Taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) zimeivua nguo serikali ya awamu ya tano iliyokuwa chini ya Dikteta John Magufuli.
Angalau sasa watanzania wanajifunza jambo moja; faida za uhuru wa habari.
Dikteta Magufuli alidhibiti vyombo vya habari kwa kutunga sheria ngumu zilizowanyima wakosoaji wa serikali uhuru wa kuchapisha habari. Ilibidi vyombo vya habari vitoe taarifa nzurinzuri za kumpendeza Dikteta Magufuli.
Shirika la habari la Taifa (TBC) likaongoza ngonjera za kumsifu Dikteta Magufuli.
Mashirika binafsi ya habari yakaitikia kwa beti za kusifu na kumpamba Dikteta Magufuli.
Chombo cha habari kilichochapisha taarifa zisizopendeza kilishughulikiwa.
Tafsiri ya uzalendo ikawa kumsifu Dikteta Magufuli, kuandika habari za kupendeza hata kama ni za uongo na kuficha madudu ya serikali. Huo ndio uzalendo wa nyakati za Dikteta Magufuli.
Waliotaka kuutafuta ukweli, walikiona cha mtema kuni. Walitekwa na kupotezwa. Ukweli ungepatikana, nani angemsifu Dikteta Magufuli kwa nyimbo na mapambio?
Propaganda za kusifu zilibamba kwelikweli. Watu wakaaminishwa kwamba eti Magufuli amefanya mambo makubwa ndani ya muda mfupi. Wajinga ambao ni wengi wakaamini kwamba hakuna Rais aliyewahi kufanya makubwa zaidi ya Dikteta Magufuli.
Yote hayo ni kwa sababu wanahabari walitakiwa kuandika hayo. Aliyethubutu kuandika kinyume aliandamwa na vitisho, makaripio na hata kufanyiwa mambo yasiofaa kwa utu.
Lakini sasa Dikteta Magufuli hayupo.
Tumejua; kumbe alibinya uhuru wa habari ili wananchi wapate habari za kumpamba tu na sio zile zinazomchafua hata kama zina ukweli.
Kama kungelikuwa na uhuru wa habari, yapo mambo ambayo kama yangesemwa hadharani, yangepigiwa kelele na serikali ingechukua hatua (hata kwa aibu tu) kuyarekebisha. Taarifa za CAG zimeonesha ufisadi wa kihistoria ndani ya ardhi ya Tanzania baada ya Dikteta Magufuli kuondoka. Laiti kama angekuwa hai, pengine tusingepata taarifa hizi za ufisadi.
Bashiru hana raha, hana amani kutokana na kuhusishwa na madudu kadhaa kwenye ugonjwa na msiba wa mwendazake. Yeye anajitetea mbele ya wazee wastaafu na maprofesa wastaafu kuwa Mwanasheria Mkuu (AG) ndiye aliwapotosha msiba ulipotokea.
Aliwashauri wenzake kwamba mambo ya kumwapisha Samia kuwa rais yangeweza kufanyika baada ya mazishi. Kauli hiyo ikatafsiriwa kuwa yeye Bashiru anathubutu kuzuia Samia kuwa rais. AG akakaa kimya kabisa. Bashiru amemchukia sana AG. Kunahitaji upatanisho.
Bashiru anakana kuhusika na ukwapuaji wa fedha BoT. Kumekuwa na tuhuma kuwa yeye, Mpango, Dotto na Dr. Mchembe (daktari wa JPM) walichota fedha BoT wakati wa ugonjwa na msiba wa JPM. Samia aliagiza ripoti ya ukaguzi toka kwa CAG inayoonyesha matumizi Kati ya Jan na Machi.
Uteuzi wa Bashiru kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ulitia shaka. Yeye anadai hakuwa consulted na JPM. Alimwita usiku kumwambia kesho yake anamteua. Na siku ya kuapishwa, JPM alikuwa tayari anaumwa. Alitokea kwenye drip kuja kumwapisha. Baada ya kuapishwa Bashiru hakukutana naye tena
Kwa muda ambao JPM hajazidiwa kabisa, Bashiru alikuwa anapewa maelekezo yote kwa simu.
Bashiru anadai kuwa alilalamika kwa JPM kwamba watu, hata ndani ya chama chake, wananung'unika kuwa anamuandaa kuwa mgombea 2025; JPM akajibu, "kuna ubaya gani?"
Bashiru anawaambia baadhi ya mabalozi rafiki zake na maprofesa wa UDSM kuwa ni kweli JPM alizungukwa na "majizi na majambazi" ndani na nje ya Ikulu; kwamba JPM alishayajua lakini hakuweza kuyashughulikia kwa vile alishawekeza muda na mali kuyajenga na kuyatetea hadhrani.
Dk Mchemba alikuwa daktari wa JPM siku za mwisho akichukua nafasi ya Dk Ng'wale aliyehamishiwa kwa First Lady. Alikuwa CEO wa Hospital ya Mzena. Pia ni ofisa TISS. Alishika nafasi zote 3 kwa amri ya JPM. Alienda BoT na Dotto wakiwa na saini ya Mpango wakamzonga Gavana.
Taarifa zinasema tayari Dk Mchemba amefutwa kazi na amenyang'anywa kitambulisho cha TISS baada ya "kusota ndani."
Hapo hapo kuna bifu la Bashiru dhidi yaMufti Mkuu. Bashiru anadai kuwa wakati serikali inasita kutangaza msiba wa JPM, Mufti alitumia vibaya muda huo Mufti Zubeir alikuwa rafiki wa JPM. Na alimtumia katika mengi. Baada JPM kufariki dunia, kabla ya kifo kutangazwa, Dk. Mchembe na kundi lake walimdanganya Mufti awasaidie kumshauri Samia ajiuzuru umakamu kwa hoja kuwa JPM akitoka hospital anamfukuza kazi bila kujali katiba
Walitaka Samia kwanza ajiuzuru ndipo watangaze msiba, ili apatikane mwanaume mwenzao ashike uongozi wa nchi. Samia alikataa. Ikumbukwe Mufti ndiye alikuwa anatumwa na DPP kwenda mahabusu kushawishi watu wakiri makosa (plea bargain). Wengine walikuwa wanampa hela ampelekee DPP.
Bashiru anamshangaa Samia kwa kumteua DPP kuwa Jaji. Anamuona kama mmoja wa majangili ya utawala wa JPM. Anampongeza Former DGIS Robert Makungu (RAS TABORA) kuwa ni mtu mwadilifu anayefa kuwa DG wa TISS
Kisa, eti Makungu alimheshimu sana JPM ila fitna zilimfanya rais asigundue uadilifu wa Makungu. Bashiru anamlaumu sana Kabudi kwa kumshauri vibaya JPM kuhusu jumuiya ya kimataifa. Ndiye alimzuia rais kumwajibisha Makonda kwa madai kuwa atawapa kiburi Wamarekani
Bashiru anasema kuwa Makonda ni kiumbe mchafu kuliko kitu chochote duniani.
Anatamba kuwa yeye na JPM walirejesha mali za chama na kukusanya mapato makubwa. Waliendesha uchaguzi bila kutegemea misaada ya wafadhili na wakibakiwa na salio zaidi 20bn. kwenye account ya chama
Bashiru anajiandaa kuandika kitabu ili kujisafisha. Anamwona JK kama adui wa taifa. Eti alimzonga sana JPM wakati wote mpaka akatishia kususia Ikulu na kwenda kuishi Chato; na kwamba Rais Museveni ndiye alisaidia "kumrejesha." Kifupi, Bashiru aweza hata kujinyonga! He's stressed!
#SautiKubwa