda maovu wote ikiwa ni pamoja na mafisadi na Utabarikiwa
 
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG).

Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye Ripoti ya CAG. Wabunge wamesikika hata wakishauri adhabu kali wapewe wahusika.

Bunge limehitimisha mjadala wa Ripoti husika. Nini kitafuata? Wahusika wa ufisadi na ubadhirifu huo mkubwa watafanywa nini na ni nani hasa mchukua hatua hizo?

Kiukweli, sisi walipa kodi wa nchi hii tungependa kuona hatua kali zinachukuliwa dhidi ya mafisadi na wabadhirifu waliotajwa au kuhusishwa na mambo hayo ndani ya Ripoti ya CAG.

Tunalipa kodi kwa maendeleo yetu. Kutumiwa isivyo kwa kodi na wale tuliowapa dhamana ya matumizi ya kimaendeleo ya kodi zetu kunaumiza sana. Tunatamani na kutaka hatua zichukuliwe. Wabunge wameona na kusema; wachukua hatua wafanye hivyo.
Igizo ndiyo limeishia hapo subiri episode nyingine
 
Back
Top Bottom